Waafrika ni watu wa ajabu sana mbona huko kwenu watuhumiwa lukuki wanakufa mikononi mwa polisi na mko kimya? kwa shobo hamjambo

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
Tukio la Mmarekani mweusi kuuliwa na Polisi limezuwa gumzo kubwa hadi wa-Afrika kulaani kila muda na kuchukuwa muda mwingi wa wa-Afrika mitandaoni na vijiweni na wengine kutoa mauchungu yao.

Rais wa Ghana naye eti ana laani ?nimecheka sana

Naomba nitoe reference za nchi 2 tu ninazozifahamu Tanzania na Afrika kusini hizi nchi watu weusi wengi hufa mikononi mwa polisi kwa kipigo kikali tena za ukatili kesi mbalimbali za watu kufa vituoni ni vingi familia nyingi wamepata uchungu sababu ya polisi halafu ngekewa anaishi Buza, Mlandizi, Korogwe anatokwa na mishipa kwa kubishana kwa uchungu kisa ya Mmarekani mweusi kuuawa na polisi mbona huko kwenu weusi halisi Africans wanauawa kwa vipigo vikali na wala hamufanyi maandamano mitandaoni kulaani na huwa mnachukulia poa tu.

Rais wa Ghana nimemshusha hadhi huenda huko Ghana kuna familia nyingi zina machungu ya kuondokewa na wapendwa wao sababu ya police brutality na hajawahi kulaani ..
 
Uko sahihi kwa Tanzania kuna matukio mengi na haya ni baadhi tu.

Ben saanane

Aqwilina

Mawazo Alphoce

Mauaji ya kibiti na mengine mengi ya watuhumiwa kuuwawa vituoni kwa kipigo..kiukweli Tanzania kuna mkoloni mweusi.
 
Tukio la Marekani limeaminika upesi kwa sababu kuna watu walirekodi mkanda wa video na hamna chombo chochote ambacho kimepinga uhalisia wa hiyo video. Inawezekana vile vile wana Kamera za barabarani.

Badala ya kuwabeza waandamanaji nafikiri inatakiwa tuwapongeza kwa kujitoa kwao kudai haki ya binadamu mmoja mweusi ambaye ameuwawa kwa makusudi kabisa na askari wa kizungu.

Katika nchi nyingi Kupata picha za matukio kama hayo - si rahisi na pia ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom