Wa Lissu na Magufuli ni upepo unaovuma kwa kasi na utapita tu, kuna atakayeshindwa vibaya battle hii

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,185
2,000
Hakuna marefu yasiyo na ncha, uzuri ni kwamba historia ni Mwalimu mzuri sana,

Ipo siku ataanza kuandamwa mtu mwingine alafu watanzania hawa hawa watamsahau Lissu,

Najua upepo uvumao kwa nguvu uacha alama na athari mbali mbali,

Magufuli hana cha kupoteza katika battle hii, anayepoteza ni mtanzania wa kawaida sana, ambaye pamoja na mimi tunashinda hapa JF na mitandao mingine tukishangilia na kuagiza popcorn bila kujua kwamba tuna jukumu la ziada sana kuhusu suala ili,

Nahisi kutokana na shambulio au yanayoendelea kati ya Miamba miwili ya siasa yaan Magufuli na Lissu, yalipaswa kutuachia somo la kutatua haya,

1.Kujua hivi ni wapi unapopatwa na janga kama la Lissu upeleke malalamiko yako kama serikali haionekani kujali?

2.Ulinzi unapaswa kuimarishwa tu au tatizo siyo ulinzi, ni mipango ovu dhidi ya mtu hata kama analindwa, na je tunatatua vipi ilo,

3.je wajua kwamba battle likiisha kuna kila aina ya mmoja wapo kupotea kabisa na kujuta kwa aliyoyafanya? Yaan kwa kipindi watanzania watakuwa na wanyemshangilia akiwa mpya kabisa?

Lazima mmoja ashindwe na akishindwa atakuwa kajuzibia baadhi ya Mambo kwa sababu mmoja ana uwezo wa kumfanya mtu asiishi kwa raha hata kama exile family yake iko Tz,

Ndo ana uwezo wa kuamua kwamba sasa ukiwekwa ndani mpaka aamue kisa muhimili wake una Monocotyledon root,

Je wajua kwamba atakayepotea kuna muda atakosa hata shilingi kwa tenda zake kadhaa huku akiwa kanyang'anywa hata ubunge kwa Mizengwe,

Wazungu wahuni sana uwatumia watu kama chewing sweets na kukuacha solemba, wakati huo mshahara wako ukiwa umezuiwa, makampuni yako yakiwa yamefungwa, passport yako ikiwa imezuiwa, wakati huo maisha yanaminywa,
Namuona Lissu aliye loose battle , watanzania wakiwa wamemchoka, wazungu na Ma Bbc wakiwa hawamuiti tena, wakati huo akiwekewa mizengwe ya kufukuzwa ubunge na kunyimwa stahiki zake,

Namuona Lissu anayeachwa aingie nchini alafu amalizwe kimya kimya kwa njia yeyote(sijasema kumuua hayo umeyawaza wewe)
Naona kesho yenye kesi za uahini dhidi ya Lissu,

Namalizia na swali kwa Lissu na wafuasi wake kuwa !!!
Huoni kwamba unapoteza Muda tu huko ulipo kaka yetu??
Ilibidi ukaushe maisha ni matamu kuliko siasa kaka yangu,

HAYA YOTE SULUHU NI KATIBA MPYA,

Uzi huu ntaufufua 2022

Nisome hapa

ICC alichomoka Kenyatta na kesi ya mauaji sembuse Magufuli?!! - JamiiForums

Inawezekana mgombea Urais kupelekwa mahakamani muda wa kampeni ushahidi ukiletwa? - JamiiForums
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,489
2,000
Dunia ya miaka 10 iliyopita siyo dunia ya leo. Mambo yanabadilika sana kwasababu maarifa yameongezeka. Historia ina tabia ya kujirudia: Hata Nyerere naye aliwafanyaga hivihivi wakina Kambona, Jumbe na wengine lakini MUDA ni kitu kibaya sana, walitokea wengine na walimyumbisha hadi akaamua kukimbia Ikulu mwaka 1985.Akajisemea mwenyewe kwamba hakuna kitu kigumu kama kuwabana watu walio elimika.

Lissu is just a tip of the iceberg kwasababu tu yeye ni mwanasiasa, ndiyo maana anaonekana sana. Lakini amini nakuambia kuna watu wabaya sana kuliko Lissu ambao wako karibu na Raisi na wanamchekea kila siku na kunywa naye chai. Ambacho mnashindwa kukielewa ni kwamba panapo moshi hapakosi moto.

Raisi ana maadui wengi sana hapa nchini tena ndani ya Serikali na Chama chake kuliko hao wakina Lissu na upinzani. Tena kama kumuumiza watamuumiza haohao ndani ya chama chake kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Kikwete.

Mtanange baina ya Raisi Magufuli na Lissu ni sehemu ndogo sana ya mitanange ambayo Raisi anapigana nayo sasa au ambayo ataanza kupigana nayo hivi punde....
 
britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,185
2,000
Dunia ya miaka 10 iliyopita siyo dunia ya leo. Mambo yanabadilika sana kwasababu maarifa yameongezeka.
Kwa afrika mkuu bado sana, dunia hubadilika ulaya na america tu wakati afrika ikiwa static

Jiulize wapi bado wanamini katika udikteta, 70% ni afrika wakati ulaya wakiwa wanaisha isha,
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,303
2,000
Labda wewe unamuona kuwa anacho cha kupoteza lakini yeye anajiona hana cha kupoteza. Kabla ya tukio alikua na hofu lakini baada ya tukio ameona kuwa kumbe hofu haiwezi kumuweka salama, na pia kama alivyopata kusema mwenyewe kwa kauli yake baada ya kuzinduka kuwa "I survived to tell the tale". Hii ilikua ni kauli nzito sana.
muachani Lissu alie atakavyo, maana maumivu yake siyo yenu, kamwe hamuwezi kuyasikia.
Tuangalie mustakabali wa taifa letu, isije ikawa tunadhani tupo salama kumbe upande mwingine tunapanda mbegu ya chuki na visasi muda ukifika mambo yalipuke.
 
kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,328
2,000
Kwa hiyo mnataka watu waendelewe kumiminiwa risasi kama movies za Rambo huku wafanyabiashara na watoa maoni yasiyowafurahisha watawala wakitekwa na miili mingine ikiokotwa mitaani kama makaratasi?!
 
Dereva wa Kirikuu

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
743
1,000
Kwa afrika mkuu bado sana, dunia hubadilika ulaya na america tu wakati afrika ikiwa static

Jiulize wapi bado wanamini katika udikteta, 70% ni afrika wakati ulaya wakiwa wanaisha isha,
Mkuu mimi nakubaliana nawewe..
Kwa sisi waafrika bado stationary mode..hata hizi tecnologia hazitusaidii sana zaidi yakutuongezea ujinga kwa kasi zaidi.
Upeo wakuchanganua jambo/mambo unazidi kufifia tena kwa sisi vijana ambao ndio waongoza nchi wajao...
 
britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,185
2,000
..na JPM anatakiwa afanye nini ili dunia na Tundu Lissu waone haki imetendeka?

..kuna option inayotoa haki kwa TL na ushindi wa JPM nilitegemea ungeijadili.
Mkuu hiyo naomba uiweke maana nahisi unaweza kuwa na mawazo mazuri zaid,

Ila kwa sasa ilibidi kila mtanzania mtaka mabadiliko ajadili suala la katiba yenye mamlaka kidogo ya rais, ili tuwe huru, nakuhapia watanzania hatuko huru kuongea kabisa,

Kwa bahati mbaya huwa siamini mabadiliko kuletwa na wazungu bila watanzania wenyewe kuwa na mwamko juu ya katiba yenyewe na wanachotaka kibadilike
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom