DENLSON
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 944
- 1,253
Digrii za heshima (Doctorate of Honour) zimekuwa zikitolewa na vyuo mbali mbali ndani na nje ya nchi yetu kwa lengo la kutambua mchango wa mtu mmoja mmoja katika jamii kwa jambo fulani.
Mara nyingi kama sio zote hapa kwetu Tanzania digrii hizi zimekuwa zikitolewa kwa wanasiasa na wafanyabishara kitu ambacho kinaondoa hadhi, uhalisia na maana nzima ya hizo heshima zinazotolewa kwa watu husika katika jamii.
Kwa mfano, Rais Magufuli kwa kutambua mchango wa mhandisi Mzee Mfugale alimua kuipa Flyover ya tazara jina lake. Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa tuwape watu wanaochangia maendeleo kwenye jamii zetu heshima ili kizazi cha leo na kesho kijue kuhusu wao na kijifunze kupitia wao.
Waswahili wanasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, leo 1/1/2020 ni vyema mwaka huu uwe wa tofauti kwa maana digrii hizi za heshima wapewe na watu wenye mchango mkubwa wa maendeleo kwenye jamii yetu; Kwa namna ya kipekee kabisa nitaje watu wachache ambao wanastahili tuzo za heshima kwa michango yao katika jamii kwa sekta mbali mbali
Ruge Mutahaba R.I.P
Jasiri mtengeneza njia, naam Ruge alikuwa nguzo ya mafanikio kwa sanaa ya mziki wa Tanzania. Alikuwa mbunifu mwenye kugundua vipaji na kuvisapoti. Leo hii mamia ya wasanii wamepita kwenye mikono yake. Ametengeneza ajira kwa namna ambayo haiwezi kutajwa. Leo kuna Wasafi Festival kwa sababu Fiesta ipo. Ubunifu wake na uwezo wake wa kuona kipaji na kukiendeleza vinamfanya kuwa mtu wa kipekee sana katika nchi yetu.
Ze comedy Group (Orijino Komedi)
Hawa wanastahili tuzo ya heshima, walianza vipindi vya komedi kipindi ambacho jamii haitambui sana sanaa ya vichekesho, kifupi vichekesho havikuwa ajira. Wakaiendeleza na kuifanya ipendwe leo hii sanaa ya vichekesho ni ajira kubwa Tanzania.
Joseph Mbilinyi (Mr Sugu)
Moja kati ya watu wa kwanza kuimba nyimbo za kufoka kwa kiswahili. Sugu nastahili tuzo sio tu kwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya muziki wa kizazi kipya bali hata kwa kuonesha njia kwa vijana kufanya mziki na kuikuza sanaa ya Tanzania.
Mr Blue (The game changer)
Ndio ni Mr. Blue ambae alikuja kuubadlisha mziki wa Tanzania toka rap au kofoka mpaka kuingia kwenye mziki laini ambao leo ndio uliobeba mafanikio ya wasanii wengi kama sio wote. Huyu anastahili tuzo ya heshima amewatoa vijana wengi kupitia aina ya muziki aliokuwa akiimba wengi wamezoea kuuita wabana pua.
Msaga Sumu
Leo mtaani kuna aina mpya ya mziki unaitwa singeli huyu jamaa ndio mwanzilishi wa huo mziki. Kwanini asipewe tuzo ya heshima? Kupitia yeye na aina yake ya muziki leo watu wengi wanaimba na kupata fedha kupitia mziki wa singeli.
Nasibu Abdul (Diamond)
Naam ni Diamond mtoto wa Tandale ambaye kupitia yeye Afrika na dunia leo inaimba mziki wa Tanzania. Diamond amebadili mziki wa Tanzania kutoka ubishoo na umaarufu kuwa biashara kubwa. Amepanua mawazo ya wasanii wengi kuhusu uwekezaji nje ya muziki leo wasanii wengi wameanza kuwekeza katika biashara tofauti na muziki. Haya ni mafanikio makubwa na yanastahili pongezi.
Steven Kanumba R.I.P
Wanasema pengo lake halizibiki kwenye sanaa ya maigizo. Ni kweli Kanumba ni moja kati ya watu waliofanya sanaa ya maigizo ianze kupata soko ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Kumpa tuzo ya heshima Kanumba kunataibua hamasa ya kupata warithi wake katika tasnia ya maigizo nchini.
Wako wengi sana kuna waandishi wa habari, waandishi wa vitabu, wanamichezo, wanasiasa, wanasheria, wakulima, wazazi, watumishi, wanajesi, maaskari, walimu, madaktari na wengine wengi unaweza kuongezea majina yao ili kuheshimu michango ya watanzania wenzetu katika sekta zote Biashara, uchumi, kilimo, ufugaji na utumishi pia.