Ni kweli nilikuwa nje. Nikasoma huko nikarudi na tumawazo twangu tupya. Kazini pale kuna tuzee tumeshikilia usukani na tunaendesha mambo kwa nadharia na fikra za miaka ya 70. Nilikuwa frustrated nikaviacha. Sasa niko mtaani huku naisoma namba. Ukija na mawazo yako mapya halafu ukagusa ulaji wa watu unaweza hata uka-restishwa in peace usipokuwa mwangalifu. Yule daktari bingwa wa moyo na hospitali yake ya moyo alikuja na moto kufungua hospitali ya rufaa yenye uwezo wa kufanya operesheni kubwa kubwa za moyo hapa hapa nchini akishirikiana na madaktari wenzake kutoka Texas. Kumbe anaingilia ulaji wa watu na safari zao za kwenda kutibiwa nje. Unajua kilichompata? Kanchi haka kaone hivi hivi tu mkuu japo mambo yanabadilika pole pole. Tuwe na subira!
Wasmehe bure...Wametoka mbali na maslahi ya kustaafu bado ni mabaya lakini mbona wengine tumevumilia na kidogo tume impose some changes?