Wa9ja na Mademu wa Kibongo

Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,384
257
Siku moja katika blog fulani kulikuwa na mjadala mkali sana kuwa dada zetu wa kibongo (walioko mtoni/majuu) wanajiachia sana kwa watu wa afrika Magharibi ambao (wawest) huja kuwatosa vibaya sana, na wadada walijitetea kuwa wanashindwa kutoka na wabongo kwa sababu wabongo wanachenga nyingi sana, hawaonyeshi kuwa mambo ya ndoa yapo, wanapenda kutumia sana, yaani yale mambo ya moja baridi moja moto na nyama choma.

sasa leo wakati napitia clips za Big Brother africa zimenikumbusha tena hii discussion.
Kelvin (Nigeria) Amekuwa akimuomba Elizabeth (Tanzania) kwa karibu wiki tatu sasa (kila siku), na Elizabeth ameonyesha msimamo wa kutokumuelewa mshikaji. watu wengi wanasema Elizabeth amekuwa ni mgumu kwasababu anajua yupo under camera, lakini mambo yangekuwa yanafanyika nyuma ya pazia angekuwa ameshamfungulia mshikaji siku si nyingi.

Pamoja na kumtafuta na kumwimbisha mtoto bado jamaa leo alimuudhi sana Elizabeth kwa kumtamkia maneno ya kibaguzi yaliyomfanya (Eliza) alie machozi http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=19865
Kelvin amejitahidi kubembeleza sana ili aweze kusamehewa lakini Eliza alibaki na msimamo kuwa yameisha lakini hatakuja kusahau. Kelvin ame-buy time ametafuta muda mwingine aje kuongea na mtoto tena na waweze kuyasuruhisha lakini Elizabeth amezidi kuwa mgumu kwa kumwambia Kelvin aachane naye na asimsumbue, Kelvin amejitahidi sana kuvumilia lakini hakusaidia kitu http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=19929 Lakini kilichonifurahisha ni usiku ulipofika muda wa kulala Kelvin amekuja kumfunika Elizabeth mablanket, Elizabeth amepigwa na butwa na kuonekana kutokufurahia kitendo hicho amefoka kwa kumuuliza Kelvin anafanya nini kwani hamuelewi elewi, Lakini kinachonichekesha ni Kelvin kuendelea na Ma-care, maana jamaa kashughurika weka mto sawa, weka nywele za mtoto sawa kama vile hawajagombana mchana. Mwisho Jamaa anamuuliza Eliza kama kuna kitu anataka kama Maji, Eliza aliyekuwa amechukia ameishia kucheka http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=19916

Nimefikia conclusion waacha wadada zetu waende huko west kama mambo yenyewe ndio hayo, maana huyu jamaa anajua kabisa kuwa yupo under camera lakini hajali yeye anabembeleza mtoto. Najiuliza wanaume wangapi wa Kibongo tungeweza kufanya hata nusu ya Kelvin? Na mimi sioni kama jamaa anafanyia kamera naona uhalisia kabisa na feeling za kweli kwa Elizabeth.

Najua wapo watakaosema kuwa wapo wanaume wenye kuonyesha ma-care zaidi ya hii ya Kelvin, tukiachana na wapenzi kwa wana Ndoa, kuna appology kama ya Kelvin kwa wanandoa hasa upande wa akina Baba?
 
Mkubwa mimi mfatiliaji sana wa big brother hasa big brother ya U.K wanayofanya kila mwaka ila naona kwamba jamaa kevin ni kama mzungu kabisa maana hajali kabisa kama kuna camera wala nini yeye anafanya kilichompeleka na mule ndani watu wengi wanaogopa kufanya vitu kwa ajili ya camera sasa sijui camera wanaogopea nini.......ila kevin nimemsifu sana yaani...Na naamini wakishakaa hata mwezi humo ndani watasahau camera!!
 
Mbogela nawe umedanganyika kirahisi...Huyo Kelvin Msanii tu,anajua anachotafuta.Keshajua kuwa Elizabeth anaogopa camera..lakini mambo yangekuwa nyuma ya pazia alikwishamaliza kazi siku nyingi.Elizabeth keshamzoea Kelvin na anapenda vituko vya kelvin....muangalie vizuri anavyomtazama Kelvin sio kama siku za mwanzoni.
 
halafu hawa washiriki wa mwaka huu mbona wanajificha ficha wakati wa kuoga ...
 
halafu hawa washiriki wa mwaka huu mbona wanajificha ficha wakati wa kuoga ...

Bado naona wanaficha almasi zao ila wataziachia tu mida ikifika,so kigogo kaa mkao wa kula mida ndo hii..
 
Bado naona wanaficha almasi zao ila wataziachia tu mida ikifika,so kigogo kaa mkao wa kula mida ndo hii..

mi nachelewa kwenda kazini walaaakh nione watoto hawa wakioga lakini wapi....dahhh
 
ila kevin yuko fiti katika kubembelezaaa..najifunza kweli kwake na wadau wamefarijikaa...umebadilikaa!!!!
 
mi nachelewa kwenda kazini walaaakh nione watoto hawa wakioga lakini wapi....dahhh

Mkuu nadhani shower Hour imeondolewa haipo kwani DSTv wana censor sana hii show ya mwaka huu, nadhani hawaonyeshi kabisa kuoga, wewe mzee wahi zako kazini tu, ukirudi jioni mchungulie mama watoto wako inatosha ha ha ha
 
Mbona na sisi tunawakanyaga Wanawake wa Kiboboo na tunawaacha vilevile hadi wanatulilia " Sikonge, why you do me like this ohh..." Wewe unajidai "Too much chilli on your food ..... Go away bwanaa..."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom