Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wote wa Mikoa wakabidhi mchango wa msikiti wa Chamwino

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,592
Vyombo vya ulinzi na usalama vikiwakilishwa na mkuu wa Majeshi General Mabeyo na wakuu wa mikoa wakiwakilishwa na RC Ndikilo wa Pwani wamekabidhi mchango wao wa ujenzi wa msikiti kwa shehe wa wilaya ya Chamwino shehe Matitu.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wamechangia jumla ya sh 30 milioni.

Wakuu wa mikoa wamechanga jumla ya sh 26 millioni na hadi sasa jumla ya michango imefikia sh milioni 142 tangu ilipoanza kuchangishwa.

Nalo Kanisa la AIC mkoani Simiyu limechangia ujenzi huo wa msikiti sh milioni 2 ambazo zimekabidhiwa kwa shehe Matitu na RC Mtaka kwa niaba ya muinjilisti wa Kanisa hilo.

Chanzo: Star tv habari!
 
Jaman narudia na naomba watu tusigombanishwe Na hizi dini za mapokezi tena tulizoletewa na watesi wetu (wazungu Na waarabu). Kanisa kuchangia ujenzi wa msikiti sioni tatizo, kwani mkristu akiugua akalazwa muislam hawezi kwenda kumuona hospital au vice versa. Tuwe waungwana kwenye maswali ya kijamii, dini zituweke karibu kuliko kutugawa.

Tena ndugu zetu waislam ndio hupenda kusema tunamwabudu Mungu mmoja, sasa kusaidiana kujenga nyumba za ibada kuna shida. Usiwe na imani kuliko msahafu au biblia, ndipo utaanza kufuata mafundisho ya wanadamu wenye personal interests/agenda za kutugawa.
 
Jaman narudia na naomba watu tusigombanishwe Na hizi dini za mapokezi tena tulizoletewa na watesi wetu (wazungu Na waarabu). Kanisa kuchangia ujenzi wa msikiti sioni tatizo, kwani mkristu akiugua akalazwa muislam hawezi kwenda kumuona hospital au vice versa...

Hivi unaamini bado watu tumelala hatujui motive behind ya huo mchango? Tulishaamka zamani sana boss, hapa tulipo tunawachora tu.
 
Jaman narudia na naomba watu tusigombanishwe Na hizi dini za mapokezi tena tulizoletewa na watesi wetu (wazungu Na waarabu). Kanisa kuchangia ujenzi wa msikiti sioni tatizo, kwani mkristu akiugua akalazwa muislam hawezi kwenda kumuona hospital au vice versa...
Baada ya Jiwe kuvurunda ndio umekuja na vimaelezo vya ujanja ujanja kujustify upuuzi uchangishe mchango wa msikiti kanisani we ndio frustration zenu hazijaisha tu.
 
Jiwe huwa akiona hali imekuwa ngumu kwake hukimbilia ngao ya Jeshi au dini!

Hapo anataka makundi mengine ya waislamu yenye kupinga ujenzi wa msikiti huo kupitia sadaka za kanisani yakae kimya kwa heshima/kuhofu jeshi.

But honestly, hakuna muislamu wa kweli anayeogopa jeshi linapokuja suala la kulinda sanctity ya imani yake, si vizuri kudrag majeshi kwenye kiki za kisiasa!

Staili anayojaribu kutumia ili kuwafunga mdomo wanaopinga sadaka za kanisani kujenga kanisa ni staili ile ile iliyotumika kuondoa mjadala wa kivuko cha Dar Bagamoyo kwa kukipeleka jeshini.

Mbona hatukuona hayo majeshi yakichangia ujenzi wa kanisa la chamwino?

Mbona hatukuona wanakwenda msikitini ili kuchangia ujenzi wa kanisa?
 
Vyombo vya ulinzi na usalama vikiwakilishwa na mkuu wa majeshi General Mabeyo na wakuu wa mikoa wakiwakilishwa na RC Ndikilo wa Pwani wamekabidhi mchango wao wa ujenzi wa msikiti kwa shehe wa wilaya ya Chamwino shehe Matitu...
Bakwata ilianzishwa na Nyerere akisaidiana na Paulo Bomani , hakuna Muislam hata mmoja aliyeshiriki

Nakala : Mohamed Said
1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
Kitendo alichofanya Rais Magufuli kuitumia madhabahu kuchangisha fedha za msikiti kinaonesha uwezo wake mdogo wa uelewa wa Biblia na Ukristo kwa ujumla wake. Mkristo halisi hawezi kufanya upumbavu wa aina hii. Imani kuu ya Ukristo ni imani kwamba Yesu Kristo alikufa na kufufuka kisha kupaa mbinguni.

Imani hii ndiyo central divine ya christianity na kwayo mtu huokoka na dhambi ya ulimwengu anayepingana nayo ama asiyeiamini sehemu yake ni motoni. Hii ni kwa mujibu wa Biblia. Sasa Uislam hauamini ikiwa Yesu Kristo aliuliwa, akafufuka na kisha kupaa mbinguni na ndivyo unavyofundisha. Imani hii kinadhani ya uislam ni kumpinga Kristo. Sasa mtu anayechangisha fedha ili auendeleze uislam maana yake anasaidia kazi ya kumpinga Kristo. Sasa sijui ikiwa huyu bwana mkubwa analielewa hilo.

Mimi nawapenda waislam kwa dhati ya moyo wangu ila imani yao siyo imani yangu hivyo sintowadhulu nitawapenda daima na kuishi nao ila siyo kwa kiwango cha kuwasaidia kueneza dini yao.
 
Hii nchi imekuwa kama nchi za vishoka wa North Korea, Cuba, Venezuela etc. Wao uchumi na maendeleo hapana, just power consolidation. Next -------- Uchumi kuanguka na kuanza kula ugali wa muhogo na mchele wa msaada ulijaa mchanga kama miaka ile------
 
Back
Top Bottom