Vyuo vimeamua kucheza rafu: TCU iweni makini.

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Kwa mshangao mkubwa nimeona vyuo vikuu vikicheza rafu na kusababisha maumivu makubwa kwa wanafunzi. Nina uhakika na rafu hizo. Kuna jamaa Yangu alikuwa amechaguliwa vyuo vinne, na akaamua kuthibitisha chuo kimoja kilichokuwa cha kwanza kutoa kutoa jina lake. Alithibitisha kwa SMS na online mapema kabisa 07/10/2017.

Cha kushangaza ametokea kwenye orodha ya wanafunzi walioomba tena second round kwenye vyuo vingine viwili! Kati ya vyuo hivi viwili kimoja alikuwa amechaguliwa ile awamu ya kwanza lakini hakuthibitisha. Sasa wamedanganya kuwa aliomba tena chuo hicho second round kwa kozi hiyo hiyo waliyokuwa wamemchagua first round lakini hakuthibitisha! Hata mantiki ya rafu hiyo haina kichwa wala miguu.

Chuo cha pili wanachodai aliomba second round ukweli ni kwamba alikuwa ameomba first round chuo hicho na hawakumchagua katika hiyo first round japo ndiyo chuo alichokuwa anakipenda kwa kozi hiyo. Sasa wameamua kudanganya kuwa aliomba second round na wakamchagua kitu ambacho siyo kweli.

Athari ya rafu hizo kwa mwanafunzi ni kutokupangiwa mapema au kutokupangiwa kabisa mkopo maana inaonekana hatima yake bado haikajulikana hivyo TCU kushindwa kuwasilisha taarifa zake heslb kwa wakati.

Ninawataka TCU wawaagize viongozi wa vyuo hivi wawasilishe ushahidi kuthibitisha madai yao kuwa wanafunzi wameomba tena kudahiliwa kwao baada ya kuwa wamedahiliwa na kuthibitishwa kwenye vyuo vilivyowadahili awamu ya kwanza!

Vinginevyo hasara waliyosababisha jina lichelewe kupelekwa Heslb waifidie wao. Natoa siku tatu baada ya hapo nitátafuta msaada wa kisheria niwapeleke mahakamani!
 
Kwanza haiingii akilini! Haiwezekani MTU ukaomba chuo kwenye second round kwa kozi hiyo hiyo uliyoikosa kwenye first round kwa chuo hicho hicho. Naona walipoona kuwa kuna wengi hawakuthibitisha kwenye chuo chao, wakaamua kuwarudia waliowatosa lakini wakajifanya kuwa wameomba second round! Kilichonikera ni kusababisha jina LA mtoto libaki kwenye sintofahamu TCU hivyo huenda ikawa ndiyo sababu ya mtoto kutokupata mkopo mpaka sasa na anahangaika kweli! Lazima niwashughulikie!
 
Nakuna wengine hawajapata kabisaaa hatari chuo cjui watafanyaje
 
Kuna matatizo mengi sana
Kuna rafiki yangu wamemuweka kweny orodha ..et hajathibitisha chuo chochote wakat alishathibitisha tayar
 
Kwanza haiingii akilini! Haiwezekani MTU ukaomba chuo kwenye second round kwa kozi hiyo hiyo uliyoikosa kwenye first round kwa chuo hicho hicho. Naona walipoona kuwa kuna wengi hawakuthibitisha kwenye chuo chao, wakaamua kuwarudia waliowatosa lakini wakajifanya kuwa wameomba second round! Kilichonikera ni kusababisha jina LA mtoto libaki kwenye sintofahamu TCU hivyo huenda ikawa ndiyo sababu ya mtoto kutokupata mkopo mpaka sasa na anahangaika kweli! Lazima niwashughulikie!
Haya majanga sijui tutayamaliza vipi. Kijana anaambiwa ameomba tena bada ya kuwa approved wakati alisha confirm. Mwingine ana ambiwa hakuconfirm ana mutliple admissions ukweli alikonfirm kitambo halafu wamempachika program ambayo hakuomba (hana vigezo) na waka acha ile aliomba, akapata na ku-konfirm. Hawa wote wawili bado hawajapata mkopo. Sioni watafikiriwa na nani mkopo wa style hii
 
Safi sana kwa kuamua kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani ,mkuu mimi wamenizungusha nimechoka sasa ,naomba tuungane tupeleke madai mahakamani maana kukaa kimya ni kujinyima haki zetu wenyewe haiwezekani tupelekeshwe kiasi hichi ,please tutafutane by Email wisdombaga@gmail.com
 
Asante mkuu tutawasiliana. Haiwezekani watu kucheza na maisha ya watu!
 
MBONA UNAONGEA KAMA MTU MWENYE AMRI ? UMETOA SIKU 3....
Hakuna mubembeleza MTU aliyefanya forgery kusingizia MTU kaomba second round wakati siyo kisha kusababisha madhara kwenye mchakato mzima wa udahili na uombaji wa mkopo!
 
Back
Top Bottom