W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani?

Umemwelewa mtoa mada? huko kote unako ongelea mimi sina shida napo,swali langu kwako ni kwamba umemwelewa mtoa mada?

maana hii itakusaidia hata wewe mbeleni kuwa,unapokuwa umeulizwa swali ni vyema ukajikita ktk jibu la swali husika pasi kurefusha jibu na kutoka nje ya mada

- Again read my lips, hata siku moja siwezi kusaini karatasi ya kumpa Waziri anayetuhumiwa wizi nafasi ya kujiuzulu, ningeshauriana na Mh. Zitto, kwenda ambele zaidi kwa kudai wafikishwe kwenye Sheria,

- Nisingeweza kusaini karatasi ya kuwapa mwanya wa kujiuzulu tu! ni utamaduni mbovu sana kwa the future ya taifa letu!

William.
 
Huyu ndiye aliyetaka ridhaa ya kura za wabunge wetu kutuwakilisha bunge la East Afrika, sasa kwa mtazamo kama huu ambao hata ile tunaita common sense tu inateleza, tungewakilishwa na mtu wa aina gani?

heheheeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

inawavua watu nguo! KWELI HUYU WILLIAM HANA TOFAUTI NA KIGWANGALA I VEMA ASINGEKUBALI KUJIINGIZA KATIKA MEGO HUU KUMBE NI WALE WALEE!!!!!!!!!!

JE MWAJUA RAIS BADO ANAZO NAFASI 7 ZA KUTEUA WABUNGE ILI WAWE MAWAZIRI, LABDA BAADA YA HUYU KUSHINDWA KUJIELEZA BUNGENI NA ILI KUTEULIWA KUWA MBUNGE WA SHIRIKISHO LA A MASHARIKI

KILICHOBASKI ANAJARIBU KUCHEZA NA AKILI YA JK ILI AMTEULE ALE ZAIDI KULIKO NGEREZA KWA MGONGO WA SHERIA,

JIMBO LA MTERA KUMBE BADO HALIJAPATA MTU STAHIKI 2015 HEBU WENGINE ZAIDI WAJITOKEZE!
 
- Siwezi kutetea Waziri mwizi hata siku moja au kiongozi yoyote mwizi, lakini ni lazima kuwepo na legal facts kwa mbunge wa jamhuri kufikia kumuita waziri mwizi, kwa sababu sasa unaichokonoa Serikali, CAG imetoa hesabu, kama ilivyokuwa kule Ubalozi wa Italy, walitoa mahesabu ikawa kazi ya DPP kutengeneza LEGAL FACTS, kesi ikaenda kwenye sheria!

- Unajua sometimes unaweza ukawa emotional na ukaishia kuharibu kila kitu, kama kuna mawaziri wezi na facts zipo, dawa ni kulilia kesi mahakamani kwanza, ama sivyo unawapa nafasi ya kujiuzulu tu na basi, ni utamaduni mbaya sana!

William.

Hauwezi kutetea waziri mwizi au kiongozi mwizi sawa nimekusoma ila naomba nikuulize "Hivi wewe ukipata uwaziri hautakuwa mwizi?" Maana unaweza ukawa mstari wa mbele kuwakandamiza mawaziri wezi bungeni,kumbe ikawa ni njia tu ya kuwafanya watu wakuone mwema na haupendi wizi,kumbe na wewe ni bonge la jizi.Ukiwa waziri kupitia CCM asilimia 70 utakuwa mwizi tu!
 
- Mkuu understand kwamba nimepata bahati ya kutembelea 90% ya Dunia, huko kote kwenye nchi zilizo serious na Sheria, CAG inatakiwa kuwa na meno ya kisheria, kubali kwamba hapa Tanzania hatuna hilo ndio maana tupo kwenye hii confusion, taifa haliwezi kuongozwa kwa mashinikizo ya makelele yasiyo na Sheria ndani yake,

- Kubalini kwamba tumekosea sasa turekebishe, huwezi kuwa na CAG isiyo na meno kisheria, infact inaktisha sana tamaa!
William.

Bw Malecela, ulisahau kutembea Uingereza. Kwa nini?
Tazama hapa chini
===============================================
Jeremy Hunt to make statement to Parliament as aide resigns over BSkyB row
Aide to Culture Secretary Jeremy Hunt resigns over 'absolutely illegal' advice emails to News Corporation executives, as cabinet minister prepares to make statement to Parliament.
***********************************************************************
Resignation of Gay Minister Jolts New British Government
By JOHN F. BURNS
Published: May 30, 2010
LONDON - In a political upheaval that shook Britain's new coalition government and prompted fresh debate about the acceptance gays find in the country's public life, a widely admired cabinet minister resigned on Saturday after newspaper disclosures about his taxpayer-refunded rental payments to a long-term gay partner.

British Minister Resigns Over Personal Expenses
By JOHN F. BURNS
David Laws left his post as chief secretary to the treasury after newspaper reports accused him of claiming nearly $60,000 in rent as an official expense.
 
Sasa Bil hivi kwa mfano Mtu unamjua vizuri na all of sudden unamkuta ni owner wa twin tower hivi utakuwa mzushi ukusema kuna kitu illegal anafanya, au facts gani wewe unatafuta?
 
- Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

- Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!

William.

Tulikuwa tunajiuliza kwa nini ulikosa ubunge wakati tulikua tunaamini kuwa wewe ni kijana makini kumbe wewe ni kijana bogasi,
Kama mbunge unawakilisha wananchi inamana kwamba umeaminiwa na kupewa zamana. Kuhiyo ukiwepo bungenei una wakilisha mawazo ya wengi. Wewe kama kiongozi unatakiwa uangalie na upime hoja iliyo wakilishwa inamanufaa gani kwa wananchi wako, kama inagusa maisha yao tetea mpaka mwisho wake bila kuogopa kifo. Badilika jina la baba alitoshi kuwa kigezo cha wewe kupata uongozi watu tunapima mambo mengi kama haya. Chukuwa mfano wa vijana wa mzee mwinyi jina linawasaidia kwa % 2 acha ujinga
 
- Mkuu wangu katika kukaa kwangu kote nje miaka 30, hakuna kitu cha muhimu nilichojifunza kama kutengnisha Sheria na Siasa, ninasema hivi mawaziri wanaotuhumiwa kuiba kama legal facts zipo washitakiwe, kama hakuna waachwe waendelee na kazi zao, lakini siikubali dhana ya kujiuzulu tu ni simply waste!

William.

Unapoongelea siasa kutenganisha na sheria una maana gani? Mwili wako unawaza kubaki hai bila sheria ya maumbile yanayofanya mwili huo uwe hai? Hakuna kitu cho chote duniani kinachoweza kuwa na uwepo bila sheria, hata jiwe lina sheria ya maumbile kubimbirika kwa kufuata gravity hadi litakapofikia sehemu ambayo gravity hairuhusu kuendelea kubimbirika.

Malecela you kidding me? Come on, kama ni kutembea duniani wengi humu jf wametembea na kuona nchi mbalimbali zinazofuata utawala wa sheria na uadilifu wa viongozi, hakuna kulindana katika ukweli. Na kutembea nchi nyingi duniani si kumjengea uwezo mtu kuwa na upeo mkubwa katika kufafanua, kuelewa na kupambanua maisha na masuala ya siasa na utawala, inategemea na uwazi na utayari wa mtu mwenyewe. Wengine wameathiriwa na hulka ya mitandao ya kijamii, mitandao ya kifamilia, mitandao ya kiukoo, mitandao ya kiutajiri, mitandao ya kimaskini, na mitandao ya kutofungamana upande wo wote.
 
- Mkuu understand kwamba nimepata bahati ya kutembelea 90% ya Dunia, huko kote kwenye nchi zilizo serious na Sheria, CAG inatakiwa kuwa na meno ya kisheria, kubali kwamba hapa Tanzania hatuna hilo ndio maana tupo kwenye hii confusion, taifa haliwezi kuongozwa kwa mashinikizo ya makelele yasiyo na Sheria ndani yake,

- Kubalini kwamba tumekosea sasa turekebishe, huwezi kuwa na CAG isiyo na meno kisheria, infact inaktisha sana tamaa!

William.

Halafu penda kuwa mkweli na uwe makini na maneno yako kama ni kweli wewe ni mpenda sheria. 90% ya dunia umeshaimaliza, are you kidding me? Anyway labda sababu ya ubaharia wako ila hiyo haikupi uwezo wa kusema hivyo bwana CHRISTOPHER COLUMBUS! Back to the thread, you need to be bold and critical, i think if you have political ambitions in a nation like the contemporary Tanzania get well prepared, usisome magazeti na hizo experience zako za kuzunguka dunia, kumbuka hapa sio Phillipine au Amerika, hii ni Tanzania inayopitia mageuzi ya haraka ya kisiasa, nchi iliyokuwa na wasomi wa aina mbili, wachache wanaofurahia nchi baada ya kujipendekeza kusimamia ubadhirifu, na wengi waliokaa kimya kuangalia wapi pa kutokea kuwakomboa wananchi, ndo maana leo tunabishana kwa hoja nzito sana, kwa mantiki hiyo ni vizuri kwa sasa ujifunze kujenga hoja nzito sio kuogopa siasa za majina kama unavyosema.
 
Hauwezi kutetea waziri mwizi au kiongozi mwizi sawa nimekusoma ila naomba nikuulize "Hivi wewe ukipata uwaziri hautakuwa mwizi?" Maana unaweza ukawa mstari wa mbele kuwakandamiza mawaziri wezi bungeni,kumbe ikawa ni njia tu ya kuwafanya watu wakuone mwema na haupendi wizi,kumbe na wewe ni bonge la jizi.Ukiwa waziri kupitia CCM asilimia 70 utakuwa mwizi tu!

- Ndio maaana nimeshauri sana mawaziri kuthibitishwa na bunge kwa kufuatilia ripoti za TAKUKURU na Usalama Wa Taifa, kwa sababu ukifanya hivyo utaona kwamba wizi ni tabia ya kuzaliwa nayo, so itakuwa ni vigumu kumpa uwaziri mtu mwenye tabia ya udokozi toka utotoni mwake!

- US kuna wakati jamaa alitakiwa kwenda kuwa Balozi, nchi moja ya Asia kamati ya Bunge ilipompitia ikagundua kwamba alipokuwa mtoto alikuwa na tabia sana ya kuvuta bangi, wakampiga chini kwa dai la kwamba hataisaidia US na tatizo la Bangi toka Panama kuingia US illegally!

I hope umenielewa!

William.
 
Unapoongelea siasa kutenganisha na sheria una maana gani? Mwili wako unawaza kubaki hai bila sheria ya maumbile yanayofanya mwili huo uwe hai? Hakuna kitu cho chote duniani kinachoweza kuwa na uwepo bila sheria, hata jiwe lina sheria ya maumbile kubimbirika kwa kufuata gravity hadi litakapofikia sehemu ambayo gravity hairuhusu kuendelea kubimbirika.

Malecela you kidding me? Come on, kama ni kutembea duniani wengi humu jf wametembea na kuona nchi mbalimbali zinazofuata utawala wa sheria na uadilifu wa viongozi, hakuna kulindana katika ukweli. Na kutembea nchi nyingi duniani si kumjengea uwezo mtu kuwa na upeo mkubwa katika kufafanua, kuelewa na kupambanua maisha na masuala ya siasa na utawala, inategemea na uwazi na utayari wa mtu mwenyewe. Wengine wameathiriwa na hulka ya mitandao ya kijamii, mitandao ya kifamilia, mitandao ya kiukoo, mitandao ya kiutajiri, mitandao ya kimaskini, na mitandao ya kutofungamana upande wo wote.

- Point yangu ni kwamba ninasikitishwa sana kuona wananchi wanakuwa very emotional na kujiuzulu tu badala ya kulilia Sheria kwanza, nili linanisumbua sana maana 90% ya Dunia niliyotembelea wananchi wangedai Sheria kwanza ni sisi tu Tanzania leo mwaka 2012 bado tunalilia mawaziri kujiuzulu tu, that is very disturbing!

William.
 
Ukimaliza ubishi wako jaribu kupitia post zote upate kufunua ubongo zaidi, inaweza kukungezea asilimia moja ukawa na 91% mazee.
 
soma hii uijibu
Kwa kuwa humu jamvini watu wako wazi saana na W J Malecela watu wamekuelekeza labda ukagombee Jimbo la mtera 2015, je kwa hili la wizi na ukosefu wa uwajibikaji wa serikali ungekuwa upande gani? Ungetia saini form ya Zitto au ungelinda chama chenu kama wenzio akina Kingwa?

Utakuwa mbunge wa wananchi au wa chama?
 
Tulikuwa tunajiuliza kwa nini ulikosa ubunge wakati tulikua tunaamini kuwa wewe ni kijana makini kumbe wewe ni kijana bogasi,
Kama mbunge unawakilisha wananchi inamana kwamba umeaminiwa na kupewa zamana. Kuhiyo ukiwepo bungenei una wakilisha mawazo ya wengi. Wewe kama kiongozi unatakiwa uangalie na upime hoja iliyo wakilishwa inamanufaa gani kwa wananchi wako, kama inagusa maisha yao tetea mpaka mwisho wake bila kuogopa kifo. Badilika jina la baba alitoshi kuwa kigezo cha wewe kupata uongozi watu tunapima mambo mengi kama haya. Chukuwa mfano wa vijana wa mzee mwinyi jina linawasaidia kwa % 2 acha ujinga

- Guess what nimesema sana kwamba ukiingia Biashara ya utumbo huwezi kuogopa harufu, hizi ninaita changamoto tu, otherwise ninaamini unaielewa point yangu kwamba siamini kwamba watuhumiwa wanatakiwa kujiuzulu tu, niaaamini wanatakiwa kwenda kwenye Sheria kwanza!, mengine baadaye!

William.
 
uliiona hii post?
Sasa Bil hivi kwa mfano Mtu unamjua vizuri na all of sudden unamkuta ni owner wa twin tower hivi utakuwa mzushi ukusema kuna kitu illegal anafanya, au facts gani wewe unatafuta?
 
Willy anapikwa kuja kuliibia Taifa, Wizi na Ujambazi uliojaa kwenye Serikali dhaifu hauoni. Hufai hata kuwa mjumbe wa nyumba 10 10. Hujachaguliwa kuwa mbunge kwa sasa tayari tumeshakuona upo kimaslai zaidi kuliko kupigania na kuzilinda rasilimali zetu. Ni bora urudi huko melini @ New York, tutakuwa tumepunguza mzigo wa kuibiwa, kuliko kukaa hapa Tanganyika utakuja kutuibia Rasilimali zetu.
 
- Point yangu ni kwamba ninasikitishwa sana kuona wananchi wanakuwa very emotional na kujiuzulu tu badala ya kulilia Sheria kwanza, nili linanisumbua sana maana 90% ya Dunia niliyotembelea wananchi wangedai Sheria kwanza ni sisi tu Tanzania leo mwaka 2012 bado tunalilia mawaziri kujiuzulu tu, that is very disturbing!

William.

Laiti ungejua kwa nini wananchi wanaipenda njia ya kujiuzuru leo usingekuwa kinara wa kupotosha wananchi. Kujiuzuru ni moja ya very legal political remedy wananchi waliyonayo. Kama mkuu wa nchi hataki kumuwajibisha basi wananchi wanaweza kudai hilo kumbuka 'vox populi vox dei'. Shauri yako bana.
 
Kwa kuwa humu jamvini watu wako wazi saana na W J Malecela watu wamekuelekeza labda ukagombee Jimbo la mtera 2015, je kwa hili la wizi na ukosefu wa uwajibikaji wa serikali ungekuwa upande gani? Ungetia saini form ya Zitto au ungelinda chama chenu kama wenzio akina Kingwa?

Utakuwa mbunge wa wananchi au wa chama?

1. For sure nisingesaini kaaratsi ya kuwapa mawaziri kujiuzulu tu, HAPANA NISINGESAINI NO WAY!, NINGEMSHAURI MH. ZITTO, TWENDE MBELE ZAIDI NA KUDAI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE!

2. Hata siku moja siwezi kutetea msimamo wa chama wa kuwalinda mawaziri ambao Sheria imeridhia kuwa ni wezi, unless kama Sheria haijaridhia kama ilivyo sasa!

William.
 
- Siwezi kutetea Waziri mwizi hata siku moja au kiongozi yoyote mwizi, lakini ni lazima kuwepo na legal facts kwa mbunge wa jamhuri kufikia kumuita waziri mwizi, kwa sababu sasa unaichokonoa Serikali, CAG imetoa hesabu, kama ilivyokuwa kule Ubalozi wa Italy, walitoa mahesabu ikawa kazi ya DPP kutengeneza LEGAL FACTS, kesi ikaenda kwenye sheria!

- Unajua sometimes unaweza ukawa emotional na ukaishia kuharibu kila kitu, kama kuna mawaziri wezi na facts zipo, dawa ni kulilia kesi mahakamani kwanza, ama sivyo unawapa nafasi ya kujiuzulu tu na basi, ni utamaduni mbaya sana!

William.

Mkuu bunge ni idara ya kutunga sheria, na sio idara ya kusimamia sheria. Kwa hiyo wabunge hawahitaji mtu kuvunja sheria ili kumshikisha adabu, hata akikiuka adabu na nidhamu, pia anaweza kushikishwa adabu.

Kuna njia nyingi za kuweza kufanya uhuni. Moja ni kufanya usiku na nyingine ni kufanya mchana kweupe kwa kujifunika sura. Kwa namna hii inakuwa ni vigumu kupata ushahidi wa kisheria kama wewe ni mbunge. Lakini kuna njia nyingi tu za kujua mwizi ni nani. Mtu akiwa na nyumba ya shilingi milioni 600 wakati hata mshahara wake na marupurupu yake ya miaka 20 hayafikii nusu ya hiyo, huyo ni mwizi tu. Hata kama ushahidi wa kisheria haupo.
 
Back
Top Bottom