Vyuo vya Uandishi wa Habari na Utangazaji havitoi bidhaa zenye ushindani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vya Uandishi wa Habari na Utangazaji havitoi bidhaa zenye ushindani.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Radio Producer, Oct 2, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wadau,

  Leo napenda kutoa machache kuhusu vyuo vya uandishi wa habari na utangazaji hapa Tanzania kuanzia ngazi ya cheti na hata ngazi ya juu. Ukweli usiopingika bidhaa au wanafunzi wanaotoka katika vyuo vyetu wengi wao hawana kabisa competence na hali hii imefanya tanisia ya habari kudharauliwa na kuwa haina kitu. Mfano mzuri unaweza kuanzia tu pale unapopokea wanafunzi wa field, kiukweli unaweza kushangaa mtu amekuja kufanya mazoezi hajui hata pakuanzia, unadhani kwa hali hii ataenda kuwa na ushindani sokoni?

  Matatizo yanayochangia.
  1. Mifumo isyokidhi viwango ya ufundishaji katika vyuo. Nimejaribu kutembelea vyuo vingi kwakweli tunahitaji sana kujitahidi watanzania. Vyuo vingi vimeazimana mitaala ya kufundishia na kuiagana bila kujiuliza na kudesign mitaala inayoendana na muda na mazingira. Unajua unatakiwa kufikiria kwanza unataka kutoa product gani? Wengi tunataka kutoa wanafunzi wanaojua kila topic ili tuonekane wataalamu na ndipo tunapojikuta tunatoa vifaa ovyo kabisa.
  Ushauri hapa ni kutengeneza mitaala inayokidhi mahitaji ya viwanda wanavyoenda kufanyia kazi.

  2. Ukosefu wa vifaa vya kufundishia, hili linachangia sana, chuo kinafundisha utangazaji mpaka mwanafunzi anamaliza chuo microphone ameiona kwenye kitabu tu? Mixer ndo anaisikia tu? Hatari sana. Jitahidini wenye vyuo mtengeneze angalau studio zenye gharama nafuu hata milion 2. Simanishi radio ya kurusha matangazo namanisha studio ya kuandalia vipindi na mazoezi.

  3. Vyuo vingi havifundishi Radio Production. Siwezi kukuficha kama mwanafunzi hajasoma radio production kiukweli sokoni atatembea mpaka atachoka tu kama si kuhonga rushwa ya ngono. Hiki kitu ni muhimu sana, nimejaribu mwenyewe kufundisha hizi kozi kwa muda wa mwezi 1 nimeamini hizi ni kozi muhimu, wote niliowafundisha walienda sokoni kwa kasi sana na mpaka sasa wanafanya kazi zao vizuri na radio hizo.

  Nawashauri wenye vyuo tufundisheni uhalisia wa kozi hizi na si theory na kuiagana.

  Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri na msaada zaidi.
  Website: Radio Consult Company Limited
  Email: consultancy@radiotz.com
   
 2. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Vyuo ni vingi sana na watangazaji ni wengi sana ila ushindani ndiyo hakuna kabisa.
   
Loading...