Tetesi: Vyombo vya Usalama vilivyojipanga kumpokea Tundu Lissu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Tundu Lissu ameripotiwa kuwa ameaga rasmi huko Ubelgiji na ataunganisha ndege jijini Dubai kabla ya kutua JNIA.

Maofisa wa Uhamiaji pamoja na wale wa Usalama (wapya) waliopo JNIA wapo wanaendelea na shughuli zao.

Kuna mawili matatu hivi kutoka kwa maofisa Uhamiaji na Usalama.

1. Mgeni huyu (Tundu Lissu anatumia pasi ipi ya kusafiria)

Hivyo utaratibu wa kumpokea Tundu Lissu waweza kuchukua muda mrefu.

Kitakachopatikana kwenye mahojiano ndicho kitakachoelekeza hatua zitakazofuata.

2. Angalia madhumuni ya safari na sababu za kurudi.

3. Afisa uhamiaji kuridhika na majibu kulingana na sheria ya uhamiaji na kama kuna "ya ziada"

4. Idhinisha kuingia kwa kugonga muhuri wa kuingia au toa muda maalum ikiwa ni pasi ya kigeni.

5. Kama ni Tundu Lissu zuia "self check- in" na muongoze chumba cha mahojiano.

Hizi ni za hapa na pale.

JNIA imebadilika sana kuna watu wapya na wengi mno ambao wanahakikisha usalama wa uwanja, udhibiti wa kitokacho na kiingiacho na mazagazaga mengine.

Kuna kijana wa Nigeria alishindwa kueleza kwa ufasaha amepataje pasi ya kusafiria ya kitanzania ilhali hafahamu lugha ya kiswahili.

Wakamchukua kuingia kwenye vyumba vyao maalum kwa mahojiano maalum.

Msinitupie mawe mazee haya nimeyapata na mengine kuyaona hapo JNIA nilipotua mchana leo.
 
Onyo
34F78A75-048B-416A-BEE6-00AAE991BCE5.jpeg

6E0B3B0A-5EF0-4FB0-9E2B-6B427E1108C5.jpeg
 
Pa kuanzia ni je, huko Kenya na baadae Ubelgiji, alipelekwa au alienda kwa pasi gani? kama ni ya Tanzania na alikuwa na medical visa katika nchi hizo- Kenya na Ubelgiji, sioni taabu ya kwanini azuiliwe kuingia ili hali hiyo pass ya Tanzania imetolewa na serikali yetu wenyewe na hakuna maelezo yeyote kusema kwamba either ime-expire au kufutwa/ cancelled.

Sioni sababu yoyote ya kumzuia isipokuwa kama ni kum-detain aende kujibu kesi zake za kisutu... ni mu huru bado hadi hapo kesi zake zitakapo tolewa maamuzi...
 
This is silly for you! Umetia kinyaa na ukongwe wako humu lakini kichwani u mtupu kama kenge.

Hakuna sababu yoyote ile inayomzuia raia yeyote halali wa nchi yake kurejea kwao.

Uhamiaji wanaweza kuzuia kutoka bali si kurudi kwenu kajifunze hayo we mbayuwayu!!
 
Sijui ni kwanini Siku zote Mbwa hupenda sana Kujipeleka kwa Nyoka aina ya Chatu ili akamezwe na Kuuwawa nae hata kama ukijitahidi Kumzuia.

Yaani amekuja wakati mbaya sana. Namuhurumia sana TL

Naona kwenye barua yao hata jina hawataki kumtaja ila nawaomba CDM tu watumie busara akapokelewe na familia yake aende zake kwake tukutane kwenye kampeni
Na kama akikamatwa taarifa zitajulikana tu ila sio waende wakajazane pale halafu Polis watapata upenyo wa kufanya watakvyo
 
Sijui ni kwanini Siku zote Mbwa hupenda sana Kujipeleka kwa Nyoka aina ya Chatu ili akamezwe na Kuuwawa nae hata kama ukijitahidi Kumzuia.
Jibu ni rahisi tu ndugu yangu, ni kwa nini yesu aliwazuia wafuasi wake wasizuie kukamatwa kwake pale maaskari walipokuja na Yuda kumkamata? Ukijua hilo basi, yatosha kutokuendelea kuuliza hilo swali tangu asubuhi...Lissu ndiye pekee anayeweza kujibu hilo swali au ni mbwa pekee anayejua kwanini anamsogelea Kujipeleka kwa Nyoka aina ya Chatu ili akamezwe na Kuuwawa nae hata kama ukijitahidi Kumzuia...majibu mengine yote yasiyotoka kwa wahusika wenyewe yatakuwa either in hearsay au speculations...
 
This is silly for you! Umetia kinyaa na ukongwe wako humu lakini kichwani u mtupu kama kenge.

Hakuna sababu yoyote ile inayomzuia raia yeyote halali wa nchi yake kurejea kwao.

Uhamiaji wanaweza kuzuia kutoka bali si kurudi kwenu kajifunze hayo we mbayuwayu!!

Usidharaua ukongwe wangu.

Kuna mawili matatu ya kuokota.
 
Sitashangaa hili likitokea
Kwa roho mbaya zilizotawala nchi yetu naingiwa na woga
Maswali na Majibu mnayo toka ile siku pale Dodoma
Mumhoji nini
Lissu alipashwa kuwahoji ninyi
Anarudi kwao hata kama Hana Travel Document Anarudi Nyumbani
Kwani nini mbaya ninyi polisisiem kha??!
 
Back
Top Bottom