Waafrika Kusini walikuwa wamechoshwa na sera za ubaguzi wa rangi

Yussufhaji

Member
Sep 9, 2018
35
28
13/11/2021

Yafaa kusema wakati wa kipindi cha ukingoni cha Afrika Kusini na sera za ubaguzi wa rangi dhidi ya wasio weupe (wasio wazungu) watu wengi nchini humo ukijumuisha na baadhi ya hata wazungu wenyewe walikuwa tayari wameshachoka na sera hizo,

Hatua kali zilizo chukuliwa dhidi ya wanaharakati waliopinga sera za ubaguzi kama kukamatwa ovyo bila ya sababu za msingi, mahakama kukosa haki na uhuru, hatua kandamizi ya vikosi vya ulinzi na usalama dhidi ya wanaharakati hao mfano mauji ya SHARPEVILLE ya mwaka 1960 ambapo zaidi ya 69 walipoteza maisha, pia watu wanaokisiwa 700 waliuawa huko SOWETO mwaka 1976, Wanafunzi Soweto walivyojitoa mhanga kuwakabili makaburu, mauaji ya BOIPATONG ya mwaka 1992.

Hatua kandamizi zilizochukuliwa na serikali ya kibaguzi zilizidisha kuwaleta watu wa Afrika Kusini pamoja bila ya kujali rangi na asili zao kuzipinga sera hizo.

Haitashangaza kusema De Clerk hakuwa na uamuzi wowote juu ya kumaliza utawala wa kibaguzi nchini humo.

Alichokifanya De Clerk ni kutambua nguvu ya umma, ni kutambua kuwa watu wa Afrika Kusini wamechoshwa na sera hizo za ubaguzi na wapo tayari kwa lolote lile kupambana na sera hizo.

De Clerk alitambua pia uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa serikali yake ya kibaguzi ulikuwa umefifia, mwaka 1977 Umoja wa Mataifa (UN) iliikea vikwazo vya ununuaji na utengezaji wa silaha na vifaa vya Kijeshi Afrika Kusini katika azimio lenye namba 418, Refworld | Security Council resolution 418 (1977) [South Africa].

Mwaka 1986 Baraza la wawakilishi na bunge la senate nchini Marekani kwa pamoja waliiwekea vikwazo vya kiuchumi Afrika Kusini hadi hapo itakapo ondosha sera za kibaguzi, 1986 Anti-Apartheid Act | The Anti-Apartheid Movement in North Texas .

De Clerk hakuwa na maamuzi zaidi ya kulinda maslahi ya kiuchumi na kijamii ya wazungu nchini humo wakati huo huo akichukua jitihada za kuuridhisha umma wa watu wa Afrika Kusini na jamii ya kimataifa kwa kuchukua hatua mbalimbali chanya za kuondoa sera za kibaguzi nchini humo.

Moja ya hatua muhimu ikiwa ni kuachia huru wafungwa wa kisiasa na wanaharakati akiwemo Nelson Mandela aliye fungwa gerezani kwa kipindi cha miaka 27!

Naam, ninamsifu De Clerk kwa kukubaliana na ukweli kuwa "Zama za Serikali ya kibaguzi" nchini humo zilifikia tamati! Watu wa Afrika Kusini wamechoshwa na utawala wa kibaguzi, na hatua iliyobaki kwake ni kufungua mikono iliyofungwa kwa miaka mingi ili kulinda maslahi ya wazungu wenzake nchi humo.

Hadi mwaka 2014 inakisiwa kuwa zaidi ya asilimia 80% ya ardhi ya Afrika kusini inahodhiwa na wazungu. https://www.google.com/amp/s/mg.co.za/article/2014-09-15-do-40-000-whites-own-80-of-south-africa/?amp.

Nimalizie makala hii iliyosheheni maoni yangu binafsi, kwa kunukuu maneno ya mwanaharakati na kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema

"I am not for reconciliation, I am for justice. There is no reconciliation without justice and justice is the return of land"

Akiwa na maana "Mimi sipo kwa maridhiano, mimi nipo kwa haki, hakuna maridhiano bila ya haki na haki ni kurejeshwa kwa ardhi".

