Waafrica Wanajikomboa Kiuchumi kwa kutoa Utawala Mbovu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Waafrica wanajokomboa polepole bila watu kujua. Ivory Cost wanataka serikali mpya, Tunisia hawamtaki dicteta, Nigeria wamechoshwa na rushwa, Tanzania wamechoshwa na rushwa na Egypt wamechoshwa na ubabe na umasikini. Utawala wa Nchi za Africa hautaweza tena kujificha kwenye sera za ufisadi. Kitu kimoja tu kitawauwa mafisadi nacho ni Technology.
 
Nina maana gani nikisema Technology: tuanze na mfano mmoja tu wa hii JF kama unakumbuka zamani ilikuwa vigumu kwa Watanzania wazalendo kusema maovu ya serikali kwasababu walikuwa hawajui wamwambie nani lakini baada ya Watanzania kupata mtandao hakuna siri. Sasa Tanzania ina watumiaji wa mtandao 700,000 tu je itakuwaje wakifika 7,000,000.?. Simu kama unafahamu ilianza hivyo hivyo lakini sasa kuna Watanzania zaidi ya 10m au 25% ya Watanzania wanatumia simu.Cha pili kama umesikia Egypt wamekata mtandao na simu lakini bado tumeona picha, Dunia imekuwa wazi na hakuna sehemu ya mafisadi kujifisha tena kuna namna nyingi sana za kupata habari ambazo hakuna mtu anaweza kuzuia.Cha tatu wikileaks kama unafahamu hawa jamaa wamepata majina ya viongozi waliofisha pesa Swiss! hii ni kwasababu ya Technologia sasa dunia nzima itawajua wezi ni wakina nani!. Hata kwenye mikataba ya madini, maongezi ya mabalozi n.k technologia inabadilisha mwelekeo kwani sasa kila mtu anajua hakuna mkataba wa siri tena! hivyo wawekezaji inabidi wasaini mikataba ambayo hata ikijulikana itawaweka sehemu nzuri. Chenge mfano walijua ameiba pesa kwasababu ya Technologia, hivyo Technologia inafungua macho watu na itakomesha mafisadi.
 
Back
Top Bottom