Wa kurekebisha uvurugaji wa nchi wa miaka 10 ya JK; Migiro? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa kurekebisha uvurugaji wa nchi wa miaka 10 ya JK; Migiro?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Synthesizer, Jan 23, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kuna uvumi kwamba Migiro ni new factor katika mbio za uraisi. Jambo la kukumbuka ni kwamba katika miaka 10 ya utawala JK Tanzania itakuwa imevurugwa mno, itahitaji mtu makini, serious, mwenye busara na ukali wa kiasi kuirudisha katika mhimili unaostahili - mtu wa namna ya Kagame-Kagame hivi; no-nonsense president. (Mara nyingine natamani Kagame awe raisi wa kwanza wa East Africa).

  Miaka 10 ya Mwinyi nchi ilivurugwa sana, na japo mapungufu yake mengi, Mkapa alifanikiwa kuturudisha kwenye mstali unaofaa kwa kiasi fulani. JK ame-reverse mazuri yote ya Mkapa na kutupeleka pabaya zaidi ya tulipofikishwa na Mwinyi.

  Sasa ukiweka mikaka 10 ya JK, ukaweka miaka mingine 10 ya uozo mwingine wa uongozi basi nchi yetu itakuwa kaput, isisile, imalike, crap!

  Sasa fikiria; Asha Migiro for a no-nonsense president kututoa tutakapofikishwa na JK?
   
 2. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  We unadhani nani anafaa badala ya kulia na Migiro si umtaje tu huyo unayemwakilisha. After all Mama Asha Migiro alishakutangazia kuwa anataka U-Rais? ama unaogopa kivuli chake?
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Baada ya miaka 50 ya CCM bado tu kuna watu wanategemea kuwa CCM ni mkombozi na suruhisho ya matatizo yetu kweli??
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Natamani mapinduzi ya kijeshi angalau yatasaidia.
   
 5. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Hakuna cha Rose Migiro wala nini hapo anapigiwa debe ili kuendeleza zile agenda za Abuja za 1987! Sasa kigezo cha gender kinaletwa lakini ukweli chini yako au mbereko ni lile azimio la Abuja.
   
 6. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Huo uvumi umeutoa wapi au ni ndoto za mchana..ccm wameshindwa kututoa tulipo kwani kwa sasa tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele
   
 7. m

  mpendadezo Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  mimi naona tuondoe hii system ya kutoa rais ambaye alikuwa yuko nje zaidi tunarudi kulekule ni rahihi kununuliwa na mabepari hii ni inahitaji mtu ambaye ni aggresive, mwanawasa type or kagame ina mambo mazito ya kuondoa mwanamke hataweza kupambana na mijizi sampuli ya rostam na manji.angalao watu kama sita, lowasa na dr slaa wana ujasiri wa kusimamia ukweli
   
 8. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  If Migiro hafai basi Lowasa is our best fit! Anyway, napita tu bandugu wajuzi wa haya mambo tupeni michango yenu!
   
 9. h

  herimimi Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani amefanya nini hapa Tz hadi atajwe urais?
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako ukipenda unakuwa kipofu kabisa. Nchi hii ameanza kuivuruga Mkapa na hili lajulikana ila kwa uozo wako wa mawazo unasema ameirekebisha. Ufisadi wote ulianzia kipindi cha Mkapa mpaka na yeye mwenye akajiuzia Kiwira, ww haya huyaoni ? EPA , Kagoda nk huoni tu ? basi ww ni .............................

   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Migiro ndo anaondoka un,kuna uwezekano atakuja Gombea
   
 12. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Soma magazeti, labda kama hujui kiingereza sema tukusaidie kutafsiri; The Citizen; "Migiro factor" fuels 2015 polls debate". The emminent return home of Dr Asha-Rose Migiro after expiry of her tenure as United Nations deputy secretary general, has given fresh momentum to speculations on who will emerge victorious in the hotly contested slot of CCM candidate in the 2015 presidential election.
   
 13. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Yaani unaniambia nina tatizo la kupenda kisha unasema aliyeanza kuvuruga nchi ni Mkapa? Naona wewe umezaliwa enzi za utawala wa Mkapa, na hukuona enzi za skandali za Loliondo, dhahabu kuvushwa na mapailot, biashara ikulu, First-lady-cum-president, degradation ya wasomi na wafanya kazi, wahindi kushika hatamu za nchi, wafungwa kuombewa msamaha kwa raisi na mama zao, nk!
   
 14. k

  kiche JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwa mfumo uliopo ndani ya ccm ni maajabu kuwa kuna mtu anaweza toka ccm akaleta mabadiliko,binafsi hata unishauri vipi kamwe siwezi kukubali,ccm imefika sehemu hawana dira, na bila dira chombo cha usafiri hakiwezi kufika kule kiendako,walipewa ushauri na Kolimba lakini ajabu yaliyotokea ni drama!!!
   
 15. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Mwinyi na Mkapa walipogombea uraisi walitangaza nia zao? Sie tunachambua mada kutokana na mazungumzo yanayoendelea nchini. Sasa kama wewe umezamisha kichwa chako ndani ya mchanga na kujifanya husikii wala kuona kinachoendelea ni vema ujiondoe humu JF, usitupotezee wakati na pumba zako sizizo na msingi unazoona ni worth ku-post. Period.
   
Loading...