Vyuo Vikuu Vya Serikali Badilikeni na Kufanya Yafuatayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo Vikuu Vya Serikali Badilikeni na Kufanya Yafuatayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Feb 24, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni ukweli usipingika kuwa asilimia 100 ya uendeshaji vyuo vikuu vya Serikali inatokana na fedha toka Serikalini kuu. Kwa hali ilivyo sasa na huko tuendako hii ni hali ya hatari na inayofaa kufanyiwa kazi mapema ili katika kipindi cha miaka 10 mpaka 15 ijayo vyuo vyetu vikuu vya Serikali viwe na uwezo wa kujitegemea kwa angalau asilimia 60 kama sio 100.

  Ili lengo hili litimie inapendekezwa vyuo vya Serikali vifanye yafuatayo

  1. Vyuo vyote vikuu vya Serikali vianzishe Mifuko ya Akiba na Uwekezaji. Lengo liwe ni kwa kila Mwanachuo husika na aliyepitia katika chuo hicho awe anawekeza angalau shilingi 5,000 kila wiki katika Mfuko wa Akiba na Uwekezaji wa chuo chake.

  2. Vyuo vyote vya Serikali viombe maeneo makubwa hapa nchini yaliyo na madini na gasi na kuyamiliki na kisha kuanzisha uchimba wake.

  3. Vyuo vikuu vya Serikali vianzishe ukulima wa Mashamba Makubwa ya Miti ya Aina mbalimbali za Mbao. Lengo la chuo kimoja liwe ni kupanda angalau Ekari 150,000 za miti ya mbao kila mwaka kwa miaka 15 mfululizo. Iwapo uwekezaji huu katika mashamba makubwa ya miti ya mbao utafanyika, baada ya miaka 10 mpaka 12, kwa bei za sasa, chuo kikuu husika kitakuwa na ukakika wa kupata faida isiyopungua shilingi bilioni 3,900 kila mwaka kutoka katika mashamba yake ya miti ya mbao pekee. Kiwango hiki cha fedha kinaweza kuendesha Chuo kama Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa Zaidi ya Miaka 300 au Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 30.
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  wazo zuri .
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapa barani africa ni who to trust with your contribution of money?
   
 4. w

  warea JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakifanya hivyo wajasiria mali watafanya kazi gani?
  Nani atagundua maarifa mapya uzalishaji? Tunataka tuendelee kutumia vizuri rasli mali zetu kuzalisha kwa tija.
  Hii ndio kazi yao.
  Tunataka tuongozwe kwa kanuni bora, tutibiwe kwa njia sahihi na bora, tujenge nchi kwa mbinu bora zaidi.

  Badala ya kuwatoa wasomi kwenye maabara na madarasani wakafanye hizo kazi, afadhali tuwachukue wamachinga woote tuwape hiyo ardhi na vitendea kazi wakapande miti na kuzalisha. Sio kuchuuza mali za wakwepa kodi.

  Serikali nao wasimamie suala la nishati ya umeme ili wale jamaa wa mkaa wasiendelee kukata miti watakayopanda waungwana.
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mkuu si kweli kua public universities zote zinaitegemea serikali kwa 100%. Ingekua ivyo shughuli na majukumu yasingetimizwa kwa 100% na vyuo hivyo. Kwani pesa toka serikali ni ndogo sana na mara nyingi hutumika kwa kulipia mishahara.

  Vyuo vikuu kama UDSM na SUA vina vyanzo vingine vya pesa hususani kutokana na shughuli za research and consultancy. Shughuli izi zinaviingizia vyuo mapato makubwa. Pia vyuo ivyo hupata pesa kutokana na grants na aids kutoka kwa wajomba (marafiki wa maendeleo).
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Utekelezaji wake ni mgumu ssana, wengine hiyo pesa wanatumia siku tano
   
 7. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Aise hapo vitakua vyuo au makapuni ya biashara? Ni kama useme muhimbili ili kujitegemea wafungue shamba la mizabibu waanze kutengeneza wine
   
 8. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wala simaanishi hivyo. Vyuo vyetu imefikia hatua vipunguze sana utegemezi toka Serikalini na kwa Wafadhili. Tunakokwenda si kuzuri hata kidogo. Ni muhimu sana Vyuo Vyetu na wahitimu wake wakatuongoza katika namna bora ya kutumia rasilimali za nchi yetu badala ya kuwaachia wageni toka nje.
   
 9. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sawa mkuu. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa vyuo vyetu vikuu ni tegemezi mno. Naomba uangalie Facts and Figures za vyuo vyetu ndiyo utaona ukweli wa kile ninachokisema na umuhimu na mantiki ya mapendekezo niliyoyatoa.
   
Loading...