March 19, 2019
Beira, Mozambique
Maafa mkubwa yaliyotokea kusini mwa Afrika kutokana na kimbunga cha Idai kilichokuwa na mwendo kasi wa kilomita 177 kwa saa na mvua kubwa iliyoleta mafuriko makubwa. Hili la sisi wana-wa-Afrika kukosa uchungu na kuchukuliana linaonekana na habari ya maafa haya kukosa habari ndefu hapa JamiiForums na media za barani Afrika kwa ujumla. Tuna uharaka wa kujadili maafa yanayotokea Mashariki ya Kati, Ulaya na Ocenia lakini maafa ktk bara letu hayazungumziwi kwa hisia kali.
Shirika la Msalaba mwekundu Red Cross na serikali ya Msumbiji wanatuambia Zaidi ya mamia ya watu wamepoteza Maisha kutokana na kimbunga Idai. Rais wa Mozambique Mh. Filipe Jacinto Nyusi amesema inakadiriwa watu 1,000 wamepoteza maisha na maelfu ya watu kukosa makazi, chakula na maji safi ya kunywa.
Pamoja na vifo vingi vya watu pia Miundo mbinu kama bandari ya Beira , viwanja vya ndege, maghala ya vyakula, madaraja na barabara vimeharibiwa nchini Mozambique. Magonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea kutokana na kukusekana maji salama.