Vyuo vikuu vina mpango gani kuziba mapengo yanayoachwa na wahadhiri waandamizi wanaofariki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu vina mpango gani kuziba mapengo yanayoachwa na wahadhiri waandamizi wanaofariki?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, Apr 21, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Salaam wanaJF!

  Katika siku za hivi karibuni tasnia ya elimu ya juu imekua ikikumbwa na majonzi ya mara kwa mara kutokana na kuondokewa na wahadhiri waandamizi na waliobobea katika fani zao.

  Nawakumbuka marehemu Profesa Mwaikusa, Dr. Ndibalema, Dr. Katunzi, Dr. Shechambo na Profesa Mjema. Hawa ni baadhi tu ya waliofariki hivi karibuni.
  Mungu awarehemu na kuzidi kuwapumzisha mahala pema peponi. Amina

  kutokana na vifo hivyo, nilidhani vyuo vikuu vingekuja na mipango mikakati na madhubuti katika kuweza kuweka njia za mapengo hayo kuzibwa (pengine ndani ya miaka 5 hadi 10 ijayo) lakini cha ajabu, sijaona wala kusikia mipango yoyote ile.

  Na kwavile katika tasnia ya elimu ya juu, mentor-ship ni jambo la lazima na muhimu sana kuwepo ili wahadhiri chipukizi waweze kupata misingi na miongozo ya kuja kua wahadhiri bora na waliobobea katika nyanja zao; mipango mikakati kwa vyuo vikuu kwakweli inahitajika haraka sana. La sivyo baada ya miaka 10 kutakua na wahadhiri waandamizi katika vyuo vikuu wasio na mwelekeo wowote na wasio na misingi na miongozo bora ya uhadhiri.

  Lazima vyuo vikuu vyote viweke mikakati ya kuwatumia ipaswavyo wahadhiri waandamizi walio hai, ili wahadhiri hao waweze kuwa mentor wahadhiri chipukizi katika kusimamia maandiko na kazi zao; katika kuwashirikisha kwenye miradi mbalimbali (kushirikisha hapa namaanisha kushirikishwa tangu mwanzo wa mchakato wa kuandaa miradi, na si kushirikishwa katika kwenda kujaza madodoso tu, kwani kwa namna iyo kutakua hakuna effective mentorship).

  Kwa namna hiyo, baada ya miaka 5-10 kwa kiwango fulani pengo la wahadhiri waandamizi wanaofariki litapunguzwa.

  Nawasilisha.

  Wasalaam,

  Nyanda.
   
 2. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unajua hili lilikuwa ni tatizo la serikali ya jamhuri ya muungano ya Tanzania. Ila kwa sasa naweza kusema succession plan katika level ya wahadhiri waandamizi linafanyiwa kazi kwa kasi nzuri. Nitajaribu kufafanua katika phase 2.
  1. Mara baada ya uhuru na early 2000s, serikali haikuwa na mpango wa kusomesha wahadhiri katika level ya PhD, hivyo wahadhiri walitegemea scholarship, na kwa sababu haikuwa rahisi kupata basi ni vyuo vichache vyenye kuweza kupata hizo scholarship ziliweza kusomesha watu wake kiurahisi, mfano SUA, na vyuo vingine ilitegemea sana pia qualification za mhadhiri, maana pia kulikuwa na utofauti, mfano UDSM ilihitajika uwe na PhD ili ufanye vitu fulani ndani ya chuo, lakini vyuo vingine mfano IFM wao ni masters tu ilihitajika ili uwe na uwezo wa kufanya vitu hivyo hivyo vya PhD holder wa mlimani, hivyo hali hiyo ilipelekea wahadhiri wengi wa vyuo kutokuona umuhimu wa PhD. Na pia PhD haikuwa gateway to money success, maana vyuo kama Mzumbe wao waliweza kuwa consultant wazuri tu katika level ya master na mfano CPA, hiyo pia ilimaanisha kwao hakuna umuhimu wa PhD.
  2. Late 2000s serikali kupitia loan board na kwa kushirikiana na wafadhili ilisisitiza sana umuhimu wa PhD, mfano German+TZ gov, Denrmark+TZgov, Netherland+TZ Gov, etc, hivyo katikati na hapa mwisho wa 2000s wahadhiri wengi sana wameenda kusoma hizo PhD, nadhani by 2015 kutakuwa na wahadhili waandamizi wa kutosha.

  Jambo lingine lililokuwa linakwamisha wahadhiri (PhD) holder kutoka Dr kuwa ma professor, ni ukiritimba wa walio na uprofessor kuwatunuku hawa walio chini, kwani suala la mikataba likuwa linachangia kwa kiasi kikubwa kwa walio juu kutokuona umuhimu wa kuwepo ma professor wengi, na hivyo kuweka vigezo vingi vigumu ili kuweza kuingia wachache katika ulimwengu wa ma professor, maana ilikuwa professor akistaafu basi anapatiwa mkataba, na kama pangekuwa na professor basi angeweza kukosa mkataba hivyo kwa upande mwingine huyo anayetakiwa kuwafanya wengine wawe ma professor anaweza kuwa mgumu ili kuja kulinda mkataba wake baada ya kustaafu, ndiyo maana serikali inalifanyia kazi hili suala ili kuondoa suala la mikataba kwa hawa maprofessor ili wafahamu wanajukumu la kuhakikisha wana kuwa na succession plan ya kazi zao.
   
Loading...