Waafrica wakiwa wanaongea kiingereza huonekana kama watu fulani dumb hivi

Cheki waafrica wote. Wasouth, wakenya, wabongo, wazambia, wanigeria nk. Wakiwa wanaongea kiingereza wanaonekana kama watu wenye uelewa wa chini sana na slow learners. Cheki clips za bunge la South Africa, hadi maspika wanaonekana kama watu fulani wazito sana akilini, maskini wa misamiati nk. Hii lugha ya mkoloni imetushika pabaya sana.
Sauzi kiingereza ni lugha ya pili kwa matumizi. unaweza kataa iki ninachokiandika hapa ila huo ndiyo ukweli.
100% ukiwakuta wao kwa wao wanaongea ni lazima watumie lugha zao za asili.
ukienda maofisini mtaani kote wanazungumza lugha zao za asili tu.
kiingereza kinatumika wanapojua kuwa we ni foreigner.
2016 rafik yangu alinipeleka mpumalanga. kufika uko ni kama umeenda usukumani ndani ndani uko. kinachofanya ujue wapo ndani ya SA ni mazingira tu ila kwenye lugha hakuna.

ukanda huo nchi wanayoongoza kwa kuongea kiingereza kizuri ni wazimbabwe.
 
Ushawai kutana na waingereza wa kaskazin mwa London au Southampton!? Wanavyoongea ! Je ushakutana na warusi au waarab wakiwa wanaongea kiingereza!?
Kuwa na misamiati mingi pia uchangia na unao ongea nao ,

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Wengi husound dumb. Wakorea kusini huogopa kuongea kiingereza kwa kuhofia kuaibika.
 
Shuleni unafundishwa kiingereza kwa kiswahili! Masomo mengine pia, ukirudi nyumbani kila unayekutana ni Kiswahili na labda lugha ya mama yako.

Wanao fundisha Kiingereza nao ni wachache wana umahiri wa kufundisha kwa ufasaha. Chuo kikuu siku hizi naambiwa mkufunzi anachanganya Kiingereza na Kiswahili eti waelewe.

Ukimaliza chuo hata ukipata ajira unaokutana nao wanaongea Kiswahili tu. Kukutana na asiyejua Kiswahili labda mara moja kwa miaka miwili. Hapo tusiwe na tatizo?

Misingi yetu katika lugha hii ni hafifu. Na siku hizi kuna watu wanaponda umuhimu wa kuijua lugha ya kiingereza kwa kigezo na maneno ya kipuuzi kuwa ni lugha ya mabeberu au wakoloni.

Sio dhambi kujua lugha yako ya asili na lugha ya kigeni kwa ajili ya mawasiliano. Hata wajapani na wachina wanafundishwa na kujifunza lugha za kigeni. Hakuna hasara ya kujua kuongea kiingereza.
 
Unaeleza kuhusu kiingereza tu?Mbona hata humu JF kuna "wahashimiwa" wanaandika kiswahili kama wametoroka juzi Guinea ya Ikweta.Sasa kuongea sijui itakuwaje!Lugha ni sanaa.Lugha Ina asili ya watu.Lugha ni kipaji.Msikilize yule Bongozozo na mapigo ya sauti yake(intonation) ni kama mtoto anaongea.Lugha ina asili.Usiwacheke wala kuwaita "some dumbs"!😝😝😝😝😝
 
Shuleni unafundishwa kiingereza kwa kiswahili! Masomo mengine pia, ukirudi nyumbani kila unayekutana ni Kiswahili na labda lugha ya mama yako.

Wanao fundisha Kiingereza nao ni wachache wana umahiri wa kufundisha kwa ufasaha. Chuo kikuu siku hizi naambiwa mkufunzi anachanganya Kiingereza na Kiswahili eti waelewe.

Ukimaliza chuo hata ukipata ajira unaokutana nao wanaongea Kiswahili tu. Kukutana na asiyejua Kiswahili labda mara moja kwa miaka miwili. Hapo tusiwe na tatizo?

Misingi yetu katika lugha hii ni hafifu. Na siku hizi kuna watu wanaponda umuhimu wa kuijua lugha ya kiingereza kwa kigezo na maneno ya kipuuzi kuwa ni lugha ya mabeberu au wakoloni.

Sio dhambi kujua lugha yako ya asili na lugha ya kigeni kwa ajili ya mawasiliano. Hata wajapani na wachina wanafundishwa na kujifunza lugha za kigeni. Hakuna hasara ya kujua kuongea kiingereza.
Tofauti yetu sisi na hao wenzetu wachina na wajapan ni kwamba sisi huku tunafanya kiingereza ni zaidi ya mawasiliano unaonekana msomi na mwenye akili tofauti na wenzetu unaweza kukuta hata kiongozi mkubwa tu na kiingereza hajui vizuri na ni kawaida.
 
Ukisema wanasound dumb unamaanisha nini ??

Kwamba ni dumb kimsamiati kwa lugha wanayozungumza au

Ni dumb kwa hoja wanazotoa kwa namna wanavyozungumza?
Wanakuwa slow/wazito. Pia sababu ya umasikini wa msamiati hujikuta wanawasilisha mawazo yao siyo kwa ufasaha. Wanaonekana kama ni watu wa IQ ndogo hivi.
 
Kosa ni kuongea / kutumia tool (lugha ambayo hauja-imaster vizuri) kama una alternative (lugha kazi yake ni mawasiliano kwahio ni busara kutumia nyenzo zote au nyenzo unayoiweza zaidi) ili kufikisha ujumbe... kwahio kuna mambo muhimu yafuatayo:-

  • Je Muhusika angeweza kutumia lugha mbadala anayoijua vema kuwakilisha ujumbe na watu wakamwelewa (yaani wasikilizaji nao wanaelewa hio lugha ya mtumiaji)
Kumaster / kuongea / kuielewa lugha ambayo sio mama na kueleweka sio kuwa dumb, bali ni ujuzi zaidi na kipawa cha kujua / kuelewa lugha zaidi ya moja..., (Mtanzania anayeongea Broken Kichina , kifaransa au kingereza) ana ujuzi kuliko mimi ambae hata cha kuombea maji siwezi.

Pili Jamii husika zina english zao hata UK penyewe; Scousers, (liverpool), Cockney (london), Brummies (Birmingham), Geordies (Tyneside) wakiongea English zao ni tofauti na Scousers huwa ongea yao inachekesha; Kama tu ilivyo huku kiswahili cha wasukuma, wahaya, wachagga au cha watu wa morogoro kinavyopendeza na kufurahisha....

Moral of the Story; unaweza kumcheka mswahili kwa kukosea kiswahili ila sio kwa kukosea Kingereza, Kijerumani au Kifaransa (hapo utamsifia kwa kujaribu).
 
Wanakuwa slow/wazito. Pia sababu ya umasikini wa msamiati hujikuta wanawasilisha mawazo yao siyo kwa ufasaha. Wanaonekana kama ni watu wa IQ ndogo hivi.
Hapa hoja unamaanisha wakati wa kuzitetea ?

Maana kwa kawaida hoja hufanyiwa research na kuandikwa kabla.
 
Back
Top Bottom