Waafrika tumefikia kwenye hatua mbaya sana. Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu, wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa

StudentTeacher

JF-Expert Member
Jan 30, 2019
1,987
2,000
Makala hii iliandikwa kwa kiingereza na Mwandishi Kay Musonda na kuchapishwa na jarida la Modern Ghana, toleo no.215 la April 1 mwaka huu. Nimefanya tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili pengine tutapata la kujifunza.
________________
Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo (ulokole). Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajituza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama kina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake kama mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admision' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' kama njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afrika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Wachungaji hawa wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kwa Nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangia kwa kusema Ameen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu kama Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Afrika namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata kama ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote (Mithali 12:27)
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya utani huu kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone kama hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio kama kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi (Kumb 28:6).

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe kama Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanaishi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa (Mithali 1:7). Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika roho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo.
Huu ni uzi bora kabisa kwa mwaka huu. Yatokeapo hayo yanatoa taswira kwamba watu wapo gizani kwa kiwango gani
 

kacnia

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
3,494
2,000
mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama,
ni mafanikio gani aliyapata huyu mtu kiasi cha sisi waafrika kujivunia?

what I know alitumika kuvunja umoja wa Africa uliokuwa katika mchakato pevu chini ya gadafi, na kuforce ushoga na mambo mengi, he is just a black weapon in white hands.

kwa hayo mengine tuko pamoja
 

StudentTeacher

JF-Expert Member
Jan 30, 2019
1,987
2,000
Kwa maelezo yako haya yote, bila shaka wewe ni mhubiri ama mchungaji wa kilokole and the like!

Kada ambayo ndiyo imeongelewa sana na mtoa mada.

Kwa muktadha huo, kiustaarabu kabisa, wewe haukustahili kuchangia chochote, ulipaswa kuwa ni muangaliaji tu wa kinachojadiliwa na wanabodi ili ujifunze usiyoyajua, sababu elimu haina mwisho.

Lakini kuendelea kutulisha tango pori lilelile chungu kwa kulipaka sukari ni tabia ya kudekeza ubishi usiokuwa na manufaa yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ni tango pori haswaaa
 

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
496
1,000
Mimi ni mlokole mzuri tu na ni mzee wa kanisa TAG ila huwa napingana sana na baadhi ya mafundisho na mifumo ya vyuo vya biblia jinsi vinavyo wa shape watu wao.Huwa nawaukiza watu ni kwanini walokole wengi ni masikini??wale walokole wafukutwa...tofaut sana na wakristo huko Kkkt au Rc..MAFUNDISHO ni tatizo sana...
Yan huwa time nyingine unamwangalia mchungaji af unamoima unaona kabisa hapa hamna usalama huko tunapopelekana.
NB
Nimezaliwa Moravian..nimekulia UKWATA.
Hata mimi ni mmoravian mkuu huko nako kumeharibika sana siku hizi yaani ibada nzima inatawaliwa na michango mwanzo mwisho
 

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
496
1,000
Mafanikio hayatokani na bidii tu, yanatokana na bidii iambatanayo na roho wa mafanikio!
Sio kila masikini hana bidii, kuna watu wanabidii ya kazi, ubunifu, na nguvu lakini bado ni masikini!
Ukiambatana na roho wachafu, wabaya, hata usomeje, ubunije, ujibidisheje, hutoboi!
Mkuu hapo sipingani na wewe lkn tambua kuna baadhi ya makanisa hayo ya kinabii watu wanashinda makanisani tangu asubuhi mpaka jioni 24/7
 

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,518
2,000
Mafanikio hayatokani na bidii tu, yanatokana na bidii iambatanayo na roho wa mafanikio!
Sio kila masikini hana bidii, kuna watu wanabidii ya kazi, ubunifu, na nguvu lakini bado ni masikini!
Ukiambatana na roho wachafu, wabaya, hata usomeje, ubunije, ujibidisheje, hutoboi!
Huyo roho wa mafanikio yukoje?
Ndugu, naona unataka kuleta msamiati mpya.
 

nanilii

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
324
500
Yaani Mwenyezi Mungu amesema sana kuwatahadharisha wanadamu , lakini hawsikii, sa si anakuona hujaokoka, kwahiyo wewe utamuambia nini : Mungu anasema ; watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa, tena , jamani siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo - wapi hawasikii,
kuna dhehebu moja Askofu anasafiri na kiti chake, afu wakati wa Ibada inawekwa sauti kuuuuuubwaaa yaani mpaka mimi nilikuwa nawaonea sana huruma wamama walioongozana na watoto chini ya miaka 10. yaani ni kelele hata tulio mbali tunaona shida.
sasa hii yote ni kuwapumbaza waumini kwamba pale ndo kuna Mungu na huyo kiongzo ndiyo '' mwenyewe '' chochote asemacho, kasema Mungu. ( yaani kisaikolojia anakuwa kawateka hasa wa mama) ma sauti hayo makubwa, yaani shida, shiiiiidaa
 

Science Priest

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
2,303
2,000
Mafanikio hayatokani na bidii tu, yanatokana na bidii iambatanayo na roho wa mafanikio

Sio kila masikini hana bidii, kuna watu wanabidii ya kazi, ubunifu, na nguvu lakini bado ni masikini

Ukiambatana na roho wachafu, wabaya, hata usomeje, ubunije, ujibidisheje, hutoboi
Wachina hawaamini kwenye uikristo lakin wameendelea sana ulishajiulizaga
Ili ufanikiwe unatakiwa uwezekeze kwenye kazi na sio kusubiria miujiza
 

Science Priest

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
2,303
2,000
Yaani Mwenyezi Mungu amesema sana kuwatahadharisha wanadamu , lakini hawsikii, sa si anakuona hujaokoka, kwahiyo wewe utamuambia nini : Mungu anasema ; watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa, tena , jamani siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo - wapi hawasikii,
kuna dhehebu moja Askofu anasafiri na kiti chake, afu wakati wa Ibada inawekwa sauti kuuuuuubwaaa yaani mpaka mimi nilikuwa nawaonea sana huruma wamama walioongozana na watoto chini ya miaka 10. yaani ni kelele hata tulio mbali tunaona shida.
sasa hii yote ni kuwapumbaza waumini kwamba pale ndo kuna Mungu na huyo kiongzo ndiyo '' mwenyewe '' chochote asemacho, kasema Mungu. ( yaani kisaikolojia anakuwa kawateka hasa wa mama) ma sauti hayo makubwa, yaani shida, shiiiiidaa
Ni kweli hatujaumbwa tuishi kwa miujiza lakin dini imekua biashara
 

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,217
2,000
Huyo roho wa mafanikio yukoje?
Ndugu, naona unataka kuleta msamiati mpya.
Usichokijua, mtu mmoja anaweza kuishi huku ndani yake kuna roho wengi kwa kazi tofauti tofauti wanaomwendesha mtu huyo! Usifunge ufahamu wako, jiachie usome vyanzo vingine vya maarifa juu ya mambo ktk ulimwengu wa roho!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom