W J Malecela kwa hili la wizi na kutokuwajibika kwa mawaziri ungekuwa upande gani?

Huo ndio ukweli Ndugu yangu. Pale kwa CAG kuna watalaam wengi zaidi wa Mahesabu. Ukipata muda mtembelee Utouh akupe zaidi Info. Serikali ya CCM walifanya makusudi kutoipa uwezo wa kushtaki Ofisi ya CAG maana wanajua wao ndio wangekuwa Victims wa Kwanza.

- Finally, you see my point, saafi sana kwamba sasa unanielwewa kwamba bila Sheria, tunakuwa tunatwanga maji tu kwenye kinu! Mawaziri watuhumiwa watishia kujiuzulu tu sasa tutakuwa tumelisaidia ni nini taifa la kesho?

William.
 
- Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

- Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!

William.

kaka
inamaana hata ile ripoti ya CAG haikuwa na FACT yeyote ile? na vipi kuhusu yule Raia wa pakistan ambae alibeba twiga wawili ,tembo na baadhi ya wanyama? vipi kuhusu tuhuma za TBS wanaotusababishia watanzania kutumia vitu ambavyo ni vya kiwango cha chini na kuleta uongo uliosababisha wajumbe wa kamati kusafiri kutoka tanzania hadi nchi za nje kukagua kampuni hewa za ukaguzi wa magari? bado Usingeweza kuziona FACT mkuu ?

unajuwa bwana kuna mambo yanafanywa na viongozi kiasi kwamba hata kama ni chama chako inakuwa ni ngumu sana kuyavumilia

jifunze kuwa mkweli kwani utakuweka huru daima

angalizo: NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU NI MWIKO
 
CAG amefanya jitihada kubwa mno, na laiti angepewa makucha zaidi ya kuwafikicha wahusika mahakamani muda mrefu angekuwa ameshasafisha safu ya uongozi kwa kiasi fulani. Utaratibu wa kuweka wizara nyeti zote chini ya Office ya Rais kwa tafsiri ni kwamba office ya raisi imeweka rasimu ya kuwalinda wahujumu uchumi nchini.

CAG kwa dhamiri alipoona mambo yanazidi kuharibika bila hatua kuchukuliwa ndipo alipoamua kugeukia kwenye mhimili wa Bunge kuokoa jahazi. CAG imejitahidi kuokoa jahazi so far.

- So we have a good case at hand ya kudai Sheria mpya ya kuiunganisha CAG na Sheria, ili tusifikie tena confusion kama tuliyonayo sasa!

William.
 
- Hizi ni siasa at best, mkuu kwenye modern politics tunataka Sheria, kama unayosema ni kweli mbona leo tuna ATC ambayo haina ndege? I mean Sheria kwanza mkuu siasa pembeni!

William.

Wakati ule kosa moja halikuvumiliwa kwa sababu ya kujali kulinda rasilimali za nchi. Leo mnasema mnataka legal facts na matokeo ndio hayo shirika la ndege limefilisika, wakati kipindi cha awamu ya kwanza karibu nusu ya mkoa ya Tanzania ilikuwa inajivunia huduma ya shirika la ndege Tanzania na hata kuwa na route za UK na Uarabuni. Jenga utetezi mwingine hapa umeteleza. Hizo taratibu za legal facts ndizo zilizoua mashirika ya umma kwa kulindana.
 
Hapa naona tunampigia mbuzi gitaa, in short Willie asingesupport move in a simple analysis because of the facts he has given already, simply asingesupport. The question remains je sheria anayotaka yeye peke yake kwa mtazamo wake ingekuwepo je angefanyaje? Ila ashasema anaogopa siasa za majina which implies that he knows nothing of ministerial responsibility whether individual or collective responsibility which is the main pillar on check and balance. There are so many political remedies out of court yeye anaziona sio 'modern', hakuna haja ya kumuelimisha mtu huyu zaidi ya yeye kusubiri akapambane na Lusinde wakati CDM wapo pembeni wanachukua jimbo! Shauri yake!
 
- Kwanza ningedai FACTS, so far sijaziona zote na very clear of what happened and what did not happen, with FACTS at hand kwanza ningerudi jimboni kwangu kuwafahamisha wananchi FACTS za kilichotokea na kuwauliza nini msimamo wao kwanza, maana ni wao ndio ninaowawakilisha kule Bungeni!

- Unajua unapomtuhumu Waziri wizi ni lazima kuwepo na Legal Facts, kwa sababu muhimu hapo ni historia ya mbele ya safari, unajenga utamaduni wa kujali sheria, kwa hiyo unatakiwa umakini sana kwenye conclusion kwamba kweli ni wezi, siamini kuwa kama FACTS zipo clear, kuna kiongozi yoyote bungeni angeshindwa kusaini!

William.

Kwani pale uliitaji fact gani? Maana CIG kaweka wazi kila kitu na pia huo muda wa kurudi kwa wananchi wako kuwauliza muda si ungekua umekwisha? Bado embu jitetee tena vizuri na kwa makini zaidi!
 
kaka
inamaana hata ile ripoti ya CAG haikuwa na FACT yeyote ile? na vipi kuhusu yule Raia wa pakistan ambae alibeba twiga wawili ,tembo na baadhi ya wanyama? vipi kuhusu tuhuma za TBS wanaotusababishia watanzania kutumia vitu ambavyo ni vya kiwango cha chini na kuleta uongo uliosababisha wajumbe wa kamati kusafiri kutoka tanzania hadi nchi za nje kukagua kampuni hewa za ukaguzi wa magari? bado Usingeweza kuziona FACT mkuu ?

unajuwa bwana kuna mambo yanafanywa na viongozi kiasi kwamba hata kama ni chama chako inakuwa ni ngumu sana kuyavumilia

jifunze kuwa mkweli kwani utakuweka huru daima

angalizo: NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU NI MWIKO

- Ripoti ya CAG ingekua na legal facts, na kungekuwepo Sheria ya kuiunganisha CAG na Sheria, tusingekua tunabishana hapa, ninashangaa sana kwamba tuna sheria ya kuwa na CAG, lakini hatuna Sheria ya kuwapa meno kisheria,

- sasa nini faida hata ya kuwa nao CAG as a nation?

William.
 
Wakati ule kosa moja halikuvumiliwa kwa sababu ya kujali kulinda rasilimali za nchi. Leo mnasema mnataka legal facts na matokeo ndio hayo shirika la ndege limefilisika, wakati kipindi cha awamu ya kwanza karibu nusu ya mkoa ya Tanzania ilikuwa inajivunia huduma ya shirika la ndege Tanzania na hata kuwa na route za UK na Uarabuni. Jenga utetezi mwingine hapa umeteleza. Hizo taratibu za legal facts ndizo zilizoua mashirika ya umma kwa kulindana.

- Mkuu ndio maana huwa ninasema sana kwamba Awamu ya kwanza ilikuwa na mapungufu sana ya kutoheshimu sheria, either kwa makusudi au kutokujua ndio maana mpaka leo inapokuja ishus za kisheria tunaleea hewani sana,

- I mean unawezaje kuwa na CAG, ambayo haina meno ya kisheria ya kumuwajibisha mtuhumiwa? Kama huwezi kuwa na Sheria ya kuwapa meno CAG ni bora kutokuwa nao kabisa!

William.
 
Bwna Malecela nimekuuliza, ningeomba ujibu post yangu, wewe ni mwanasheria? Unadhani kila kitu lazima kihukumiwe kisheria?
 
Je wanapaswa kuwajibishwa o noT
- Hapana kwangu the ishu ni sheria, kama mawaziri ni wezi kuwepo na njia ya moja kwa moja ya kuwafikisha kwenye Sheria bila ku-negotiate nao kama tunavyofanya sasa, sio modern politics hizo mkuu wangu! Nchi zote zilizoendelea Duniani hao mawaziri sasa hivi wangekwua kwenye sheria sio kwenye makelele ya siasa!

William.
 
Hapa naona tunampigia mbuzi gitaa, in short Willie asingesupport move in a simple analysis because of the facts he has given already, simply asingesupport. The question remains je sheria anayotaka yeye peke yake kwa mtazamo wake ingekuwepo je angefanyaje? Ila ashasema anaogopa siasa za majina which implies that he knows nothing of ministerial responsibility whether individual or collective responsibility which is the main pillar on check and balance. There are so many political remedies out of court yeye anaziona sio 'modern', hakuna haja ya kumuelimisha mtu huyu zaidi ya yeye kusubiri akapambane na Lusinde wakati CDM wapo pembeni wanachukua jimbo! Shauri yake!

Ni kweli kwani kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho. Kwa wenye jicho la kuona mbali unaweza jifunza kitu fulani cha kumsoma mtu, na huyu ndiye tuliyemtegemea kuwa atuwakilishe kwenye bunge la Jumuiya ya East Africa, na angetuwakilishwa kwa kiwango hiki anachochangia hapa, hapo kazi tunayo, na nasikitika kutamka wazi hawakufanya makosa.
 
Kwani pale uliitaji fact gani? Maana CIG kaweka wazi kila kitu na pia huo muda wa kurudi kwa wananchi wako kuwauliza muda si ungekua umekwisha? Bado embu jitetee tena vizuri na kwa makini zaidi!

- Mkuu understand kwamba nimepata bahati ya kutembelea 90% ya Dunia, huko kote kwenye nchi zilizo serious na Sheria, CAG inatakiwa kuwa na meno ya kisheria, kubali kwamba hapa Tanzania hatuna hilo ndio maana tupo kwenye hii confusion, taifa haliwezi kuongozwa kwa mashinikizo ya makelele yasiyo na Sheria ndani yake,

- Kubalini kwamba tumekosea sasa turekebishe, huwezi kuwa na CAG isiyo na meno kisheria, infact inaktisha sana tamaa!

William.
 
Nilikuwa nakufuatilia tuu nione watu watasema nini na response yako, kwahiyo ungukuwa MB wa mtera usingesaini au ungesaini, au ndio ungesubiri legal proof, i mean usubiri mtu ashitakiwe ashinde ndio u vote?

Miaka mingapi hiyo kwa huku kwetu TZ, nadhani itakuwa kama miaka mitatu hivi mmmmh!
 
Ni kweli kwani kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho. Kwa wenye jicho la kuona mbali unaweza jifunza kitu fulani cha kumsoma mtu, na huyu ndiye tuliyemtegemea kuwa atuwakilishe kwenye bunge la Jumuiya ya East Africa, na angetuwakilishwa kwa kiwango hiki anachochangia hapa, hapo kazi tunayo, na nasikitika kutamka wazi hawakufanya makosa.

- Ha! ha! ha! ha! kuna nafasi nyingi sana za uongozi wa taifa letu sio EAC tu, so get ready maana nipo bado siendi kokote, Dunia nzima inatawaliwa kwa Sheria sisi tu ndio bado leo 2012 tunatywalana kwa makelele, inasikitisha sana, wananchi badala ya kulilia Sheria wanalilia mawaziri kujiuzulu tu, inasikitisha sana!

William.
 
Kwa kuwa humu jamvini watu wako wazi saana na W J Malecela watu wamekuelekeza labda ukagombee Jimbo la mtera 2015, je kwa hili la wizi na ukosefu wa uwajibikaji wa serikali ungekuwa upande gani? Ungetia saini form ya Zitto au ungelinda chama chenu kama wenzio akina Kingwa?

Utakuwa mbunge wa wananchi au wa chama?

- Ripoti ya CAG ingekua na legal facts, na kungekuwepo Sheria ya kuiunganisha CAG na Sheria, tusingekua tunabishana hapa, ninashangaa sana kwamba tuna sheria ya kuwa na CAG, lakini hatuna Sheria ya kuwapa meno kisheria,

- sasa nini faida hata ya kuwa nao CAG as a nation?

William.

Umemwelewa mtoa mada? huko kote unako ongelea mimi sina shida napo,swali langu kwako ni kwamba umemwelewa mtoa mada?

maana hii itakusaidia hata wewe mbeleni kuwa,unapokuwa umeulizwa swali ni vyema ukajikita ktk jibu la swali husika pasi kurefusha jibu na kutoka nje ya mada
 
- Finally, you see my point, saafi sana kwamba sasa unanielwewa kwamba bila Sheria, tunakuwa tunatwanga maji tu kwenye kinu! Mawaziri watuhumiwa watishia kujiuzulu tu sasa tutakuwa tumelisaidia ni nini taifa la kesho?

William.

