Vyombo vya utangazaji viache kuajiri watangazaji vilaza; wanafukuza wateja

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Cheap labor is always expensive. Hivi vituo vya utangazaji vinavyookota watangazaji mitaani bila kujali viwango na uwezo wao, vinakera sana. Unaajiri mtu asiyejua hata kusoma wa kutamka maneno ya kawaida kabisa, bila shaka ni kwa bei ngogo lakini hasara kwa mwenye kituo.

Nimesikia watangazaji wengi wakiwemo RFA, hadi nafikia kiasi cha kufunga station kwa sababu ya maudhi ya watangazaji. Huko ni kukimbiza wateja.

Utakuta hata radioni wamekusanyika kujadili mada bila utaalamu na bila hata kufanya utafiti. Wanaongea pumba kiasi kwamba hata uzito wa mada unapotea. Tatizo ni nini?

Mfano angalia hii you tube mtu anayesema 'ZARI ZE BOSS LEDI" TENA KWA KURUDIA RUDIA NA HALAFU ANAJILAMBA MIDOMO KWA SAUTI, bila kujua anakera na kufukuza wateja.

Huyu jamaa anakera kweli kweli!
 
Wakati umefika mamlaka zinazohusika zisimamie ajira za hawa WATANGAZAJI.Nasema hivyo kutokana na utangazaji wao umekuwa usio na Maadili, Mzaha , Utani na Udhalilishaji.Mkiamka asubuhi mnashangaa hata Zembelwa au Mpoki ni WATANGAZAJI mnajiuliza alienda Chuo lini? Jibu hajaenda sasa IWEJE atangaze?
 
Hivi kuna tofauti gani kati ya mtangazaji na mwandishi wa habari?
Nahisi labda mtu yoyote anaweza kuwa mtangazaji na hili siyo hapa Tanzania tu hata mbele utakuta mwanamziki au mwigizaji anatangaza au kuhost show flani ya tv lakini si mwandishi wa habari...
 
Wakati umefika mamlaka zinazohusika zisimamie ajira za hawa WATANGAZAJI.Nasema hivyo kutokana na utangazaji wao umekuwa usio na Maadili, Mzaha , Utani na Udhalilishaji.Mkiamka asubuhi mnashangaa hata Zembelwa au Mpoki ni WATANGAZAJI mnajiuliza alienda Chuo lini? Jibu hajaenda sasa IWEJE atangaze?
Zembwela huwa ananikera sana akitangaza, ana utani mwingi, hayupo serious halafu anapenda kurudi rudi jambo au neno lisilo na msingi wowote.
Huwa nachukia hadi na change station
 
Kuna mtangazaji mmoja kule Arusha Triple A anaitwa Masai yaani ukisikia anajadili au anaendesha kipindi na mwenzie yeye ni kudandia mazungumzo ya mwenzie ili aongee yeye tu anakera sana hadi unahamisha station hampi mwenzie nafasi nae aongee anajiona ndio oxygen ya Triple A ! Aache ushamba wa masifa tu
 
Wakati umefika mamlaka zinazohusika zisimamie ajira za hawa WATANGAZAJI.Nasema hivyo kutokana na utangazaji wao umekuwa usio na Maadili, Mzaha , Utani na Udhalilishaji.Mkiamka asubuhi mnashangaa hata Zembelwa au Mpoki ni WATANGAZAJI mnajiuliza alienda Chuo lini? Jibu hajaenda sasa IWEJE atangaze?

Mkuu, ni majanga!.
 
Watangazaji wengi Vilaza.

Utakuta wengine wanajifanya wachambuzi. Wachambuzi juu ya jambo wasilokuwa na ufahamu nalo. Wanajadiliana utadhani wanawake wanasuka nywele saluni ama vijana wako kijiweni wakipoteza muda bila kitu cha maana. Hii ni nini? Vyombo vya habari viko kuhabarisha watu, kuelimisha, ku empower, kuburudisha, n.k . Huwezi kupata kitu chochote cha kujenga kwa vyombo vyenye watu vilaza.

Kwa kweli ni maudhi sana na fedheha kwa taifa. Tuwaombe serikali wadhibiti viwango vya vyombo hivi ili kuhakikisha ubora unazingatiwa.

Wanakudhi kweli kweli.
 
mleta mada uko safi sana. Watangazi wa tz wengi ni kero sana
Sahara media wamezidi aisee, pamekuwa kama uwanja wa kujifuzia kazi. Na wakishapata uzoefu wa kutosha tu huwaoni tena.
 
Kabisa mkuu kuna hawa channel ten hasa hasa kipindi cha asubuhi cha habari na magazeti yani unakuta mtangazi anatafuta neno la kusoma km ndio anaanza kujifunza kusoma
 
Wakati umefika mamlaka zinazohusika zisimamie ajira za hawa WATANGAZAJI.Nasema hivyo kutokana na utangazaji wao umekuwa usio na Maadili, Mzaha , Utani na Udhalilishaji.Mkiamka asubuhi mnashangaa hata Zembelwa au Mpoki ni WATANGAZAJI mnajiuliza alienda Chuo lini? Jibu hajaenda sasa IWEJE atangaze?
Kwa sheria ipi? huko Bungeni mnakowalipa mamilioni mbona vilaza ni wengi tena wengine na piechidi zao!
 
Redio na tv nyingi sasa zimekuwa za mipasho tena ya kizaramo. Hakuna nidhamu kabisaaaaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom