MC Chere
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 586
- 400
"Ebwana hapa nilipo nina ndugu kibao wamejazana hapa, na siwezi kuwafukuza, yaani walipiga simu eti anko tunakuja kukusalimia, hata kuwazuia siwezi, sasa ninajaribu kuwaelekeza namna maisha ya mjini yanavyotaka kujichanganya changanya ili mkono uende kinywani, lakini inaonekana somo lipo mbali na sasa maisha yanakaba mpaka naona kero kwa uwepo wao. Na tena bwana nitaomba kama ukiipata hiyo mashine naomba uwaajiri hawa vijana, nitawashawishi hata wawili waje na kuwapa elimu zaidi ya kufanya kazi".
Hayo ni maongezi niliyoyanasa kutoka kwa bwana mmoja aliyepo Dar akimwelekeza rafiki yake wa Iringa kwa simu wakati huo tupo internate cafe.
Jamani, Watanzania wenzangu mliopo vijijini, msidhani kuwa waliopo mjini mambo yao ni poa, ni ujanjaujanja tu jamani, sasa unapofunga safari kwenda kwa mtu just kumsalimia tu, kwanza amekuomba umsalimie!? Pili unasalimia hadi miezi mitatu?
UJINGA HUZAA UMASKINI, TUBADILIKE JAMANI.
Tujali kutumia muda kujiingizia pesa.
By MC Chere kipenzi cha Lara 1.