WA IRAN NA WA OMAN wafanya ufisadi wa ardhi Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WA IRAN NA WA OMAN wafanya ufisadi wa ardhi Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Quonquerer, Aug 5, 2010.

 1. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani nimepata tetesi kuwa Iran inatarajiwa kupewa hekta laki na ishirini mkoa wa Pwani ku - swap na deni la mafuta wanalotudai na tayari walishapewa hekta 5000 huko Mkuranga kwa kupitia kwa wakubwa licha ya watalaam wa kilimo na chakula kupinga jambo hilo kwa sababu linakiuka utaratibu wa TIC wa ubia!

  Na nasikia wa Iran wameshashusha vitu fulani kwa wakulu kwa ajili ya uchaguzi, sitaki kuvitaja ila ni vya thamani kubwa! Oman nao wanahusishwa kwa mipango hiyo michafu.

  Kama kuna mtu ana full nyuzi na data azimwage na tuzimwage upinzani au njia nyingine sahihi angalau tuzime jaribio hili la kutaka tuwe watumwa nchini mwetu! Saa ya ukombozi ni sasa! Muungwana ni vitendo!
   
 2. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hii ni hatari sana - nakumbuka ile mikataba enzi za ukoloni ya mtu kugawiwa eneo lote la ukanda wa pwani!
  Kama ni kweli, basi huu ni utumwa wa dhahiri - nadhani deni hili ni lile ambalo RA alipewa hard cash akalipe halafu hakulipa!
   
 3. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Jamani tunauzwa huku tunaona.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kilimo kwanza, maswali baadaye

  Vyanzo vyote vimeshitukiwa unategemea nini??????
   
 5. R

  Ramos JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Very easy to solve. Lakini itakuwa easy tu kama Slaa akiwa raisi...
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umepata tetesi,fanya utupatie habari zilizokamilika.Sidhani kama ni busara kujadili tetesi.
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Mkuu umewaona/umewasikia hao tu? mbona wako wengi tumeshawakatia ardhi yetu mkuu. Nenda Kilombero ukaone jamaa walivyokatiwa nchi,na si Wairan au wale jamaa waliowakimbiza Wasangu pale Mbeya. Mkuu ukienda mikoani utalia. wale jamaa waliokimbizwa Zimbabwe na kuja Bongo unajua wanafanya nini na wapi.

  Inatisha na kukatisha tamaa,inauma na kukera mno. Mswahili ukiomba eka mbili tu ni vikwazo hadi basi. Tuamkeni jamani.
   
 8. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Thibitisha tetesi zako
   
 9. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anyway, kama kuna yeyote mwenye kujua mizizi ya hii dhuluma aiweke hapa, ili uhakika uwepo na tuweze kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupambana nalo ili kunusuru ardhi ya TZ.

  Angalizo - " lisemwalo lipo, kama halipo laja "
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wairan na Waoman ni wawekaezaji kama walivyo wengine kama vile waingereza, wamerakani, wasweden wapo kwa mujibu wa sheria za uwekezaji..kama humpendi mu-irani fanya hivyo hivyo kwa wazungu..usiwe mnafiki mfano:-

  Huko Arusha asilimia 70% ya makampuni ya uwindaji wa rasilimali yetu katika hifadhi ni "Waingereza".. hao ni wawekezaji? Wazungu

  Huko Pangani wamepokanya almost wilaya nzima wakorea kusini kilimo kwanza..waasia weupe

  Sijaona tatizo la wairan unless una matatizo yako binafsi na sura zenye uislamu ..period

  Sheria ichungulie kwanza proportinality ya wazungu wanaovuna kwenye migodi, ardhi, uwindaji, etc ..wao sawa wairan balaa ..double standards zitawamaliza? wabongo.
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,974
  Likes Received: 21,140
  Trophy Points: 280
  anachopinga mtoa mada ni UKIUKWAJI WA TARATIBU ZA TIC NA UBIA na sio nani kapewa........na vilevile mtoa mada anasema hao WAIRAN wameshusha vitu fulani kwa WAKULU[rushwa??] kwa ajili ya uchaguzi.......bado hujaona tatizo hapo??
  BTW ww ndio unaonyesha mdini kwa jinsi uivyojibu hii mada.kuna maswali mengi tu yakumuuliza mleta mada kabla ya kurukia hoja ya udini.
   
 12. F

  Fanta Member

  #12
  Aug 6, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah Tumain, mbona uko mdini dini kiivyo aisee??
   
 13. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani nafanya jitihada, kulileta hapa maana yangu tushirikiane. Kuna mtu anaweza kuwa na data kamili! Vita ya ufisadi ya mtu mmoja, ni kwa faida yetu wote. Ila mwaka huu, we have to reward Dr. Slaa, Mwalimu Nyerere mwingine ameingia jamani!!!!!!! Uwiiiiiiiiii!!!Go go go Dr!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  ASema usiogope.
  uzalendo ni utayari wa kuitetea nchi yako kwa kila hali.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Watu wengine mnashanga eti Mwalimu Nyerere mwengine ameingia ,hivi huono kama Nyerere ametudumaza ? Watu wanapata uhuru juzijuzi na wameshatupita na wengine hata kombe la dunia wamechezesha ? Naweza kusema Nyerere ameweza kwa 100% kuifanya stability hapa Tz na kuifanya kuwa nchi moja yenye kupigiwa mfano kwa kuwepo kwa amani ndani baina ya wananchi wake ,ila siku hizi mambo yameanza kuharibika.
  Nyerere alikuwa mpigania uhuru ameshapigania tumeupata na yeye amekwenda zake ,sasa hatupiganii tena uhuru hivyo hatuhitaji Nyerere mwengine ,we vipi ???
   
 16. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe. Hata wewe unajua kwamba uhuru tulishapata, kwa hiyo vita kubwa ni ya ufisadi na Dr. Slaa mpaka sasa hivi ndiye Mtanzania pekee anayeonekana kuwa na uwezo wa kupambana na tumuunge mkono kwa hilo. CCM ya Nyerere si ya sasa hivi. Yaani kila zama na kitabu chae! Aluta continua!
   
 17. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa kumbe unaleta tetesi ili mwaka huu tuweze kumreward Dr.Slaa! Nani unadhani anaweza kutupa data kamili?KAm unataka kumweka Dr.Slaa madarakani si lazima kuleta tetesi kwani sifa zake zinajulikana.
   
 18. bona

  bona JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ngoja tusubiri waanze maendeleo ya hayo maeneo then tuconfirm hizi news tusipende kua watu wa ku sensitionalize issues unnecessarily.
   
 19. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2014
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa hilo deni la Mafuta....!! maana tujuavyo mafuta yote huwa tunalipia huu uwendawazimu wa kusema tunadaiwa ni upuuzi usiokubalika.... hata mjinga hawazi kubaliana na hili.... hao waliochukua mafuta ya Iran ndio walipe hilo deni msituletee uchifu mangungu karne hii ya sasa
   
 20. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2014
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndio maana wanang'ang'ana kuichakachua katiba mpya ili wakitoka madarakani tusiwezi kuwatia kitanzi....
   
Loading...