Vyombo vya Habari vitakavyoshirikiana na Mh Paul Makonda vitachukuliwa hatua gani na waliotoa Tamko?

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Kama baadhi ya vyombo vya Habari vitakwenda kinyume na matamko ya Nevile Meena Jana vitachukuliwa hatua gani iwapo watatoa taarifa za Paul Makonda?

Sijajua Tamko hilo kuhusu vyombo vya Serikali na chama ambacho Paul Makonda ni mwanachama wao nao wamelipokeaje Tamko hili.

Nasubiri kuona huo utekelezaji wa Tamko kitu nachokiona ni kigumu na inaweza ikawa na mgongano ndani ya vyombo vingine kimsimamo.

Sasa hivi Paul Makonda ni fursa kubwa ktk sekta ya Habari Tanzania kwa mambo mengi mazuri anayoyafanya kwa wana Dar es salaam.

Ila ukiondoa Yale ambayo ni madhaifu kwake kitu ambacho mwanadamu yoyote yule anacho!!

Hakuna mkamilifu hata mmoja chini ya jua
 
Kitakachotokea watakuwa hawamualiki kwasababu kutakuwa hakuna coverage Ila tbc hawana jinsi nadhani
 
Uhuru wa waandishi wa habari uko wapi? Hizi ni KIKI tu!!! Jina la Makonda linauza magazeti mjini hapa.
 
Uhuru wa waandishi wa habari uko wapi? Hizi ni KIKI tu!!! Jina la Makonda linauza magazeti mjini hapa.
May be huo ndiyo Uhuru wa waandishi wa Habari kupangiwa cha kufanya na vyama vya uandishi na uhariri pia.

Napenda sana nione hilo Tamko lililotangazwa na Neville Meena linatekelezwa ndiyo nitajua umoja wa wana habari.

Kesho sitarajii kabisa kuona,kusoma au kusikia jina la Paul Makonda kwa Tamko la Neville Meena
 
Vyombo hivyo ni hivi hapa, 1.TBC 2.HABARI LEO 3. MZALENDO. 4.UHURU. Hebu ongezea vingine unavyo vijua.
 
Back
Top Bottom