Wa-tanzania muda umefika kuchukua hatua dhidi ya hawa viongozi legelege, kabla hatujaangamia wote! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa-tanzania muda umefika kuchukua hatua dhidi ya hawa viongozi legelege, kabla hatujaangamia wote!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpiganiaUhuru, Oct 15, 2012.

 1. MpiganiaUhuru

  MpiganiaUhuru JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 180
  Wana-JF!
  Nachukua fursa hii kusema kwa uchungu mkubwa kuwa hivi karibuni tumeshuhudia viashiria ambavyo vinatoa picha halisi ya kule Watanzania tunakoelekea (Machafuko makubwa). Viashiria hivi ni kama vile:
  1. Jamii kutokuwa na hali ya uvumilivu tuliozoea kuiona (inayosababisha msemo wa nchi ya amani)
  2. Udini wa kupindukia (mf, kujaa kwa vyombo vingi vya habari vya kidini, fujo mbalimbali zinazoambatana na udini, mambo ya kidini kuingizwa kwenye sera za nchi, nk)
  3. Kuwepo kwa makundi/mitandao ya watu ambayo kazi yao kubwa ni kutengeneza mazingira ya kutafuna rasilimali za nchi. Mfano wa maeneo yanakopatikana makundi haya ni kwenye Vyama vya siasa hasa CCM, Vyombo vya dola, Halmashauri, Wizara, Ikulu, Idara za Serikali, Mashirika ya Umma kwa ujumla wakishirikiana na Wafanyabiashara. Mitandao hii inapambana kufa kupona kujihakikishia kuendelea kuwepo kwenye maeneo yanayowapa ulaji, hivyo wakati mwingine yanasababisha hata vifo, vilema au majeraha kwa wale wanaoonekana kwenda kinyume nao.
  4. Maneno mengi ya ki-uchochezi kwenye midomo ya watu hasa Viongozi wa Kisiasa mfano, Chama fulani cha kisiasa ni cha dini au kabila (kanda) fulani, viongozi na watendaji wote walio madarakani ni mafisadi, Wazanzibar wanadhulumiwa na Wabara, nk.
  5. Vyombo vya habari kutoa taarifa yoyote bila kuzingatia athari zake kwa jamii
  6. Dini nyingi kupoteza mwelekeo (kujikita zaidi kuchangisha fedha kutoka kwa waumini kuliko kuhamasisha masuala ya amani, upendo na uvumilivu)
  7. n.k

  Maoni yangu:
  Kwa kuwa nchi inakuwa na uongozi ili kuiongoza ikiwa ni pamoja na kuidhibiti jamii ili viashiria hivi visijitokeze, ni wazi kuwa uongozi tulio nao umeshindwa kuongoza na sasa kinachosubiriwa ni hali kuzidi kuwa mbaya na kusababisha kila mtu kuongozwa na utawala binafsi hivyo kupelekea kuwa na machafuko makubwa tena muda si mrefu. Uongozi uliopo madarakani umetoa mchango mkubwa sana kutufikisha hapa tulipo. Mfano mkuu wa nchi amekuwa akikaa kimya kwa mambo ambayo ni very sensitive kama vile kutokemea kauli za udini na ukabila badala yake anasubiri athari zikishajitokeza anaenda kutoa pole halafu anatulia (mf, kubomolewa kwa makanisa), kadhi mkuu (Kiashiria cha udini kwenye sera za nchi isiyo na dini) amechaguliwa kwenye utawala wake, mauaji mengi ya kikabila yamefanyika kwenye utawala wake na bado yanaendelea na hana suluhisho la kudumu, n.k.

  Nini kifanyike:
  Jamii ambayo imeshayaona haya inapaswa kuchukua hatua za haraka bila kuchelewa vinginevyo tanaelekea walikokuwa wenzetu wa Rwanda (Mauaji ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yatamgusa kila mtu kwa namna yake). Ni heri kufanya hata mauaji ya watu wachache wanaotupeleka huko kuliko kusubiri maangamizi haya! Mungu tuokoe na dhahama hii!

  Naomba kuwasilisha kwa michango zaidi!
   
 2. k

  kukukakara JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  We una maoni gani, kifanyike nini
   
Loading...