Bila ya shaka De Clerk aliupiga mwingi katika kulinda maslahi ya wazungu nchini humo!

Karibu!

Yussuf H. Khatib

Email: hajjyussuf2@gmail.com

WhatsApp: wa.me/+255777158131

fb: Kirjaudu sisään Facebookiin

FB_IMG_16366700176692547.jpg


Sent from my SHV40 using JamiiForums mobile app
 
Waafrika kusini wenyewe bila kupelekwa kama mbwa hawaendi, kipindi cha nyuma wakati naangalia zile movie zao za kupinga ubaguzi wa rangi nilikwa nawaonea huruma, ila kumbe saizi yao kufanyiwa vile
 
Huyo de Clerk anaonekana hero na anaumaarufu mkubwa ila, bado anamakandokando mengi ya ajabu.

Hakuwahi kukubali kua sera za kibaguzi ni za kinyama na kishetani ,bali anakiri kua zilikua mbaya.yani hajawahi tubu dhambi walizozifanya kwa waafrika ,ila anaamini ni sawa tu waafrika walikuwa ni makoloni.

Anaamini waafrika kusini kuteswa kwao ni by product ya ukoloni, hivyo wao hawatakiwi kulaumiwa,wako sawa na mataifa mengine kikoloni.

Hii ni nadharia mbaya sana,bora mungu amemchukua
 
Huyo de clerk anaonekana hero na anaumaarufu mkubwa ila, bado anamakandokando mengi ya ajabu.

Hakuwahi kukubali kua sera za kibaguzi ni za kinyama na kishetani, bali anakiri kua zilikua mbaya.yani hajawahi tubu dhambi walizozifanya kwa Waafrika, ila anaamini ni sawa tu waafrika walikuwa ni makoloni.

Anaamini waafrika kusini kuteswa kwao ni by product ya ukoloni, hivyo wao hawatakiwi kulaumiwa,wako sawa na mataifa mengine kikoloni.

Hii ni nadharia mbaya sana, bora mungu amemchukua
Kuna watu mnapenda kudeka deka

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ila watu weusi hawana kipawa cha utawala, wakipewa nchi lazima tu itakuwa "Shithole Country" hata iweje yaani sisi waafrika ni nuksi tupu.

Angalia hiyo SA ilivyokuwa kipindi hicho na kisha iangalie tena leo ilivyo tofauti ni kama usiku na mchana hata wenyewe wananchi wa huko hili wanakiri wazi kabisa.

Angalia Zimbabwe ya Smith na hii ya akina Mugabe na Mnangagwa yaani ni nchi mbili tofauti kabisa, hata Tanzania ya wakoloni na hii ya ccm ni tofauti kabisa.
 
Ila watu weusi hawana kipawa cha utawala, wakipewa nchi lazima tu itakuwa "Shithole Country" hata iweje yaani sisi waafrika ni nuksi tupu.

Angalia hiyo SA ilivyokuwa kipindi hicho na kisha iangalie tena leo ilivyo tofauti ni kama usiku na mchana hata wenyewe wananchi wa huko hili wanakiri wazi kabisa.

Angalia Zimbabwe ya Smith na hii ya akina Mugabe na Mnangagwa yaani ni nchi mbili tofauti kabisa, hata Tanzania ya wakoloni na hii ya ccm ni tofauti kabisa.
Weka data tuone tofauti Kati ya Tanzania ya kikoloni na hii ya sasa.
 
Weka data tuone tofauti Kati ya Tanzania ya kikoloni na hii ya sasa.
Tunaangalia Standard of Living, leo hii asilimia kubwa ya watanzania wanaishi chini ya mstari wa umaskini tofauti na ilivyokuwa wakati tunapata uhuru.
 
Tunaangalia Standard of Living, leo hii asilimia kubwa ya watanzania wanaishi chini ya mstari wa umaskini tofauti na ilivyokuwa wakati tunapata uhuru.

Hii akili ya wapi mzehe!!!! Nyerere ametufanyia nini cha maana? Angalau ungesema mwinyi na kikwete
 
Back
Top Bottom