Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,883
Wizara ya elimu ya juu haina budi kubuni kuiga mazuri toka nchi nyingine ili kuunda mfumo wa elimu ya juu kwa mfumo wa kuwaunda wanafunzi kitaaluma, kimaadili ili kujenga vema future yao. Kiwango cha wahitimu wengi vyuo vikuu ni cha chini sana hilo limekuja onekana tokana na SAUT kutangaza idadi kubwa ya mamia wa wanachuo ambao wamepigwa chini kutopata graduation sababu mojawapo ni academically issue.
Oral communication through English Language ambayo ni keyboard language for their studies, ukiongea nao kiingereza utaona wanavyojiuma ulimi, nashangaa how they communicate in their classes, groups and researches. Mabingwa sana wa kusahihisha spelling, lakini kwenye communication terrible, ambapo vyuoni effective speaking ni moja ya kitu muhimu katika masomo, majadiliano na kujenga hali ya kujiamini kabla ya graduation. Hawa ndio tunaowatazamia kuwa viongozi na pengine kutuwakilisha katika mataifa ya nje kwa shughuli mbalimbali za kibishara na shughuli za serikali.
Nikianzia na mfumo wa elimu vyuo vikuu nchini ambao unajali zaidi mwanachuo amefanya assignments badala ya mahudhuria darasani ni dosari kubwa ambayo inaweza kusababisha mwanafunzi asipate elimu stahiki ila mradi amefanya class assignments kwamba ni kutoka kichwani mwake, au rafiki yake au pengine instructor what ever inamwathiri sana mwanachuo.
Kinachoshangaa wanachuo Tanzania utawaona siku za kawaida ambapo wanatakiwa wawepo madarasani utawaona wengi tu wakirandaranda mitaani, au maeneo ya chuoni wakati wenzao wako madarasani. Mfumo huu una kasoro kubwa kwa utoaji elimu bora, na pengine ndio moja ya chanzo cha kiwango cha elimu vyuo vikuu kuwa cha kujipakaa kwa nje na kuvaa majoho tu badala ya elimu hiyo inayotakiwa iwe soaked into their brain. You can find out that their brain folders are empty because they do not attend classes.
Marekani mfano mzuri wa utoaji elimu bora kwa mwanachuo
Nikichukulia nchi ya Marekani katika mfumo wake wa utoaji elimu kwa wanachuo, mfumo upo wa kuwabana sana wanachuo mahudhurio darasani licha ya academical results. Mfumo wa utoaji asilimia za credits zinategema:
Mahudhuriao darasani;
Mwanachuo anatakiwa asikose mahudhuria darasani, na ikitokea kwa ruhusa maalum kwa sababu maalumu darasa hilo anatakiwa awasiliane na instructor aweze kupanga muda kufanya full kufidia.
Kama mwanachuo atakosekana darasani siku tatu au nne atakuwa terminated katika kozi hiyo na hivyo kupata hasara ya tuition aliyolipia kwani hatarudishiwa zote ila makato ni makubwa kusajiliwa upya kwa gharama mpya katika semester inayofuata.
Assignments & Final exam: Kama mwanachuo atakosekana darasani siku tatu au nne atakuwa terminated katika kozi hiyo na hivyo kupata hasara ya tuition aliyolipia kwani hatarudishiwa zote ila makato ni makubwa kusajiliwa upya kwa gharama mpya katika semester inayofuata.
Mfumo wao mwanachuo hata kama atafanya vizuri katika assignments/tests and final exam ambapo ni wastani wa 70% ya 100% ya all field hawezi kufaulu kwa sababu one third lazima itoke kwenye mahudhurio darasani (class attendance). Wastani wa kufaulu wa class attendance, assignments/tests and final exam ni above 75%, maana yake kati ya hayo matatu moja likikosekana au kutofikiwa wastani wa wakila aspect, utakuwa umeshindwa kiwango cha ufaulu chuoni, ingwa kiwango hupishana kidogo baina ya vyuo kadiri ya board of education ya chuo, lakini basically utaratibu ndio huo.
Lengo la body of education ni kuhakikisha wanachuo wanapata elimu kwa uhakika si kusoma tu kwa ajili ya kufaulu. Mwanafunzi anayekaa darasani, kumsikiliza instructor, kuuliza maswali na kujadiliana na wenzake uelewa wake ni mkubwa kuliko anayejisomea mwenyewe kwa sababu hana nafasi ya challenge ya anayosoma. Ndio maana vyuoni mafunzo ya vikundi yanatiliwa muhimu hata madarasani utaona instructors wanawagawa wanafunzi katika makundi ili kufanya baadhi ya assigments kivikundi.
Eneo mojawapo ambalo halijapewa uzito stahiki katika elimu nchini iwe shule za msingi, sekondari na vyuo ni sports education. Eneo hili lina nafasi kubwa sana katika social aspect licha ya kuwasaidia wanafunzi kisaikolojia na kielimu. Vyuo vingi nchini ni elimu darasani tu na baada ya hapo utaona wanachuo hawana cha kufanya zaidi wasichana kuanza kujiingiza kwenye uwanja wa kujigeuza bidhaa kwa wateja mitaani na maeneo ya stareh na vijana wengine kuwa katika makundia mbayo yanawafikisha kujifunza na kufanya yasiyotemewa. Vyuo vya majuu utaona wanachuo wengi wapatapo nafasi ni mazoezi yakufa ya viungo, kukimbia na kadhalika kujiweka sawa kimaungo na walio katika michezo ni sehemu ya mazoezi na wanapangiwa KM za kukimbia na huwa recorded mazoezi hayo kwenye credits za chuo.
Michezo husaida mengi kama baada ya uchovu wa kiakili ni refreshment, darasa hufanya watu wasiwe active katika miili yao, hivyo michezo huwasaidia kujengeka kimwili na kiakili. Michezo huwasaidia kujenga ubunifu, maana katika michezo licha ya mafunzo hutakiwa ubunifu wa papo kwa papo kutokana na ushindani mchezoni. Michezo vyuoni huibua vipaji vya mastaa mbalimbali wa michezo duniani, kwani wa vyuoni hufundishika vizuri zaidi na kuelewa maelekezo na vielelezo kuliko wa mitaani wasioelimika. Wanamiziki wengi wametokea vyuoni au wamekuza vipaji vyao vyuoni.
Niliposoma kuanzia shule za msingi hadi juu kipindi changu kulikuwa na msisimko wa michezo mashuleni isivyo kawaida. Hali hiyo imekufa ghafla na nilikuja kukumbushwa kitu hicho nilipokuwa chuoni Marekani kuona michezo mashuleni pengine hufunika hata ligi kubwa. Tunahitaji kurudi nyuma kujadili nini kimekwamisha hayo.
Kwa vyo vyote kuna mengi ambayo yanachangia kudorora kwa elimu vyuoni hata shule za awali.