Kumbe unajua katika hali ya sasa mawazili wanaweza kuishia kujiuzulu, sasa huoni kuwa kujiuzulu kwao baada ya kutuhumiwa ni moja ya vigezo muhimu kwa wao kuwapeleka mahakamani? The fact that a person is of bad character inakuwa admissible kukazia ushahidi, sasa kama alifikia kujiuzuru kwa madudu ya wizara yake inatosha kuisaidia mahakama kumtia hatiani mkuu. We endelea kuisubiri hiyo sheria ya kumpa nguvu CAG wakati kuna remedies kibao. Unaposema unaogopa kutoa maamuzi ya kisiasa kwenye ishu za kisheria kumbuka siasa imo kisheria ndo maana katiba pekee inaweza kutumika hapo na principles of administrative law! Waziri anapotoa maamuzi kuidhinisha mambo ya wizara anakuwa 'functus officio' hakuna haja ya kupindapinda kona katika kumuadhibu na wanayajua hayo na pia wameajiri wataalamu wengi tu anaweza kuwatumia vizuri. Ninachokiona hapo ni kuwa wanapoona kuna maslahi yao binafsi ndipo hufanya ubabe sasa kwa nini uogope kumuwajibisha mtu kama huyo? Kwa nini uogope jina lake? Be smart my friend, taifa la sasa sio la enzi ya mwalimu.
 
Bwna Malecela nimekuuliza, ningeomba ujibu post yangu, wewe ni mwanasheria? Unadhani kila kitu lazima kihukumiwe kisheria?

- Mkuu wangu katika kukaa kwangu kote nje miaka 30, hakuna kitu cha muhimu nilichojifunza kama kutengnisha Sheria na Siasa, ninasema hivi mawaziri wanaotuhumiwa kuiba kama legal facts zipo washitakiwe, kama hakuna waachwe waendelee na kazi zao, lakini siikubali dhana ya kujiuzulu tu ni simply waste!

William.
 
- Mkuu ndio maana huwa ninasema sana kwamba Awamu ya kwanza ilikuwa na mapungufu sana ya kutoheshimu sheria, either kwa makusudi au kutokujua ndio maana mpaka leo inapokuja ishus za kisheria tunaleea hewani sana,

- I mean unawezaje kuwa na CAG, ambayo haina meno ya kisheria ya kumuwajibisha mtuhumiwa? Kama huwezi kuwa na Sheria ya kuwapa meno CAG ni bora kutokuwa nao kabisa!

William.

  • Mbona unajikanganya, unasema awamu ya kwanza ilikuwa na mapungufu kuliko sasa?
  • Haya mashirika ya umma yalifilisika awamu ya kwanza au awamu hizi ambapo mnajidai kufuata legal facts?
  • Unapima ubora wa awamu kwa mafanikio au kwa mwanguko?
  • Umeelewa nilivyokuletea mifano ya mawaziri waliowajibishwa na kusaidia kujenga nidhamu ya utendaji katika awamu ya kwanza na ya pili?
  • Kwa mtazamo wako kiongozi kama legal facts haziko wazi lakini wizara inazidi kuharibika abaki akilindwa kwa sababu ya legal facts?
  • Uwajibishwaji uliokuwa ukifanywa na awamu ya kwanza au ya pili ulijikita kwenye mamlaka aliyopewa rais kuongoza nchi na rungu hilo ndilo lililo waadabisha watendaji serikalini.
 
- Ha! ha! ha! ha! kuna nafasi nyingi sana za uongozi wa taifa letu sio EAC tu, so get ready maana nipo bado siendi kokote, Dunia nzima inatawaliwa kwa Sheria sisi tu ndio bado leo 2012 tunatywalana kwa makelele, inasikitisha sana, wananchi badala ya kulilia Sheria wanalilia mawaziri kujiuzulu tu, inasikitisha sana!

William.

wakati unafanya ukarabati wa bomba la maji,ni lazima kwanza uzibe pale panapo vuja ili bomba hilo utakaloliziba likusaidie kupata bomba jipya

hatuwezi kulilia sheria wakati hao watunga sheria baadhi yao ni wabadhilifu, kwa hiyo wakati tunalia watoke huku tunajiandaa na katiba mpya ndani yake tutaweka yafuatayo

1.si ruksa kwa waziri kutokana na wabunge
2.si ruksa kwa wabunge kuwa wenyeviti wa makampuni ya umma
3.CAG apewe uwezo wa kuwashitaki wale wote watakao kutwa na makosa
 
Back
Top Bottom