WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,415
- 1,379
Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania
ambavyo vilishiriki katika
mashindano ya mjadala wa Afrika
kuhusu Sheria za kimataifa za haki
za kibinaadamu yalioandaliwa na
kamati ya kimataifa ya shirika la
msalaba mwekundu ICRC
vimeshindwa kufika katika raundi
ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa
katika raundi za mapema ambapo
mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama
hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa
mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen
nchini Tanzania, vyuo
vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo
cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka
Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo
kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya
mashindano hayo yaliofanyika
mwishoni mwa wiki katika
mahakama maalum ya kimataifa
inayochunguza mauaji ya kimbari
nchini Rwanda ICTR mjini
Arusha,chuo cha Strathmore
University kutoka Kenya kiliibuka
mshindi na kufuatiwa na chuo cha
Christian University kutoka Uganda
huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka
Zimbabwe kikiibuka mshindi wa
spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo
ilisimamiwa na jaji wa mahakama
hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama
kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji
wa mahakama ya haki katika Afrika
mashariki Fanstin Ntezilyayo,John
Joseph Wamwara na Mutsa mangezi
kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi
kwa washindi aliyapongeza
mashindano hayo kama kifaa cha
kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo
vikuu wanaofanya sheria na kwamba
itasaidia kuimarisha maono yao
katika siku za usoni.
Source:BBC
ambavyo vilishiriki katika
mashindano ya mjadala wa Afrika
kuhusu Sheria za kimataifa za haki
za kibinaadamu yalioandaliwa na
kamati ya kimataifa ya shirika la
msalaba mwekundu ICRC
vimeshindwa kufika katika raundi
ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa
katika raundi za mapema ambapo
mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama
hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa
mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen
nchini Tanzania, vyuo
vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo
cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka
Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo
kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya
mashindano hayo yaliofanyika
mwishoni mwa wiki katika
mahakama maalum ya kimataifa
inayochunguza mauaji ya kimbari
nchini Rwanda ICTR mjini
Arusha,chuo cha Strathmore
University kutoka Kenya kiliibuka
mshindi na kufuatiwa na chuo cha
Christian University kutoka Uganda
huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka
Zimbabwe kikiibuka mshindi wa
spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo
ilisimamiwa na jaji wa mahakama
hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama
kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji
wa mahakama ya haki katika Afrika
mashariki Fanstin Ntezilyayo,John
Joseph Wamwara na Mutsa mangezi
kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi
kwa washindi aliyapongeza
mashindano hayo kama kifaa cha
kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo
vikuu wanaofanya sheria na kwamba
itasaidia kuimarisha maono yao
katika siku za usoni.
Source:BBC