Vyombo vya habari vyapigwa marufuku matangazo ya waganga wa kienyeji

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
VYOMBO vya habari vimepigwa marufuku kurusha matangazo yanayohusiana na biashara ya waganga wa kienyeji wakiwemo na wanajimu.

Yameazimiwa hayo katika mkutano uliowakutanisha wadau wa vyombo hivyo kujadili na kuboresha rasimu ya kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010 (EPOCA) walipokutana Dar es Salaam jana .


Akifafanua hayo Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habib Gunze, alisema ni hatari kwa Taifa vyombo vya habari kuhamasisha tiba zinazotolewa na waganga wa kienyeji na masuala ya utabiri wa nyota.

Alisema vipindi na matangazo ya waganga wa kienyeji na watabiri yasiruhusiwe kwenye vyombo vya utangazaji nchini kwani ni hatari kwa jamii hiyo.

Alifafanua kuwa watakaoweza kuruhusiwa ni kama kuna mtaalamu wa miti shamba ambaye anaweza na kuthibitishwa anaweza kutibu ndio apewe kipindi maalum kuzungumzia hilo

Amesema kuruhusu matangazo ya waganga wa kienyeji kwenye vyombo hivyo vinaleta madhara kwenye jamii na kutolea mfano wa tiba ya babu wa samunge na kueleza vyombo vya habari vilichangia na kuna baadhi ya watu wamedhurika na tiba hiyo na wengine kutomaliza matatizo yao japo na kupata tiba hiyo

Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya Mwaka 2010 (EPOCA) ilipitishwa na Bunge Januari mwaka jana na kufuta sheria mbili: Sheria ya Utangazaji namba 6 ya Mwaka 1993 na Sheria ya Mawasiliano Tanzania namba 18 ya mwaka 1993.

Chanzo: Vyombo vya habari vyapigwa marufuku matangazo ya waganga wa kienyeji

B
ADALA WATU NA VYOMBO VYA HABARI KUSHUGHULIKA NA MAMBO YA UFISADI VYOMBO VYA HABARI VINAHUSIKA KUPIGA MARUFUKU UTABIRI NA MAMBO YA UGANGA WA KIENYEJI KWELI TANZANIA KUNA SERIKALI !!!!!! KAZI IPO BONGO YETU
 
Back
Top Bottom