Vyombo vya Usalama vichunguze tuhuma za Uhalifu wa Mo Dewji na Genge lake kudukua mawasiliano ya watu/wafanyakazi wake

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
"Mohammed akamuita askari, ambaye sijui ni mlinzi wake Mungu anajua sitaki nimuingize katika mtihani.Akamuambia tuonyeshe Hajji namna gani anahujumu.Yule bwana akatoa simu yake akawa anaonyesha limeandikwa jina langu pale Saa tatu usiku ulisomeka mnara wa posta, saa tano ulisomeka mnara wa Vijibweni. Wakati huo saa tano mnara wa vijibweni mimi nimelala na Nahida.Akili ikanambia ngoja niangalie Tarehe. Nimeshika simu nikawaambia mbona hii tarehe saba?.Wakanipora ile Simu,.(Mazungumzo yanaendelea). Nikawaambia sikuwa Temeke pia, Mohammed akachachamaa. Halafu nikaona na namba nyinginenyingine pale za watu wa Simbasimba pale wote nao wanafuatiliwa."

"Lakini nikamuuliza Mohammed Wewe ni nani?, Ni polisi?, Ni Cybercrime?, Ni kitengo cha usalama, Jeshini au Polisi?, Rights za kwapekua..kudukua mitandao ya watu unaipata wap?.Nani kakupa Authority hiyo?, kwa sababu una pesa?.. Nilichachamaa nikamwabia unadhuumu watu kwa pesa zako. Umepata wapi haki za kunidukua mimi?Unawezaje kufanya hivyo kumpeleleza mtu..(Mazungumzo).. lakini hata kama nilionekana Posta hiyo siku Ninyi nani kawapa rights hizo?..Sasa yule afande pale akastuka, maana..sijui na sio mimi tu. Wanawadukua wengi, mi nimeona simu nyingi pale,Serikali naomba Inilindemaanake mimi Lofa nisije nikatoka hapa yakanikuta ya kunikuta... Haki za kumdukua mtu nani katoa?" - Hajji Manara Aliyekuwa Afisa Habari wa klabu ya Simba

Sitaki kuunga mkono kitendo cha Haji Manara kuusema hadharani uongozi wake uliopita kwa tuhuma kadhaa. Nimesikiliza press yote ya Hajji lakini kuna vitu vimenipa attention kidogo na mimi kama mwanabodi nimeona nishee na wenzangu. Nafahamu wakuu wetu wapo wanaosoma mijadala na kuna wakati wanaijibu ama kuifanyia kazi kimya kimya.

Sitaki kudeal na Manara, Babra wala Mo as a person wala ishu ya uwekezaji lakini nataka kujaribu kudeal na content ya facts alizozisema Manara kwani hoja hujbiwa kwa hoja. Moja ya kitu ambacho Manara amekisema ni Kudukuliwa kwa mawasiliano yake na kufuatiliwa nyendo zake yeye na wafanyakazi wenzie. Amesema hili limekuwa likifanywa na Mo "Mohammed Dewji" akisaidiwa na liyemuita "askari" japo hana uhakika ambaye inaonekana ndo analeta ushahidi ama vielelezo hivyo kwa Mo kutokana na ushawishi wa pesa za Mo. Manara ameenda mbali mpaka kuomba serikali ijaribu kumlinda kwa hilo kwani hana fedha la kudeal na hilo. Lakini ametumaanishia kuwa si yeye tu bali kuna wengine pia hawako salama katika hilo.



Nikijazia hapa, Huu ni uhalifu sababu Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 16 na pia Sheria ya 1984Na.15 ib.6 zinatambua Haki ya faragha na usalama wa mtu.
NimeQuote:
"16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi. (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii."

Sote tunafahamu kuwa mawasiliano binafsi na faragha za mtu zinaweza kuingiliwa kwa utaratibu maalum wa kisheria. Sina uhakika lakini kwa Maneno ya Manara sidhani kama Mo na watu wake walifuata sheria na taratibu zilizowekwa. Hili jambo ni hatari sana kwa usalama wa nchi na watu wake.

Kama Manara amelalamika, nadhani Alarm imekuwa raised. Ni jambo linalogusa Umma na linaweza kuwa jinai. Ni wakati wa Mamlaka husika kumchukua Manara kwa Mahojiano na pia kuchunguza tuhuma zake hizi dhidi yaMo. Ili kama ni kweli ijulikane
:-
-Ni nani huko CyberCrime au Mamlaka nyinginezo zinamsaidia Mo,
-Huyo afande mwenye Simu inayoonesha wanaodukuliwa ni nani?
-Kwa faida gani
-Na kwa utumishi gani wamfanyie yeye kazi.
-Ama ni kama wanahack, Ni kina nani hao
-Wameshahack watu wangapi hapa nchini
-Nani anawafadhili?
Nadhani watakuwa ni watu muhimu kuisaidia dola kupata taarifa mbalimbali zaudukuzi zilizokuwa pending huko nyuma pia.

Na kama si kweli basi Mo asafishwe kwa hilo na Manara awajibike kwa Defamation atakayokuwa ameifanya ikiwemo hofu kwa wafanyakazi wengine. Ukitaka kujua Seriousness ya hizi tuhuma Jaribu kujiuliza Mo ana wafanyakazi wangapi jumla. Mo anadeal na watu wangapi katika Biasahara. Mo ana ukaribu na anadeal na viongozi wetu wangapi hapa nchini?

Kazi na iendelee!

 
Babara mtu mpole kimuonekano ila ndani fisi wa hatari...ni hatari kwa afya yako...kuna video moja nilimuona anampamba sana Mo,now ndo napata majibu
 
Inawezakuwa kweli au porojo tu kisa wamempiga chini

Aalipomtaja Senzo na Diamond . Niliona si Porojo. ana connection ya kutosha kwenye Uzi wake.

Hans Pope alisema ni mkataba wa 4M , Hajji kasema ni 3M.. Hans aje akanushe sasa!

Kigwangala alisema Mo hajatia hela na anazungusha. Kaduguda akiwa kiongozi wa simba alijibu hela tayari na Mo hakusema kama ni kweli au si kweli.

We huoni nani wa kutiliwa mashaka?
 
Waswahili tuna shida wengi hatujui nini maana ya kudukua?! Kudukua ni kusikiliza mawasiliano ya watu wengine au kuingilia mawasiliano ya watu wengine na kuyasikiliza kwa minajili yeyote ile ya kujinufaisha au kujifurahisha.
Ila swala la kujua mtu yuko wapi?! Ni swala la kawaida mno kwa teknolojia ya sasa,simu zetu zina access na app ambazo unaweza kujua mtu anaekupigia au unaempigia yuko wapi ni suala la kawaida sana.
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
Tupo ukwel ndugu
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
Tupo ukwel ndugu
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
Tupo ukwel ndugu
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
Tupo ukwel ndugu
 
MANARA apigwe, afukuzwe, auawe, atolewe kafara atajua yeye na familia yake..... Siye twataka makombe tu,,,, MO weka hela baba nunua akina Banda wengine tuendelea kupiga makombe....... MANARA anapigania MASLAHI yake hana jipya, ndo binadamu tulivyo,,, angekuwa anaipenda sana SIMBA basi tokea kipindi hicho angeongea..
 
Jamaa kumbe weak hivyo, aisee!! Mwanaume ukitimuliwa na wenyewe unakomaa kimya kimya unaangalia mambo mengine.

Maskini hawezi kuwagombanisha matajiri never ever...wanakusanifu tu. GSM, MO na Bakhresa hawawezi kugombana na haka ka clip.
 
Back
Top Bottom