Waafrika tusingetawaliwa tungekuwa wapi hii leo?

Nina hakika
Tungekuwa mbali mno katika kila sekta
Wazungu,ndio waliotufanya sisi ni wajinga mbele yao,
Ila kabla ya ujio wao,Waafrika walikuwa na sifa hizi:-
Waaminifu(wengi wao)
Wana utu
Wanajua utawala
Wachapa kazi na Werevu
 
Asikudanganye mtu. Waliokwishafika Ethiopia na Liberia ambazo hazikutawaliwa wanajua tungekuwa wapi. Monrovia city is a very big slum and so is Addis Ababa. Watu wanajisaidia mitaani kama wanyama tu. Mitaa inanuka takamwili. Nchi ambazo zimetawaliwa zina nafuu sana. Na katika zilizotawaliwa, zilizochelea kupata uhuru wake kama Afrika Kusini na Namibia zina nafuu zaidi kuliko zilizowahi kupata km Ghana, Nigeria, Tanzania...
Tungekuwa mbali sana kimaendeleo.
 
Tumia. Akili mkuu hata Waarabu walikua primitive ila hawakutawaliwa na wameendelea sasa kushinda hta sisi
Hizi nchi zetu zingeendelea kwa kubadilika kwa dunia na mifumo ya utawala.
Kwasababu hapa hapa Africa kuna vyuo vikuu vilianza kujengwa na kuna baadhi ya states zilianza kumiliki currency yake yenyewe.
Kwani Ethiopia haikutawaliwa toka enzi ya Mennelick anakataa utawala wa wakoloni mbona now ile pale inasonga mbele ?!
Nilidhani ungesema walikuta shule ngapi, barabara za lami ngapi, vituo vya afya vingapi , vyuo vikuu vingapi...

Sisi waafrica akili zimechacha, maendeleo siku zote tunayapima kwa jicho la siasa ??..
Eti walikuta mfumo mzuri Wa siasa , sasa huo mfumo ulisaidia nini
 
Halafu pima imepata uhuru mwaka gani we nchi toka 1676 ilishapata uhuru lazma ingesimama firmly kiuchumi we sisi tumepata uhuru mwaka 1960 aisee
Marekani imetawaliwa. Tunafanana uchumi,?
 
Hiyo South Africa hadi ssa uchumi wake unashikiliwa na Boers na toka nyuma ulijengwa na boers.
Nchi za kuzisifia zilijiinua kwa mikono yao ya asili ni km Libya toka enzi za Umar Mukhtar mpk enzi za Gaddafi
Afrika kusini imepata uhuru juz juz lkn ina maendeleo kuliko sisi.
Tatizo sio ukoloni
 
Asikudanganye mtu. Waliokwishafika Ethiopia na Liberia ambazo hazikutawaliwa wanajua tungekuwa wapi. Monrovia city is a very big slum and so is Addis Ababa. Watu wanajisaidia mitaani kama wanyama tu. Mitaa inanuka takamwili. Nchi ambazo zimetawaliwa zina nafuu sana. Na katika zilizotawaliwa, zilizochelea kupata uhuru wake kama Afrika Kusini na Namibia zina nafuu zaidi kuliko zilizowahi kupata km Ghana, Nigeria, Tanzania...
Nchi kama Egypt mkuu ilishaanza kuwa na wasomi wake kabla ya.hawa kuku wa kizungu kuja kutawala kuna nchi nyingi tyuuu zilishaanza kusimama mkuu kabla ya kuja wazungu.
Na kuhusu ktk maswala ya kustaarabika waarabu na persians walishaanza kutu civilize kwa mavaz lugha na kiustaarabu mwingine ila hawa majamaa wakaja tifua kila kitu.
Sis tunashindwa kuendelea now au tunachelewa kwasababu ya mkanganyiko wa diplomacy ya kuitumia ktk uongozi.
 
