Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Tunakumbuka Trump alipoingia madarakani alivikandia vyombo vya usalama USA kutia ndani CIA na FBI mara nyingine hata akaunga mkono mawazo toka Urusi dhidi ya CIA.
Sasa wameamua kumwonyesha huwezi kutukana wakunga na uzazi ungalipo. Trump kaanza kuonja joto ya jiwe kwa vyombo hivi ambapo wanavujisha habari za siri za ikulu kwa vyombo vya habari. Hii ni pamoja na skendo ya hivi karibuni ya mshauri wake wa mambo ya usalama kuongea na balozi wa Urusi kumtoa hofu Urusi kuondolewa vikwazo vya uchumi vilivyowekwa na Obama. Gazeti ka Washington Post lilivujishiwa habari hizi za siri ambazo inaonekana Trump alitaka kutozichukulia hatua.
Safari ya Trump white house inaonekana itakuwa ngumu sana. Israel sasa wanalalamika habari za siri toka White House zinavuja sana!