Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Ukiangalia D.Trump, sera zake zote haziingiliani na maisha yetu kama zilivyo sera za uliberari wengine kama Obama,Clinton &Co. hivyo nashindwa kuelewa kwa nini Waafrika walio wengi tena wale waishio Afrika hawampendi Trump badala yake wanampenda Obama na Clinton!
Tuangalie sera za Trump kwa kifupi, yuko dhidi ya ndoa za jinsia moja hivyo kutakuwa hakuna Siasa za kushinikiza nchi za Kiafrika kukubali Ushoga, hakubaliani na utoaji Mimba pasipo na ulazima hapa pia Waafrika tulio wengi tunaunga mkono, hakubaliani na Siasa za USA za sasa za kuvamia kila nchi na kuingilia mambo ya ndani ya nchi ambazo hazihatarishi usalama wa USA moja kwa moja,
Trump hakubaliani na Globalization hapa pia sisi Waafrika ni wahanga wakubwa wa Globalization, sera za IMF na Benki ya Dunia ndizo zilizotufilisi Afrika kwa mfano kwenye madini sisi kupata 3% tu na zaidi ya 95% kuchukuliwa na wageni, Makampuni ya uwekezaji kupewa tax holliday ya miaka 5 na baada ya hapo kuondoka bila ya kulipa kodi yote haya ni sera za Globalization ambazo watu kama Obama na Clinton ndiyo wanazifwata!
Hivyo wewe kama Mwafrika kumchukia Trump ina maana hauipendi Afrika au haujamuelewa na haujui hata unasimamia nini!