WAAFRIKA TUSINGETAWALIWA TUNGEKUWA WAPI HII LEO? (Maoni tu, Sio Malumbano)

Swali lako zuri lakini lina makosa katika kudhania (assumptions).

a. Marekani na China zote ni nchi zilizowahi kutawaliwa na wengine. Ethiopia na Liberia ni nchi za Kiafrika ambazo hazikutaliwa na nchi nyingine.

b. Kutaliwa peke yake hakuwezi kuwa kipimo cha nchi kuwepo au kutokuwepo katika hali fulani. Na bahati mbaya nchi nyingi ambazo zimekuja kutawala wengine nazo ziliwahi kutawaliwa...

c. Kutaliwa si sababu ya kushindwa kufanya jambo lolote, na kutawala wengine si sababu ya nchi kufanikiwa kuliko nchi nyingine.
 
Swali hili ni swali la manung'uniko! Hasa lingilenga hali ya bara la afrika ilivyo kwa sasa kimaendeleo likilinganishwa na mabara mengine.
"Waafrika" Tusingetawaliwa tungekuwa wapi hii leo? Yaani kutawaliwa kwa bara la afrika imekuwa kama "favour" ya hata kuwa na vijimaendeleo kidogo tulivyo navyo!

Amerika iliwakutawaliwa na Waingereza! Na nchi Nyingi sana Duniani zimewahi kutawaliwa na mataifa tofauti tofauti!
Amerika ilianza kuendelea kwa Kasi baada ya Kujitawala yenyewe, mwingereza alikuwa anachuma na Kujenga London tu.
Je? Unafahamu Afrika ilishawahi kuivamia Ulaya na Kuipiga vibaya? Kabla ya kutawaliwa na Wazungu.

Je unafahamu teknolojia za awali kabisa za uvumbuzi zilipatikana Afrika! - Iron technology! irrigation Skills and etc.Kabla ya kutawaliwa na Wazungu.

Nyakati na Mwamko wa fikra unaweza kubadili hali halisi ghafla! Wakwanza akawa wa mwisho na wa mwisho akawa wa kwanza!
What went wrong?
Tuzidi kupambana na Matamaa ya Madaraka Kisiasa,Kuridhika Mapema na Kukata Tamaa tutawapita haooo.
High Hopes!
 
Tungepitia kipindi fulani cha mpambano Wa makabila hasa watawala wenye nguvu kujaribu kulazimisha watawala dhaifu kuwa chini yako, mfano vita ya Mkwawa Wa wahehe na Melele Wa wasangu, vita hizo zingeibua tawala zenye nguvu kama ilivyofanyika Ethiopia. Ubunifu Wa kutengeneza zana za kisasa ungeimarishwa, na kuimarisha biashara ya ndani na nje
 
Swali lako zuri lakini lina makosa katika kudhania (assumptions).

a. Marekani na China zote ni nchi zilizowahi kutawaliwa na wengine. Ethiopia na Liberia ni nchi za Kiafrika ambazo hazikutaliwa.
ila Marekani bado inatawaliwa na waliokuwa watalawa waliojiengua kutoka mataifa yako mama kiutawala. Ila wenyeji (red Indians wapi kwenye uhuru bandia)
 
Jidanganye tu. Wakoloni walitoka Tanganyika 1961, Ghana 1957, Malaysia 1957, Israel ikawa taifa 1947 nk nk. Leo hii Israel na Malaysia zimeendelea lakini nchi za Kiafrika ziko wapi? Kuna mtu hapa kasema - hapa USA ilitawaliwa - mpaka 1776, Ulaya ilitawaliwa na dola la warumi pia. Lakini baada ya kupata uhuru zilipiga hatua. Nyie mnafikiri maendeleo ni ukiwa meneja wa UDART ni kuiba na kufilisi shirika na kujenga hekalu kubwa kwa ajili ya familia yako. Maendeleo yatatoka wapi kwa attitude za aina hii? Kama hao Wamisri walikuwa wajanja toka zamani, walitawaliwaje? Bila kutawaliwa ungekuwa kama Mhadzabe wa sasa.

Back
Top Bottom