Wa-jf mnaelewa kuwa duniani kuna "court of law" na sio "court of justice" katika mfumo wa mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa-jf mnaelewa kuwa duniani kuna "court of law" na sio "court of justice" katika mfumo wa mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWINUKA E, Apr 8, 2012.

 1. M

  MWINUKA E Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ambao wanaitwa ni wanasheria kwa kusoma mawazo ya watu waliopo kwenye kozi ya Jurisprudence ni wakati sasa wa kutafuta mfumo wa kuhukumu kwa haki hapa duniani maana mpaka sasa haupo kufuatana na hoja hizi hapa chini.

  Mimi sio mwanasheria ila ni mwanafalsafa. Siku zote nimekuwa nikijiuliza kwa nini mahakama zetu haziitwi court of justice kwa maana inasadikika kuwa haki inapatikana mahakamani. Baada ya kufikiri kwa mda mrefu na kufuatilia mtiririko wa matukio yanayotokea katika mahakama zetu hasa za Tanzania kama babu sea, kesi ya lema nimegundua yafuatayo kwa utashi wangu wa kufikiri kuwa hatuna mfumo wa kutoa haki duniani mpaka sasa:

  1. Hatuna wanasheria duniani. Hawa wanaoitwa wanasheria hawasomei sheria ila wanasomea sheria zinakopatikana na namna ya kuzitafsiri.

  2. Pia nimegundua tasfiri ya sheria ni subjective na si objective. Maana hakuna standard procedures za kufuata ili kutafsiri sheria bali inategemea akili ya mtu aliyepewa mamlaka ya kutafsiri wakati wa kutafsiri, muktadha na pressure aliyonayo kwa wakati huo wakati wa kutoa hukumu.

  3. Pia nimegundua mahakimu wanaangalia validity ya premises na arguement na si truth of the premises or arguement. Hivyo kwa mtu asiyeweza kujieleza anaweza kutiwa hatiani hata kama hajafanya kosa husika.

  4. Nimegundua haki haipatikani mahakamani. Kwa sasa hakuna mfumo duniani ambao unaweza kuhukumu kwa haki. Ni Mungu (Yehova) tu ambaye anaweza kuhukumu kwa haki kwa sasa. Hivyo ni changamoto kwa hawa waliopata shahada na PHD kwa kusoma mawazo ya watu ili wakae,wafikiri na kutafuta mfumo wa utoaji wa hukumu za haki duniani
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Hilo umegundua lini? Manake liko dhahiri kama mwanga wa jua!!
   
Loading...