Vyombo vya Ujasusi vyamshtukia Trump!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,803
13,034
Sasa inaonekana dhahiri, hali si shwari kati ya vyombo vya Usalama na Ujasusi chini Marekani na Donald Trump.

Jana viongozi karibu wote wa vyombo vya usalama na Ujasusi, yaani National Security Agency, CIA,FBI, Homeland Defence,walionyesha kukerwa na rais mteule Trump kwa kauli zake za kuviponda vyombo hivyo kuhusiana na uchaguzi wa rais, kuingiliwa na udukuzi wa kielektroniki na Urusi.

Waliyasema hayo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Senate, nchini Marekani, jana asubuhi tarh 5 Jan.

Wawakilishi wa karibu vyama vyote, yaani Reoublican na Democrats, wameonyesha vile vile kutoridhishwa na kauli ya Trump kuviiponda vyombo hivyo.

Mjumbe mmoja alienda mbali na kusema Trump anatoa maneno ya kejeli pasipo ulazima huo akitoa mfano wa kiongozi wa Korea Kaskazini aliyesema makombora yake yanaweza fika Marekani.
Trump alidukuliwa akisema, hilo halitofanyika.
Mjumbe huyo alisema hajui msingi wa jibu la Trump, maana vyombo hivi vya kijasusi ndio vinaweza kusema tishio hilo ni la kweli au la.

Mategemeo ni Trump kuomba radhi.

Haya sasa, Trump anaiponda fimbo ya kupigia nyoka!
 
Kwani mpaka warusi wanadukua hao homeland security walikuwa wapi?

FBI walikuwa wanafanya nini?

Au CIA ndio iliwafungulia backdoor wadukuzi??
 
Mwsho wa cku tutaona hio vta ya trump Na majasusi wake mshnd atakua nan
 
nkumene, post: 19184718, member: 338682"]Mwsho wa cku tutaona hio vta ya trump Na majasusi wake mshnd atakua nan[/QUOTE]
Umeambiwa wanashindana?
Donald anavipasha vyombo vyake kama kuvitahadhalisha isijetokea tena jambo la kipuuzi litakaloigarimu nchi na serikali yake.
 
Joe Biden anesema sasa hivi kuwa Trump is "mindless" kwa kuipuuza Intelligence Community.
 
Siyo rahisi mkuu, kwa wenzetu kuvifumua vyombo hivyo ambavyo viko independent operationally ni kazi kubwa.

Ni rahisi sana!
Kama Raisi Trump atakubaliana na Baraza la Senet hakuna kinachoshindikana. Kwanza atateua Watu wake! Pili watamletea tathimini- baada ya hapo Seneti itaarifiwa na kupewa nafasi ya kujadili kwa masilahi ya USA.Wenzetu cha kwanza USA kwa 100yrs ijayo kama mpango unakidhi haja hiyo hapatakuwa na mkwamo.
 
Not so easy mkuu.
Fuatilia kuanzia sakata la uhasama wa John Fitzgerald Kennedy na vyombo vya Usalama , hususan FBI, na mabaya yaliyomkuta.
Msuguano kama wa Trumbp na Obama vle vile uliwahi kuwepo kai ya rumana aliyekuwa na maliza muda wake na Eisehower , rais aliyekuwa anaingia ambaye hakutaka National Security Briefings toka kwa mtanguizi wake.
 
Kwa enzi zile yes. Dunia ya sasa michezo kama ile inaweza kusambaratisha USA! Unajua kuna state ngapi ndani ya USA.
 
Kwani mpaka warusi wanadukua hao homeland security walikuwa wapi?

FBI walikuwa wanafanya nini?

Au CIA ndio iliwafungulia backdoor wadukuzi??

Hapo ndipo jeuri ya TRUMP ilipo.Inawezekana ameona system ya usalama ya marekani iko weak kwenye utawala wake labda atatumia security system ya kirusi kwa rafiki yake putin.

Inawezekana Trump alikuwa recruit wa russia kwa miaka nenda rudi akiandaliwa kuwa raisi wa marekani.Utajiri alionao waweza kuwa sio wake ni mali za warusi yeye ni agent tu na mshika mali za akina Putin na matajiri wa kirusi na shirika lao la ujasusi ndio maana anawang`onga wanausalama wa marekani
 
Kwa enzi zile yes. Dunia ya sasa michezo kama ile inaweza kusambaratisha USA! Unajua kuna state ngapi ndani ya USA.
Mkuu hao jamaa ni leaders of the underworld.
Tofauti kati ya majasusi na majambazi ni ndogo sana.
Alipouwawa JF Kennedy chunguzi zote ziliainisha uhusiano kati ya FBI na The Mob.
The Mob wanachukua contracts za kufanya kazu chafu zisizo weza kuchunguzwa.
 
Hapo ndipo jeuri ya TRUMP ilipo.Inawezekana ameona system ya usalama ya marekani iko weak kwenye utawala wake labda atatumia security system ya kirusi kwa rafiki yake putin.

Inawezekana Trump alikuwa recruit wa russia kwa miaka nenda rudi akiandaliwa kuwa raisi wa marekani.Utajiri alionao waweza kuwa sio wake ni mali za warusi yeye ni agent tu na mshika mali za akina Putin na matajiri wa kirusi na shirika lao la ujasusi ndio maana anawang`onga wanausalama wa marekani
Utajiri wa trump ameachiwa na baba yake mzazi jaribu ata kugoogle uone jamani wabongo kusoma hamtaki mnataka mtunge vitu vyenu kishilawadu tu
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom