Vyuo vya Tanzania vyafanya vibaya kwenye Takwimu za kimataifa

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,357
2,000
Kuna uwezekano karibu vyuo vyote vya TZA vinazalisha vilaza wa kutosha kwani kwa mujibu wa takwimu la shirika la URAP (University Ranking by Academic Perfomance) inaonyesha ni vyuo viwili tu vilivyopo kwenye top 68 ya vyuo bora afrika.

Chuo cha kwanza ni UDSM ambacho kwa Afrika kimeshika nafasi ya 48 kati ya 68 na kidunia ni nafasi ya 1738, kikifuatiwa na chuo kikuu cha kilimo cha sokoine (SUA) kilichoshika nafasi ya 58 kati ya 68 kwa Afrika na kidunia ni 1836.

Ambapo Makerere cha Uganda kikishika nafasi ya 9 na chuo kikuu cha Nairobi kikishika nafasi ya 25, kwa hiyo kwa nchi tatu za Afrika mashariki yaani Kenya, Uganda na Tanzania, TZ ndo ina vyuo vibovu na elimu mbovu ukilinganisha na wenzetu.

Kwenye Takwimu za vyuo bora 30 vya Afrika za Times Higher Education(THE) Hakuna hata chuo kimoja cha kutoka Tanzania huku vyuo vya Makerere na Nairobi vikiwepo kwenye list.

Tanzania ni kichwa cha mwendawezimu kwenye kila sekta?

URAP - University Ranking by Academic Performance
Top 30 African universities: Times Higher Education reveals snapshot university ranking
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,710
2,000
Fanya yako sepa ukijilanganisha na watu utaishia kujishusha tu thamani afterall huihitaji elimu kubwa sana kusurvive kwenye nchi kama Tanzania... Nasioni maendeleo waliyoyaafanya hao viongozi waliopita waliosoma nje na waliosoma kipindi ambacho wanahisi elimu ilikua bora zaidi... Tumejivunia ufisadi, kufa kwa viwanda, na madaraja katika jamii.
 
Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Hapo UDSM kelele nyingi lakin kwa Africa bado hali ni mbaya, sasa sjui hao wa Saut na vyuo vingine wanachukuliwaje aki na sjui wana pataga wapi uwezo wa kusifia vyuo vyao.

There is something wrong with our education, Lowassa alisema tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elim tu, yaani kama vile tulivo jadili katiba, kwa hapo namuunga mkono
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,357
2,000
Fanya yako sepa ukijilanganisha na watu utaishia kujishusha tu thamani afterall huihitaji elimu kubwa sana kusurvive kwenye nchi kama Tanzania... Nasioni maendeleo waliyoyaafanya hao viongozi waliopita waliosoma nje na waliosoma kipindi ambacho wanahisi elimu ilikua bora zaidi... Tumejivunia ufisadi, kufa kwa viwanda, na madaraja katika jamii.
Hapana kwa kweli llazima tujiangalie hiwezekani Makerere wawe na uwezo wa kutengeneza gari inayotumia umeme wa jua project ambayo imewapaisha sana halafu sisi turidhike yaaani.
 
maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,210
2,000
Tuangalie taarifa kama hizi zinatolewa na nani na kwa sababu gani. Viko vyuo kila leo migomo na product zao tunafanya nazo kazi. Hamna chochote. Tanzania wahitimu wake wanang'ara dunia nzima.
Naona humu watu ambao hata shule zao zinatia shaka wanacomment kuhusu elimu ya chuo kikuu.
Sisi tunaotembelea vyuo vya ndani na nje tunajua uwezo wa vyuo vyetu na tunawaambia tupo juu.
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
129,223
2,000
Hapo UDSM kelele nyingi lakin kwa Africa bado hali ni mbaya, sasa sjui hao wa Saut na vyuo vingine wanachukuliwaje aki na sjui wana oataga wapi uwezo wa kusifia vyuo vyao.

There is something wrong with our education, Lowassa alisema tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu elim tu, yaani kama vile tulivo jadili katiba, kwa hapo namuunga mkono
Subiri tamko next week kuhusu hii ishu. May be watawataka ma- lecturer na maprofesa wote kuchapisha angalau papers tatu kwenye reputable peer-reviewed international journals ili kuboost profile ya chuo. Ukishindwa unatumbuliwa.

Sekta ya elimu kote duniani ndiyo mkakati mama wa UKOMBOZI wa taifa lakini sisi tumeugeuza uwanja wa wanasiasa. Kwingineko kote mabadiliko katika mfumo wa elimu hayafanyiki bila utafiti wa kina na mara nyingi unafanywa na kupendekezwa na jopo la wataalamu maalumu wa masuala mbalimbali ya elimu wakiwemo waalimu wenyewe na hata wanafunzi. Sisi wala. Akija Mkenya Mungai anafanya yake. Akija Mulugo mzee wa Zanzibar na Zimbabwe anafanya yake. Akija Makweta anaamua yake. Prof aliyepo naye anafanya yake. Atakayekuja naye atafanya yake. Tutaendelea saa ngapi? Leo hii tunafuta masomo ya sanaa. Pengine tutakuwa taifa la kwanza duniani lenye wanasayansi tupu. Tazama hata sera yetu ya lugha ya kufundishia.

