Vyombo vya habari visipotoshe wapiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyombo vya habari visipotoshe wapiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Divele Dikalame, Sep 25, 2010.

 1. D

  Divele Dikalame Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NAWATENDAJI WAO WAACHE KUWAPOTOSHA WAPIGA KURA KWA AJILI YA MASLAHI BINAFSI

  Na. Juma Killaghai
  Kiasi cha miaka kumi na tano iliyopita niliwahi kuona filamu moja inayoitwa 'THE PANAMA DECEPTION', yaani 'UDANGANYIFU WA PANAMA', kwa tafsiri isiyo rasmi.

  Filamu hii haikuwa ya kuigiza; ilikuwa ni muunganisho wa picha mbalimbali za televisheni zilizopigwa wakati wa operesheni ya uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Panama, mnamo tarehe 20 Desemba 1989.

  Uvamizi huo uliohusisha kiasi cha askari 27,000 wa Kimarekani waliosindikizwa na kundi kubwa la Helikopta za kivita aina ya Apache AH-64 ilipewa jina la ' OPERATION JUST CAUSE'.

  Jina hili lilimaanisha kuwa uvamizi huo ulikuwa ni 'KWA AJILI YA KUTETEA HAKI' ya wananchi wa Panama, ambao kwa mujibu wa maelezo ya rais wa Marekani wa wakati huo, George W. Bush Sr., 'waliokuwa chini ya ukandamizaji mbaya sana wa Dikteta Manuel Noriega'.

  Katika filamu hiyo yanaonekana matukio mengi ya kinyama na ya kutisha. Wanajeshi wa Kimarekani waliuwa raia wengi na kufanya uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto kwa makusudi makazi ya watu wa kawaida kwenye vitongoji vingi vya jiji la Panama.

  Kitongoji cha El Chorillo hadi leo kinaitwa 'Hiroshima ndogo' kwa jina la utani kutokana na ukweli kwamba makazi yote ya wananchi katika uvamizi huo yalichomwa moto na wakaazi wengi wa eneo hilo kupoteza maisha.

  Ufukuaji wa maeneo mengi ya makaburi ya pamoja uliofanywa baada ya kukamilika kwa operesheni hiyo ulionesha kuwa watu wengi waliozikwa katika makaburi hayo walikuwa ni wahanga wa mauaji ya makusudi. Mabaki ya maiti nyingi yalionyesha kuwa waliozikwa humo hawakuwa wapiganaji.

  Maiti nyingi zikiwemo za watoto wengi wadogo wenye umri chini ya miaka mitano zilionyesha kuwa wahanga hao waliuwawa kwa kupigwa risasi kichogoni na huku wakiwa wamefungwa mikono kwa nyuma kwa kutumia nyaya za chuma!
  Jambo la kushangaza ni kwamba vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya, ikiwa ni pamoja na TV na magazeti, vilichagua kwa makusudi kutotangaza kwa uhalisia kile kilichokuwa kinaendelea nchini Panama.

  Taarifa zilizoletwa na waandishi wa vyombo hivyo waliokuwa nchini Panama wakati wa tukio 'zilikaliwa' na mahala pake kukarushwa na kuandikwa habari zilizokuwa zinahalalisha uvamizi huo wa majeshi ya Marekani. Mfano wa habari hizo ni ile iliyotangazwa na televisheni za Marekani kwa mapana na marefu zikimnukuu rais Bush:

  '….and now freedom and democracy have been restored in Panama….', yaani '…na sasa uhuru na democrasia vimerejeshwa Panama….'.

  Bush alitoa kauli hii akilihutubia Taifa lake kufuatia mafanikio ya majeshi yake katika kulisambaratisha jeshi dogo la Panama lililokuwa na askari wasiozidi 3,000, kumkamata aliyekuwa rais wa nchi hiyo Manuel Noriega, na kumsimika kibaraka wao, Guillermo Endara, kama rais mpya.

  Filamu ya 'The Panama Deception' ilibuniwa na wale waandishi ambao taarifa zao halisi walizotuma kwenye vyombo vyao vya habari zilikaliwa, ikiwa ni jitihada zao za kujaribu kuufikisha ukweli kwa ulimwengu.

  Kazi kibwa ya vyombo vya habari ni kuhabarisha. Katika kufanya kazi hii chombo cha habari kinatakiwa kifanye kila jitihada kuhakikisha kuwa habari kinazotangaza ni kama zilivyotokea. Wadau wa vyombo vya habari, hususan watendaji wake na wamiliki wa vyombo hivyo wanapaswa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa imani na hisia zao binafsi haziwi ni sehemu ya habari inayotakiwa kufikishwa.

  Kwa bahati mbaya sana hali halisi haiko hivyo. Wamiliki wengi wa vyombo vya habari duniani kote wameanzisha vyombo hivyo kama zana za kufinyangia akili za watu kwa nia ya kupelekea mbele agenda zao binafsi ambazo zimejificha katika nyoyo zao. Kwa bahati mbaya zaidi ni kwamba hata pale ambapo wamiliki wa vyombo husika wamenusurika na kusudio hilo, ni mara chache sana kwa wale waliokabidhiwa kuviendesha, yaani wahariri na waandishi, kunusurika.

  Mfano tulioutanguliza hapo juu wa filamu ya 'The Panama Deception' ni moja tu ya vielelezo vya hali hii. Ulaya na Marekani ni maeneo ya dunia ambayo watawala wake tangu karne na karne wanaamini kuwa wazungu wametukuka kuliko watu wengine wote na kwa maana hiyo wana haki ya kuwatawala, kuwaibia na kuwafanyia ubaya wowote kwa ajili ya maslahi yao na nchi zao; na iwapo hili litashindikana kwa njia ya udanganyifu, basi litawezeshwa kwa matumizi ya nguvu za kijeshi.

  Hii pia ndiyo falsafa inayofuatwa na vyombo vya habari vya mataifa hayo. Anayetaka kubisha kwamba hivi sivyo na tumuulize: Hivi ni kwa nini Waafrika kila mara wanalalamika kwamba vyombo vya habari vya nchi za Ulaya na Marekani vinaandika, kutangaza na kuonesha habari mbaya tu kuhusu Afrika?

  Kwa bahati mbaya sana Waafrika wengi, wakiwemo na Watanzania pia, tunaingia katika mkumbo wa kuvipa sifa mbaya vyombo vya habari vya nchi za Ulaya na Marekani, bila kufanya uchunguzi wa kina wa mwenendo wa vyombo vyetu wenyewe vya habari. Mwenendo wa vyombo vya habari vya hapa nchini Tanzania, bila kujali kama ni vya umma au ni vya binafsi, ni mfano halisi wa vyombo vinavyotumiwa vibaya kwa ajili ya kuendeleza agenda binafsi za wamiliki au watendaji wake.

  Kwa Tanzania, agenda hizi zimejikita zaidi katika maslahi ya kidini na kisiasa. Kwa mfano, wakati rais mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi, akiwa madarakani kila alipotajwa na vyombo hivi, bila kujali kwamba habari hiyo ilikuwa inahusu nini ilikuwa ni aghalabu kusikia:

  '….ambaye ni Muislamu…'.

  Ni kweli Bakili Muluzi alikuwa ni Muislamu, lakini uislamu wake ulikuwa unahusikaje na suala lililokuwa linaelezewa na habari hiyo?

  Mbona vyombo hivyo hivyo vilipokuwa vikimtaja, kwa mfano Fredrick Chiluba, rais mstaafu wa Zambia, hatukuwa tukisikia kiambatisho:
  '….ambaye ni mkristo mlokole….'?

  Wala hatukuwahi kusikia wakina Chisano, Dos Santos, nakadhalika wakitajwa na huku wakiambatanishiwa na imani zao za dini?!

  Kuna mifano mingi mno inayodhihirisha ni kiasi gani vyombo vyetu vya habari vinahangaika kutumika kama chombo cha kubebea maslahi ya ukristo dhidi ya yale ya uislamu na imani nyingine zilizopo kwenye Taifa hili. Hili lisingekuwa ni tatizo kubwa sana, kama jitihada hizi zingekuwa hazigusi ulingo wa siasa. Kwa bahati mbaya sana siasa inatumika kama ndiyo mbeleko ya kuyabebea hayo maslahi.

  Kwa mfano: Japokuwa kuna ushahidi mwingi sana na wa wazi unaoonyesha kuwa serikali ya CCM, na kabla ya hapo ile ya TANU, imekuwa ikitumika sana kusimamia na kuendeleza maslahi ya ukristo dhidi ya yale ya dini nyingine, vyombo vyetu vya habari vimechagua kukaa kimya.

  Hata hivyo vyombo hivi ni hodari sana wa kupiga kelele zinazohusu 'udini' pale kunapokuwa na tukio au jambo lolote linaloashiria kuwa uislamu au Waislamu watanufaika. Hakuna hata haja ya kutoa mifano kwa sababu ni mingi mno, na iko wazi kabisa.

  Wakati tukiwa kwenye mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba ya mwaka huu 2010, hali hii ya mwenendo mbovu wa vyombo vyetu vya habari imeendelea kujitokeza na safari hii, kwa wale tunaojua 'kusoma katikati ya mistari', bila hata kificho.

  Kwa kuzingatia matokeo ya chaguzi za nyuma, matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2009, na kuenea kwa mtandao wa chama kitaifa, kampeni hizi zinaonekana kutawaliwa na vyama vitatu vya CCM, CUF na CHADEMA. Tayari vyombo vingi vya habari kupitia maudhui ya taarifa wanazotoa, picha na hata mpangilio wa taarifa hizo, wameshawaamulia wapiga kura kuwa ni mgombea gani wa nafasi ya urais na kutoka chama gani anatakiwa ashinde!

  Kati ya wagombea watatu wa nafasi ya urais waliosimamishwa na vyama hivi uchambuzi wa taarifa za vyombo vya habari unaonesha wazi kuwa kuna hekaheka nyingi na za kila siku za kumtukuza na kumpamba mgombea wa CHADEMA, Dr. Wilbroad Slaa; huku pia kukiwa na juhudi kubwa za kufukia madhaifu yake na ya chama chake. Jitihada hizo pia zimejikita katika kutilia mkazo udhaifu wa wagombea wenzake na kufukia sifa zao.

  Ni vigumu kusema kwa uhakika Dr. Slaa ana sifa gani zinazompelekea apigiwe debe kiasi hicho na vyombo vya habari. Yote anayoyazungumza hivi sasa kuhusu KATIBA, ELIMU, AFYA, MAKAAZI, KUDHIBITI MATUMIZI YA UMMA, KUWA NA SERIKALI NDOGO nakadhalika, na kuonekana kuwa ndiyo yaliyobeba kampeni yake na ya chama chake wala siyo 'original'. Sehemu kubwa ya hayo ameigiza kutoka katika ilani za CUF za mwaka 2000 na mwaka 2005.
  Kwa bahati nzuri CUF mwaka 2005 waliichapisha ilani yao yote katika mfumo wa gazeti na kuisambaza nchi nzima. Wale wote waliobahatika kuhifadhi nakala za ilani ile wanaweza wakaipitia tena kujiridhisha kuwa haya ninayoyasema siizushii CHADEMA. Naamini kuwa vyombo vya habari jambo hili wanalitambua japokuwa hawataki kusema ukweli. Aidha, huwezi ukahalalisha 'promosheni' hii ya vyombo vya habari kwa kisingizio kuwa CHADEMA ni chama makini!

  Hivi unawezeje kukiita makini chama ambacho kinaweka mgombea mwenza mwenye elimu ya darasa la saba? Hivi ikitokea bahati mbaya rais akafariki kabla ya kumaliza muda wake, kweli sisi kama Taifa tuko tayari kumkabidhi uongozi mtu wa elimu ya darasa la saba ili atufikishe tunakotaka kwenda?

  Ni chama gani makini ambacho leo kinataja majina ya mafisadi kwa kinywa kipana lakini siku chache baadaye viongozi wake waandamizi wanapigana vikumbo mahakamani kutaka kuwawekea dhamana baadhi ya 'hao mafisadi' kwa kisingizio kuwa ni ndugu zao?

  Ni chama gani makini ambacho katika uzinduzi wa kampeni zake kinamruhusu mmoja wa makada wake waandamizi asimame hadharani na kushutumu jinsi kulivyokosekana dhamira ya kisiasa ya kuwatia hatiani waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi lakini wakati huohuo baadhi ya watuhumiwa hao ni wateja wake anaowatetea huko mahakani?!

  Ni chama gani makini ambacho kinaanza kuomba kura kabla ya kampeni kuzinduliwa rasmi huku kikijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya uchaguzi na inaweza kupelekea wagombea wake wazuiliwe kushiriki uchaguzi?

  Dr. Slaa wakati wa kutafuta wadhamini wa kumdhamini kuwa mgombea alikuwa anaomba kura za wafanyakazi alizodai Kikwete kazikataa! Mpaka sasa bado nimepigwa na bumbuwazi kuwa ni vipi CCM haikujaribu kulitumia tukio hilo kumwekea pingamizi. Au kuna kamchezo?

  Sitashangaa sana iwapo CCM na CHADEMA lao ni moja katika kile kinachoendelea. Tusisahau pia kuwa mwanzoni mwa mwezi wa Julai, 2010, kada maarufu wa CCM mzee Mustapha Sabodo alitangaza kuwa anaichangia CHADEMA shilingi 100,000,000.00.

