ijoz
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 731
- 709
Ni ajabu kwa vyombo vyetu vya hapa nchini vinavyokosea kuandika lugha adhimu ya kiswahili.
Baada ya Mechi kati ya Simba na Kagera Sugar, Azam Two kwenye yale maandishi wameandika Chersea 3 ( badala ya Chelsea), MPILA (badala ya mpira) unaendelea.
Channel Ten jana tarehe 14/10 (nadhani kwenye kipindi cha Baragumu Live), wakaandika Miaka 17 BIRA Baba wa Taifa (Badala ya kuandika Bila).
Ingekuwa kiingereza tungejitetea kuwa ni lugha ngeni, lakini hata kiswahili!!! Kama vyombo ambavyo naamini vina wataalamu wa lugha, na wahariri wa vyombo vya habari kuandika makosa kama hayo, sishangai kuona watu wanaandika lugha za ajabu ajabu wakiita kiswahili, pengine wanavyotazama vyombo vya habari wanaamini kinachoandikwa ni sahihi.
Tukosee mengine, lakini hata kiswahili tuendelee kukosea????