Wa-Tanzania Tujifunze Kubadilika Tabia: Mengine ni Matatizo Yetu Wenyewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa-Tanzania Tujifunze Kubadilika Tabia: Mengine ni Matatizo Yetu Wenyewe!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by W. J. Malecela, Jul 7, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - I mean nipo njiani hapa kwenye Treni, ninatokea Boston kurudi New York City, njiani humu ninajionea Wazungu masikini, lakini nyumba zao ni safi, maeneo yao ni masafi, nyumba za mbao na mabati lakini zimewekewa uzio, kwa majani senyenge, miti au hata waya tu kuzunguka nyumba!

  - Na pia bara bara sio za lami, lakini zimepangiliwa na zinaonyesha Mlango wa mbele wa nyumba, kuna box la barua, sasa sisi Tanzania jamani tumemkosea nini Mungu? I mean uchafu, wanyama wanakimbia kimbia hovyo bila mpango, hujui mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi?

  - I mean haya mengine ni yetu wananchi sio ya Serikali bana, Tubadilike tukitoka hapa JF twende majumbani na kwenye society and do something to our Society please!,

  - Tumezidi mno, tubadilike sasa!


  Willie @ NYC, USA.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  haya maswali ungemuuliza mshua .
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Absolutely nothing to do na Serikali, ni matatizo yetu wenyewe wananchi tubadilike, tuwe wasafi na tutunze mazingara yetu, JF tuwe mstari wa mbele badala ya kukaa kulaumu tu hapa asubuhi mpaka jioni, tuweke mfano kwanza!

  Willie @ NYC, USA.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  W.J.Malecela,

  Mkuu nadhani unafahamu fika kwamba wenzetu hiyo miji yao imepimwa. Hakuna ruksa kwa mtu yeyote kujenga au hata kumiliki ardhi pasipo kuwa imeandaliwa kwa ajili gani tofauti na sisi ambao kibali cha kujenga kinatoka mtu kisha jenga msingi kutokana na ubunifu wake. Bado tunaishi miaka 200 iliyopita wakati civilization iko mbele yetu na ktk jitihada za kuikimbilia tunapita njia za mkato na haya ndio matunda yake.

  Hatukurogwa, ila makosa ni zile fikra za kwamba tunatakiwa tukimbie wakati wengine wanatembea tukidhani maendeleo ni marathon, lakini kama tutaweza kujirudi na kusema sii lazima tuwe kama Ulaya na wala Ulaya yenyewe haikujengwa kwa siku moja, basi tutaweza kupanga miji, mabarabara yetu na pengine hata kuondoa kuta za magereza tunazojifungia wenyewe. Nilipokuwa Bongo katibu kila nyumba Mbezi au maeneo mapya huzungushiwa kuta ndefu na mageti makubwa ati ndio usalama wakati nyumba za Upanga na mjini ambako wahindi wengi matajiri wanaishi kwa usalama zaidi..

  Na hata ukifikira kwa makini, mwizi au Jambazi ataogopa kuingia nyumba ambayo iko wazi zaidi ya ile ilozungushiwa Ukuta kwani ukuta huo huo unakuwa kinga ya kuficha yanayotendeka ndani akivamia tofauti na nyumba ilokuwa wazi. Na hakika Ujambazi uliweza kupungua tu pale serikali ilipochukua hatua za kuwatafuta na kuwatupa lupango, kuta hazikuwa sababu kabisa ya kuzuia wezi au majambazi.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu serikali ina mchango mkubwa katika hili japokuwa wananchi nao wana mchango. Nasema serikali ina mchango mkubwa kwa sababu imeshindwa kabisa kupanga miji yetu na matokeo yake ni watu kujenga holela. Kutokana na kujenga holela ni vigumu kujua mbele ya nyumba ni wapi na nyuma ni wapi. Unakuta mbele ya nyumba ya mtu kuna choo ambacho kiko nyuma ya nyumba ya mwingine!! Hapa inakuwa vigumu hata kufuatilia suala la usafi. Serikali imeshindwa kuweka miundombinu ya maji machafu na barabara za mitaa zinazoonekana; Serikali imeshindwa kupima viwanja ili miji yetu iweze kuwa na mpangilio unaofaa. Angalia sehemu ambazo zina mpangilio kama oysterbay na masaki si unaona kuna afadhali mkuu.

  Cha kuchekesha, hivi karibuni manispaa za Ilala na Temeke zimetangaza kupima viwanja lakini bei yake haishikiki. Kiwanja kidogo kabisa cha 20mx20m ni milllion 4!! Hivi Mtanzania wa kawaida ataweza kununua kiwanja hapa kweli. Kwa maana hiyo serikali inachochea watu kuendelea kujenga bila mpangilio na hakika uchafu na miji kukosa mipangilio itakuwa ni donda ndugu kwa nchi yetu.
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Hata huko ni kuchafu sana kama kwingine kote tu!, tunahitaji kubadilika na JF tuwe mbele kwenye hili!

  Willie @ NYC, USA.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimesema ni afadhali kidogo huko kwa kuwa huwa sioni maji yakitiririka hovyo, ni afadhali ukilinganisha na sehemu ambazo hazijzpimwa kama manzese na maeneo ya Kimara. Watu tunajitahidi lakini mazingira ni magumu mkuu. Serikali inatakiwa iwe proactive. Ukitembelea Tanzania utaona kuna miji inakuwa kwa kasi lakini serikali haifanyi juhudi zozote za kuipanga inaiacha iendelee kujengwa shagilabaghila!
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Willy, tukitoka hapa twende majumbani kwenye society wapi, New York City?

  Wewe umekimbia, nani akakujengee nchi yako? Umeamua kuwa manamba Marekani, baki Marekani, acha sisi tujenge nchi. Nakubali, Tanzania yetu hali ni mbaya sana, mbaya kiasi kwamba mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu badala ya kufata ambitions na footsteps alizoacha babaake anaona ni bora awe manamba Marekani.

  Lakini sisi ambao hatujakimbia tutaijenga nchi yetu, tuvumilie tu.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo linaaaza pale serikali inapoosa kuweka miundombinu. kama
  • Huko unakopita Hizo nyumba unazoona imepangika sababu hakuna anayejenga kwa TGS yake . Nadhani ni mikopo nyie mnaita mortgage. Tatizo la nchi zetu serikali imeaccha watu wahangaike na mambo ya makazi wennyewe. Utaona hata yale maeneo yenye nafuu ni sababu ni zile nyumba zilikuwa za NHC. So ni ukosefu wa mipang miji ndo unachangia hali kuwa mbaya zaidi.
  Kama serikali na Tasisisi zake kama NSSF, PPF, LAPF na mabenki zingeweka sera sahihi basi kero ya mipango miji ingekuwa ndogo sana Kuna watu watasema watanzania hawakopesheki lakini sio kweli. mambo ya Toxic loans hata ulaya yametokea. Akwa uchache mashirika kama NSSF PPF yalitakiwa kujenga nyumba 30- 50 kila mwaka kwenye mikoa

  • Kitu kingenine kinachweza kuleta mabadiliko Tanzania ni kuondoa kasumba ya viongzi kujengewa nyumba sehemu moja. Ningekuwa mimi Nyumba za mawaziri na watendaji mbali mbali zingetapakaa kila kona iwe ni mwananyamala, Sinza, Mbagala kimara, gogola mboto. Na mikoani hivyo hivyo .
  Hawa viongzi wanatakiwa wakae na waishi mazingira wanayoshi watanzania wengi. Kwa njia hiyo nadhani kero nyingi zingefanyiwa kazi. Maana kama Mkurugenzi wa wiara ya fedha akiona kero fulani ya maji mwananyamala anakoishi may be wanawezza kuongea lugha moja na Mkurgenzi Au waziri wa wa Wizara ya maji anayeishi Kimara....... Sure hii ingefanya kazi kirahisi. Na hata isingefanya kazi waanachi labda wangesikia faraja kuwa wapo kwenye matatizo sawa na wale wanaopanda ma VX.

  Hayo ni mawazo ya mtazamaji
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Hivi jamani tunaweza kujadili bila Serikali please? Hivi kweli wananchi hatuna responsibility?

  Willie @ NYC, USA.
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huwezi kujadili Usafi wa mji Bila serikali @ Newyork Na unaposema hata Masaki ni pachafu kama kwingine hapo ndio huwa nashindwa kukuelwa unapokwepa ukweli.

  Masaki sio chafu kama mwananyamala na mwananyamala sio chafu kwana Jangwani au uwanja wa fisi.

  Au unaongelea usafi wa ndani ya nyumba ?
   
 12. L

  Leornado JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Serikali ya CCM ndio ilotufikisha hapa tulipo, mbona huongelei jinsi mnavyogawana maeneo ya wazi ya watoto kuchezea mipira na kupumzika kwa mgongo wa uwekezaji?

  Hebu acha utani bwana, hao kuku na mbuzi wanaozagaa majumbani kwetu wako bize wanajitafutia mlo. Huko ulikopita na gari moshi (Boston) hali yao kiuchumi ni tofauti kiasi kwamba kuku na mbuzi hawajitautii malisho. Pia hatuna maji ndio maana unaona vitu vimetapaa nje ya nyumba tofauti na wenzetu wao kila kitu ndani kwa ndani....Ina maana umesahau ulikotoka ua umekulia maisha yepi mwenzetu?
   
 13. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mkuu,kwa mfananisho huo sawa.....ila naomba ufikirie katika mantiki hii.
  Vumbi ni uchafu,ukiona vumbi au mchanga ambao haupo beach,ujue huo ni uchafu.
   
 14. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Willie naomba utambue kuwa matatizo hayo yanasababishwa na mfumo wa serikali zetu ulivyo mbovu kiasi kwamba uzalendo haupo unakuta serikali inamwaga mboga na wananchi wanamwaga ugali na kutupa vyombo vyakupikia. Lakini serikali za wazungu zinamifumo mizuri inayozidisha uzalendo wa wananchi.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Bro nimesoma bongo, kila siku asubuhi tulikuwa tunafagia maeneo ma mifagio ya makuti, nimekwenda JKT ni vile vile, sasa ninachokiongelea ninakijua na nimekifanya ninasema hivi usafi wa mazingara yetu hayahitaji Serikali wala CCM au Chadema, tubadilike akili wananchi jamani!

  Willie @ NYC, USA.
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Hahhaa hii fasihi uliytumia nimetumia kama dk 5 hivi kuelewa nini unamaanisha. Hapo nimekusoma . teh teh
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @William, when you dont know where your next meal is going to come from, senyenge, sanduku la posta, geti (hata la manyasi), takataka ( and I mean takataka) will be last thing on your mind. Hivi kwa kijana anayeuza maji baridi pale Ubungo mataa, au anayeuza handkerchief Somara Avenue atapata wapi muda wa kufikiria sanduku la posta kwanza la nini? au kusafisha nje ya nyumba, kwanza yake? na analalam saa ngapi?

  Pia kumbuka watu wengi walio mijini sio tu wana pressure ya kujitafutia maisha wao wenyewe, wana mzigo mkubwa wa wategemezi vijijini wanakotoka. Kiutawala, mipango miji na kama hakuna na serikali za mitaa nazo hazina wamechoka kupeleka barua za malalamiko kwa halmashauri bila majibu. Our system cannot avoid the blame. Hapo Boston mtu anaweza kujenga ukuta na kuzuia barabara ya umma kama alivyofanya Spika wetu hapa?
   
 18. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kumbuka tuko Third world. Nawezajenga kajumba kangu na kufuata utaratibu na mipangilio yote uliosema. Lakini sheria huku hazifanyi kazi, kesho unaamka unakuta jirani kajenga banda la fisi na liko barabarani kabisa. Kaachia fisi wake wanarandaranda koote na usiku ni kero tupu. Kumbuka hatuna home owners associations. Home owners associations zimesaidia sana kuboresha mazingira na kumaintain usafi ktk residential areas nyingi US, e.g. ukiacha nyasi za backyard amba mbee ya nyumba zikikua bila kizifyeka unakula warning na fine. Sheria zikiwepo na zikafuatwa hilo litakuwa sio tatizo.
   
 19. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyu malecela gani vile? Njoo huku kwetu mba(ga)ra uonyeshe mfano hai-usafi kwa vitendo
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mfumo wetu wa elimu hauna mchango katika ustawi wa jamii na responsibility au hata haki za msingi za raia
  kama mfumo wetu ukifanana na wawenzetu na sheria zikabalishwa yaani kila mtu ana wajibika na kuwajibishwa na sheria
  ni hakika tutafika hapo.

  Nadhani unajua kwamba kwa wenzetu uwezi kufanya uchafu kisa ni nyumbani kwako hatua zitachukuliwa kwa misingi ya HEALTH AND SAFETY au enviromental related issue .
  Bila sheria makini hii uchafu kwetu haitakoma mfano kuna miji ulaya kama ukichanganya taka mwepesi na recycle ujue unalo fine ni karibu mshahara wa mtu kwa mwezi mzima
   
Loading...