Uchaguzi 2020 Vyombo vya Habari vya Tanzania vimeshindwa kuandika na kuripoti pingamizi, badala yake wameripoti matokeo ya pingamizi

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Media zetu zina kazi kubwa sana safari hii, wakati mapingamizi yaliyowekwa na wakasomewa content na context ya hayo mapingamizi walirekodi na wakawa wanafurahi jinsi hoja zilivyopangwa

Baada ya kurekodi na kuandika, hakuna chombo chochote kilichoripoti Kama habari kubwa kuwa Lipumba na Mzee wamewekewa pingamizi, vilikaa na habari zao kwenye flash hivyo walaji wa habari zao hawakujua kama Kuna mapingamizi.

Baadaye jioni au usiku Mkurugenzi wa uchaguzi akatoka majibu ya pingamizi, wakaenda kumsikiliza na kuandika alichowaambia Ni matokeo. Kwa amasa kubwa wakapost na kuripoti kwa nguvu zote ushindi waliopata waliowekewa pingamizi ngazi ya Urais.

Bila kujua madhara ya dhuluma, wakajikuta wamelazimika kuwahabarisha wananchi kuwa Tundu Lisu aliweka pingamizi ...na Sasa wananchi wakajua nini kinachoendelea. Lakini pia wakawahabarisha wananchi kuhusu mapingamizi hayo ila tu hawajawahabarisha msingi wa mapingamizi kwa sababu tume haijaweka wazi msingi wa mapingamizi na haijaeleza vifungu vilivyoelezwa kuvunjwa au kukiukwa na mweka mapingamizi.

Kwa aina hii ya vyombo vya habari, kwa aina hii ya waandishi na kwa aina hii ya wamiliki na wahariri...wanadhani wanayo haja kweli ya kwenda na flash na makamera yao kwa wagombea wa upinzani? Kwa Nini wasikae hizo gharama za mafuta na uendeshaji wakafanyia kazi nyingine?

Kitu ambacho kinaendelea na ambacho kimesambaa kwa kasi, Ni clip ya Tundu Lisu inayosambazwa na maasimu wa ccm bila kusambazwa clip yoyote ya hoja kinzani Jambo linalowafanya watu waamini kwa 100% aliyosema Tundu lisu Ni ya kweli kwa msingi wa kisheria.

Kitendo cha media kuacha kurusha hizi habari kinawanyima pia haki yakwenda kuomba ufafanuzi kwa wasomi wengine maana ili uweke mdahalo kuhusu hoja za Lisu lazima pia urushe kile alichokisema hasa tumekuwa tunamjenga kwa kasi kubwa na habari zake kusambaa kwa kasi kubwa kuliko zinavyosambaa habari za hao wengine.

Kwa mtu anayewaza kimkakati akipewa kazi ya kushauri kuhusu huu utaratibu ATAWAAMBIA MNACHOFANYA NI NIKUMPA POPULARITY LISU na kuwaminya wengine wasisikike kwa wanannchi
 
Nchi imekuwa kama choo. Mtu mmoja tu anafikiri kwa niaba ya watu milioni 60. Tuko kwenye udikteta kabisa. Nawashangaa TBC wanaripoti kutupwa kwa pingamizi na NEC ambalo hawakuripoti wakati linawekwa! Tuko kwenye ushenzi mkubwa. Na hii inaonyesha kuwa mabadiliko yatakuja kwa nguvu ya umma tu.
 
Magazeti yanaogopa kufungiwa hakuna uhuru wa habari tena cyprian Musiba kazi yake ni kuchunguza vyombo vya habari vinavyoandika ukweli dhidi ya wapinzani kisha kwenda kuvichongea kwa mtukufu malaika tokea chato anayeishi chamwino sasa.
 
Back
Top Bottom