Vyuo Vikuu vya Tanzania vinazalisha zaidi wahuni kuliko hata wasomi

Ally Nassoro px

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Tafsiri nyepesi ya chuo kikuu ni sehemu inayotoa elimu huru. mwanafunzi anakuwa huru katika masomo yake na usimamizi wake binafsi.

Yaani hapa mwanafunzi anaenda kusoma pasi na usimamizi mkubwa kutoka kwa walimu wake.

Lakini kwa nchi yetu hii elimu ya vyuo vikuu naona kama haipo sawa na inaenda kutuzalishia single mother, wadada wanaojiuza mitandaoni wengi.

Msichana ambae tunamtoa mtaani akiwa na heshima zake akifika chuoni anabadilika mazima. mwanzo tulikuwa na mtoto ambae anajistili anavaa vizuri nguo za maadili lakini akifika chuo anakuwa mtu wengine kabisa.

Na ubaya wa mambo tumeshindwa kujitofautisha kati ya sisi na wazungu. wenzetu wazungu walishatengeneza mfumo wa maisha ambao unaenda kumuandaa mtoto akifikisha miaka 18 atakuwa mutual kwa kujielewa na kujitegemea.

Lakini sisi Afrika mtu akifikisha miaka 18 huyu bado ni mtoto na sio mutual afrika mutual tunaanza kumpata akifikisha miaka 26+ .

Sasa mtu anafika chuo anaenda kuachiwa huru kwa imani kuwa anajielewa . anaenda kupewa condom eti ajikinge hapa huyu mtu aendi kujikinga tunaenda kutengeneza mazingira kuwa ngono aone ni kitu cha kawaida kama kunywa maji tu.

Hatimaye leo hii wanawake wengi wanaojiuza mitandaoni ( Telegram Groups & WhatsApp Groups).

Ni wanafunzi wa chuo leo hii single mother wengi tunawapata kutokea chuo. Sasa kuna mda tunashindwa kuelewa kuwa tunatengeneza wasomi au kizazi cha ovyo ambacho tutakiita wasomi.

Leo hii tuna imani kuwa mtoto wako ili afaulu vizuri zaidi nadhani kila mtu atatamani mtoto wake akae na msomi lakini wasomi wetu ndio hawa ambao wanajiuza mitandaoni.

Leo hii ukitaja chuo kama IFM nadhani kila moja anajua wanafunzi wake wana sifa gani. sasa hili swala alienda kulichafua chuo tu ila linaenda kuwa kubwa mpaka linaenda kuichafua nchi. baada ya miaka 10 baadae.

Kama hakuna mabadiliko yatakayochukuliwa basi sifa ya vyuo vikuu vya Tanzania vitasifika kwa sifa za ovyo.

i. Kuna haja ya kuwa makini na wanafunzi tuuwe huu utaratibu wa kuwaachia hawa wanafunzi huru sana. tuwe kama kile chuo cha kule Zanzibar ( Suza).

ii. Kuna haja ya kuwa na somo maalum la ushauri na saa. ili swala la ushauri tusikichukulie dogo.

Akili ya binadamu ufanya kazi pale inapokumbushwa kumbushwa mfano rais wa nchi yoyote lazima awe na washauri wa raisi.

Kwa sababu ishajulikana kama akili ya binadamu ajakamilika na anaitaji ushauri na kukumbushwa kila baada ya mda.

Leo hii nchi hii ina uhaba wa watoa ushauri.

Tuna namba kubwa ya madkatari na walimu lakini hatuna washauri . Leo hii matatizo mengi yanatokea uwenda ni kwa sababu ya kukosa ushauri tu.

Serikali inaenda kupambana na kufungua Soba houses nyingi ili kupunguza waathirika wa madawa ya kulevya wakati serikali ilitakiwa kwanza kudhibiti kizazi kipya cha watumiaji wa madawa. kwa kupewa ushauri .

Leo hii tuna waarifu wengi na kesi ni zilezile zinazofanana . je kuna mtuhumiwa hata moja aliyewahi kukamatwa na kuulizwa au kushauriwa zaidi yake atapigwa tu basi.

Je, kumpiga mhalifu ndio njia ya kumfanya aache uhalifu ?

Serikali na wizara ya elimu iweke somo la maalum linatakuwa linatoa ushauri kwa wanafunzi japo kwa week mara moja tu wanafunzi asijisahau chuoni kafata nini

iii. Sheria na ugakuzi wa mara kwa mara.

Hapa lazima tuwe wakali tu kama tunataka kutengeneza kizazi ambacho kweli kitatunufaisha baada sheria lazima ziwe kali. kwa wanafunzi wote ambao watafunja sheria za chuo.

Wanafunzi wasipewe uhuru sana kiasia ambacho hata huko makwao hawana uhuru uo mbele ya wazazi wao. lazima awe chini ya usimamizi afrika afrika mtu hata awe na miaka 50 lakini akiitwa wanafunzi / wanachuo basi anaitaji uangalizi tu .

Uwekwe utaratibu maalum wa kuwa kuwakagua wanafunzi afya zao kila baada ya mda fulani. ( vipimo vya ujauzito na magonjwa ya ngono ).

Ili jamii yetu ikuwe na tuendelee basi kwanza lazima tuishi kwenye mfumo wetu halisi wa maisha yetu hatuwezi kucopy mifumo ya maisha ya Marekani na Ulaya alafu tujisifu tumeendelea, tunaenda na wakati .

Hatuwezi kuendelea kwa kucopy mfumo wa watu wa maisha afrika au waswahili mfumo wetu wa maisha hauruhusu watoto wa kike kuvaa nguo fupi kuvaa nguo zinazobana . huku ni kupotea na athari zake ni kubwa tunaenda kuzalisha kizazi kimoja cha ajabu sana huku baadae.

Tukiendelea hivi hivi tujiandae kuona namba kubwa ya single mother , watoto wengi wa mitaani , mateja , mashonga na wauni wengi tu ambae tunaenda kuwapa nchi tukiamini kuwa wameelimika kumbe wamehitimu tu elimu ya juu.

Asanteni .
Nawasilisha.
 
Chuo hakizalishi hizo specimen ulizotaja hapo, hizo specimen zilizotajwa zimezalishwa kwaoooh! Hivyo focus should be directed to the family level where everything beggings.
ni kweli ila % kubwa ili swala linaanzia kwa watu wakiw level ya University . nadhan chin ya level hizi usimamizi wa family unakuwa mkubwa sana ndo maana unaona hata kuconnection videos nying zinzofuja zinawagusa watoto wa chuo.

Sasa tatizo lipo kwa wanachuo wenyewe sio malezi ya family
 
Chuo hakizalishi hizo specimen ulizotaja hapo, hizo specimen zilizotajwa zimezalishwa kwaoooh! Hivyo focus should be directed to the family level where everything beggings.
Chuoni ni miaka mi3 tu kama ni tabia za ovyo basi ttz lilianzia nyumbani
 
ni kweli ila % kubwa ili swala linaanzia kwa watu wakiw level ya University . nadhan chin ya level hizi usimamizi wa family unakuwa mkubwa sana ndo maana unaona hata kuconnection videos nying zinzofuja zinawagusa watoto wa chuo.

Sasa tatizo lipo kwa wanachuo wenyewe sio malezi ya family
Familia inatoa 65% na duniani 35% chuo wanaenda kusoma sio kulelewa na kuangaliwa kama ilivyokuwa secondary na pia kuface uhuru waliokuwa hawana, trust kama 65% ya familia haijatimia utaona mapicha yote.
All in all whoever is a siglemom or drunkard ni YEYE chuo sio sio sehemu ya malezi ni kusoma TU.
My point nguvu iende kwenye family level.
 
Tatizo lilianzia home likakemewa likashuka chini ila baada ya mtoto wetu kwenda chuo na sisi kuamin ni mutual ndio tatizo lilikuwa kubwa.

imagine ukikutwa na condom nyumbani ni kesi ila chuoni condom zinatolewa kwa wingi tena free
Chuoni ni kwamba umeshakuwa mtu mzima
Ukipewa condom haina maana uitumie na hata kama ni kuitumia sio kwa papara mpaka ikupotezee malengo yaliyokupeleka huko
 
Familia inatoa 65% na duniani 35% chuo wanaenda kusoma sio kulelewa na kuangaliwa kama ilivyokuwa secondary na pia kuface uhuru waliokuwa hawana, trust kama 65% ya familia haijatimia utaona mapicha yote.
All in all whoever is a siglemom or drunkard ni YEYE chuo sio sio sehemu ya malezi ni kusoma TU.
My point nguvu iende kwenye family level.
ni kwel tuanzie kweny family level coz hapa ndo kwenye shina ila chuo pia kinachochea mabadiliko kwa wanafunzi hakun sheria inayomkea wanachuo kwa kitu chochote kile.

ngono vyuon linaonekana ni jambo la kawaida tu
 
Chuoni ni kwamba umeshakuwa mtu mzima
Ukipewa condom haina maana uitumie na hata kama ni kuitumia sio kwa papara mpaka ikupotezee malengo yaliyokupeleka huko
Mkuu ukipewa chakula unatakiwa ukifanyaje samahan nimetoka nje ya mada kidogo maana tusitafute jambo baya tukalipa sifa nzuri
 
Chuoni ni miaka mi3 tu kama ni tabia za ovyo basi ttz lilianzia nyumbani
In countries like Lebanon it's not normal Kila mtu anakula kivyake na kwa muda wake nooope familia lazima ikae dinner mom here daddy here brother there, unawaona watoto wako if they have problems they will share with you and it's where family love beggings in case Kuna changes za watoto utaona.
Ndio maana nasisitiza Kila kituo kinaanzia nyumbani.
 
Back
Top Bottom