Vyuo vikuu na siasa mbovu za tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu na siasa mbovu za tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hittler, Jul 18, 2011.

 1. h

  hittler Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini duniani,moja ya maadui watatu wakuu aliowasema baba wa Taifa mwl Julius Nyerere. Maadui wengine ni Maradhi na ujinga. Ili kujikwamua kwenye umaskini elimu ni nguzo au msingi itakayopelekea kuondoa ujinga, kuzidisha kujiamini na kutoa suluhu ya jinsi gani mtu anaweza kupambana na maradhi. Tanzania ilionekana kulitambua hilo ilipoamua kuanzisha taasisi za elimu kama shule za awali, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na vyuo vikuu.
  Inasikitisha sana kuona wanasiasa wanageuza vyuo vikuu majukwaa ya siasa na wengine kudiriki ata kuwachukua wanafunzi ili wawasaidie kwenye uchaguzi. Hili linafanyika kwa vyama karibia vyote. Ni jambo la ajabu na lakusikitisha sana kwa sababu wanafunzi wanaacha kufanya na kufuata yaliyompeleka chuo badala yake ana nadi sera za vyama. Mbaya zaidi muda wao wa kukaa chuo ukiisha wanasiasa huwasahau na kutafuta wanafunzi wengine bila kujua kwamba wamewatumia kwa maslai yao binafsi na wengi wao hawana performance ya kuridhisha.
  Tufike mahali sasa tukemee tabia hii, wanafunzi waachwe wasome muda wao ukifika wataingia kwenye siasa mbona hao wameanza siasa ukubwani?
   
Loading...