Vyombo vya Ulinzi na Usalama kila siku vinalilia ajira mpya, navyo vipewe sasa

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,548
6,102
Nimeshuhudia jeshi la Magereza likiomba ajira mpya sio chini ya mara mbili kipindi cha Mwendazake lakini halikupewa hata mmoja na badala yake kuambiwa watumie wafungwa kwa hiyo wafungwa wapewe bunduki wajilinde wenyewe?

Polisi leo nao sio mara ya kwanza kuwasikia wakiomba ajira mpya na kupigwa danadana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama hivyo hivyo tatizo nini hapa?

Najiuliza yule Rais wa awamu ya nne yeye aliwezaje kutoa ajira mpya huko majeshini takribani kila mwaka mpaka kufikia wale vijana wetu wa Jeshi la Kujenga Taifa kule makambini kwao kuanza kuchagua ajira za Jeshi lipi waende?

Leo kila siku kukicha vijana wetu kutoka Jeshi la Kujenga Taifa wanarudishwa mtaani kwa kisingizio cha Jeshi la Kujenga Taifa haiajiri mbona kipindi cha Kikwete hii lugha ya Jeshi Kujenga Taifa haiajiri haikuwepo kabisa?

Kuna aja gani ya kujaza vijana wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa mtaani ilihali kila kukicha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinalilia vipewe ajira mpya?

Kwako Mama Samia Suluhu Habari
 
Kamwamu

Au tuseme kila idara katika dola; tuondoe neno serikalini maana bungeni ni mhimili unaojitegemea
 
Back
Top Bottom