GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,743
- 118,308
MAREKANI - Mkurugenzi wa Huduma ya Usalama wa Taifa nchini Marekani, Kimberly Cheatle ameomba kujiuzulu huku kukiwa na utata wa hitilafu za kiusalama kuhusiana na jaribio la hivi karibuni la mauaji ya Rais wa zamani Donald Trump, CNN imeripoti.
Hatua hiyo imekuja huku wabunge na shirika la ndani la serikali likiendelea na uchunguzi kuhusu jinsi shirika hilo lilivyoshughulikia ulinzi wa Trump na jinsi mtu mwenye silaha alikaribia kumuua mgombea wa urais wa chama cha Republican mwaka 2024 katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania mwezi huu.
Cheatle alisema katika barua yake ya kujiuzulu kwamba amefanya uamuzi "mgumu" wa kuachia ngazi na kwamba hataki ondoka yake itikise jitihada za mamlaka hiyo kuendelea na misheni zake.
"Kwa kuzingatia matukio ya hivi majuzi, ni kwa moyo mzito kwamba, nimefanya uamuzi mgumu kujiuzulu kama Mkurugenzi wako," Cheatle aliandika. Alikubali kuwa mnamo Julai 13, siku Trump aliyofyatuliwa risasi, Mamlaka hiyo "ilikosa" dhamira yake ya "kuwalinda viongozi wa taifa letu."
Naibu Mkurugenzi wa Huduma ya Usalama Ronald Rowe ameteuliwa kuongoza shirika hilo, Idara ya Usalama wa Nchi ilitangaza.
Katika taarifa, Rais Joe Biden alisema yeye na mkewe, Jill Biden "wanashukuru" kwa miongo ya Cheatle ya utumishi wa umma.
Chanzo: habarileo_tz
Wana Usalama wa Taifa wa Marekani waje tu kujifunza Tanzania kwani ndiyo ina Wakurugenzi Wakuu Waadilifu sana.