Wataalamu wa Psycholinguistics na Language Acquisition wanasema kuwa muda mzuri wa mtoto kujifunza lugha na kuimudu sawasawa ni kuanzia miaka 0-14. Sisi tunapoteza kipindi hiki muhimu tukimhangaisha mtoto katika lugha moja na kumhamisha tena kwenda nyingine. Matokeo yake wasomi wetu hawana lugha yo yote wanayoimudu sawasawa si Kiswahili wala Kiingereza. Ni vurugu tupu. Ndiyo maana wasomi wetu hawawezi ku-reason at the deepest level kwa sababu fikra huchanuzwa kupitia lugha na bila welewa wa lugha sawasawa ni vigumu sana kufikiri kwa kiwango cha ndani kabisa kabisa. Halafu tunalalamika kwa nini hatuna critical thinkers na watu wenye maono ya kututatulia matatizo yetu.

UDSM sasa imeingiliwa na siasa na hakuna tena la maana pale. Hovyo kabisa !!!
 
maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,210
2,000
Kama PhD holder anasumbuliwa na lugha aliotumia kwa zaidi ya miaka 20. Unategemea hivyo vyuo kuzalisha wanafunzi bora na kutoa elimu bora?
Kwani PhD yake ni ya lugha?
Kwani kuwa na lugha nzuri ni kuelimika?
Tunawajua watu wenye kiingereza kizuri na vichwa vyeupe.
 
Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Subiri tamko next week kuhusu hii ishu. May be watawataka ma- lecturer na maprofesa wote kuchapisha angalau papers tatu kwenye reputable peer-reviewed international journals ili kuboost profile ya chuo. Ukishindwa unatumbuliwa.

Sekta ya elimu kote duniani ndiyo mkakati mama wa UKOMBOZI wa taifa lakini sisi tumeugeuza uwanja wa wanasiasa. Kwingineko kote mabadiliko katika mfumo wa elimu hayafanyiki bila utafiti wa kina na mara nyingi unafanywa na kupendekezwa na jopo la wataalamu maalumu wa masuala mbalimbali ya elimu wakiwemo waalimu wenyewe na hata wanafunzi. Sisi wala. Akija Mkenya Mungai anafanya yake. Akija Mulugo mzee wa Zanzibar na Zimbabwe anafanya yake. Akija Makweta anaamua yake. Prof aliyepo naye anafanya yake. Atakayekuja naye atafanya yake. Tutaendelea saa ngapi? Leo hii tunafuta masomo ya sanaa. Pengine tutakuwa taifa la kwanza duniani lenye wanasayansi tupu. Tazama hata sera yetu ya lugha ya kufundishia.

Wataalamu wa Psycholinguistics na Language Acquisition wanasema kuwa muda mzuri wa mtoto kujifunza lugha na kuimudu sawasawa ni kuanzia miaka 0-14. Sisi tunapoteza kipindi hiki muhimu tukimhangaisha mtoto katika lugha moja na kumhamisha tena kwenda nyingine. Matokeo yake wasomi wetu hawana lugha yo yote wanayoimudu sawasawa si Kiswahili wala Kiingereza. Ni vurugu tupu. Ndiyo maana wasomi wetu hawawezi ku-reason at the deepest level kwa sababu fikra huchanuzwa kupitia lugha na bila welewa wa lugha sawasawa ni vigumu sana kufikiri kwa kiwango cha ndani kabisa kabisa. Halafu tunalalamika kwa nini hatuna critical thinkers na watu wenye maono ya kututatulia matatizo yetu.

UDSM sasa imeingiliwa na siasa na hakuna tena la maana pale. Hovyo kabisa !!!
Mkuu kama uko nje ya nchi hebu rudi usaidie taifa lako
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
129,223
2,000
Mkuu kama uko nje ya nchi hebu rudi usaidie taifa lako
Ni kweli nilikuwa nje. Nikasoma huko nikarudi na tumawazo twangu tupya. Kazini pale kuna tuzee tumeshikilia usukani na tunaendesha mambo kwa nadharia na fikra za miaka ya 70. Nilikuwa frustrated nikaviacha. Sasa niko mtaani huku naisoma namba. Ukija na mawazo yako mapya halafu ukagusa ulaji wa watu unaweza hata uka-restishwa in peace usipokuwa mwangalifu. Yule daktari bingwa wa moyo na hospitali yake ya moyo alikuja na moto kufungua hospitali ya rufaa yenye uwezo wa kufanya operesheni kubwa kubwa za moyo hapa hapa nchini akishirikiana na madaktari wenzake kutoka Texas. Kumbe anaingilia ulaji wa watu na safari zao za kwenda kutibiwa nje. Unajua kilichompata? Kanchi haka kaone hivi hivi tu mkuu japo mambo yanabadilika pole pole. Tuwe na subira!
 
Daaah
Tuna safari ndefu sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom