Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Aidha kwa kukubali moja kwa moja au kwa siyo kwa moja kwa moja lkn mwisho wa siku Waafrika tunaamini kabisa kwamba Wazungu ni Super human yaani ni zaidi ya binadamu wa kawaida na chochote wakifanyacho ni sahihi!
Hili utaliona kila mahali, kosa hata liwe kubwa vipi likifanywa na Mzungu basi Waafrika tunaona ni sawa na kuliahalalisha ...
Kwa mfano yule dada ya Kikenya tuliyemdhalilishwa pale Mlimani City kwa kutuhumiwa uwizi nina uhakika 100% kama angekuwa ni Mzungu asingetendewa vile au hata tu kama angekuwa Mwarabu au Muhindi asingepigwa wala asingeguswa na si ajabu tungekwenda mbali zaidi na kumgeukia yule aliyesema Mzungu kaiba na kumpa yeye kibano!
Na kama unabisha au unakataa kama Waafrika hatuwaoni Wazungu ni Super Human fanya hii ,,thought experiment" uko br. unasafiri kwa gari, usiku mkubwa wenye giza nene kati kati ya pori kwenye gari lako kuna nafasi ya mtu mmoja tu, halafu watu wawili wanakuomba lifti mmoja Mzungu mwingine Mwafrika mweusi kama mimi utamchukuwa nani? Au fikiria Kitila Mkumbo, Zito Kabwe, Tundu Lisu Mbowe, Lowasa, Kikwete, mimi na wewe tutamchukuwa nani kati ya hao wawili?
Au kama hiyo haitoshi fikiria Zito Kabwe (hapa natolea tu mfano yeye kama Mwafrika ningeweza kutumia mfano wowote ule) ameoa juzi wewe ukaenda kwenye harusi yake bila ya mwaliko Je, utaingia? Sasa fikiria Mzungu bila ya mwaliko aende na atake kuingia kwenye harusi, Je Walinzi watamrudisha mlangoni kama walivyokurudisha wewe kwa kuwa hana kadi ya mwaliko au watamsikiliza na siajabu hata kumuibua Bwana harusi aje amsikilize?
Lakini hali ikoje kwa wenzetu? yaani Wazungu,Wahindi, Waarabu n.k wanatuonaje?