  Kwa wale wanaoijua vizuri CCM, kitendo cha kulikalia kimya tukio hilo ni cha kutia mashaka makubwa! Wengi wetu tunajua kuwa vyama vingi vya upinzanzani ni dhaifu sana kiraslimali kutokana na watu wenye uwezo kuogopa kuvisaidia ili wasije wakalipiziwa kisasi na CCM. Wengi wetu tunajua pia kuwa wachache wanaojaribu kufanya hivyo hufanya kwa siri kubwa!

  Lakini labda kubwa kuliko yote linalosababisha 'promosheni' ya vyombo vya habari kwa Dr. Slaa iwe ni yenye kutia sana shaka ni taarifa kwamba Dkt Slaa amekilazimisha chama chake kuingia naye mkataba kuwa ili agombee ni lazima kimlipe shilingi 12,000,000.00 kwa mwezi kwa muda wa miaka mitano iwapo hatafanikiwa kushinda nafasi ya urais.

  Kiasi hiki cha fedha ni wastani wa asilimia kumi na mbili (12%) ya ruzuku ya chama hicho ya kila mwezi kwa kiwango cha sasa! Kama taarifa hizi ni za kweli, na uwezekano mkubwa ni kuwa ni za kweli kwa sababu tangu zimechapishwa CHADEMA haijazikanusha, basi Dkt. Slaa pamoja na viongozi wenzake waandamizi katika chama chao au hawajui wanachokifanya, au wana unafiki unaotisha! Hivi si huyu huyu Dr. Slaa na viongozi wenzake ambao wamekuwa wakiwaambia Watanzania kuwa mishahara ya wabunge ati ni mikubwa mno na wanataka ipunguzwe? Pamoja na ukweli huu bado wana-habari mnataka mtu wa aina hii awe kweli ndiye rais wetu?

  Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 niligombea ubunge katika jimbo la Mwanga kwa tiketi ya CUF. Katika vitu vilivyonishangaza sana ni mgombea mwezangu wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, kuacha kufanya kampeni za kujinadi na kukinadi chama chake; na badala yake akaunganisha nguvu na mgombea wa CCM, Profesa Jumanne Maghembe, kuhangaika kuipaka CUF matope. Mgombea huyo, Bwana Nathanael Mlaki, alipewa shehena kubwa ya vivuli (photocopies) vya habari iliyokuwa imeandikwa na gazeti la CCM la Mzalendo kuwa ati CUF ilikuwa imetia kinyesi kwenye visima vya maji huko Tabora! Kazi ya Mlaki ilikuwa ni kuzunguka kijiji hadi kijiji akigawa vivuli hivyo kwa Wananchi; na aliifanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa hadi pale alipotaka kupigwa na Wananchi wenye hasira kali katika kata ya Kifula.

  Lakini tusisahau pia kuwa ni CHADEMA ndiyo ilihujumu juhudi za vyama vya upinzani kuwa na utaratibu wa kuachiana majimbo kutokana na nguvu ya chama katika jimbo linahusika. Katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto, CUF iliiunga mkono CHADEMA kutokana na ukweli kuwa katika jimbo hilo CHADEMA ilikuwa inaonekana kuwa na nguvu kuliko CUF. Jambo la kushangaza ni kwamba katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tunduru ambako CUF ina nguvu zaidi kuliko CHADEMA kwa kila hali, chama hicho bila kuzingatia umoja uliokuwepo kiliamua kumweka Shaibu Akwilombe apambane na mgombea wa CUF, Rajab Mazee! Hali hiyo ilijitokeza pia Mbeya vijijini na Busanda, ambako kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005, CUF ilikuwa na nguvu zaidi kuliko CHADEMA kwa kuwa ya pili nyuma ya CCM kwa wingi wa kura.

  Katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime, pamoja na kwamba tayari CHADEMA ilikwisha kuvunja makubaliano ya umoja, kwa kuzingatia kuwa jimbo hilo hapo awali lilikuwa mikononi mwa CHADEMA, CUF ilichagua kutoweka mgombea na kuwataka wanachama wake wampigie kura mgombea wa CHADEMA. Sasa hapa chama makini ni kipi? Siku zote hoja ya CHADEMA kujitoa katika umoja wa vyama vya upinzani ni kuwa ati hawawezi kufanya kazi na vyama ambavyo siyo makini! Ni umakini gani huo wanaouzungumzia?

  Kwa bahati nzuri au mbaya, hawa wenzetu historia inawatuhumu vibaya. Ni hawa hawa ndiyo walioisambaratisha Kamati ya Kuratibu Mabadiliko ya Katiba Tanzania (KAMAKA) mwishoni mwa miaka ya tisini iliyokuwa inajumuisha takriban vyama vyote vya upinzani, na hivyo kuua kabisa nguvu ya pamoja ya kudai katiba mpya. Ndugu zangu wana-habari, je, hiki kweli ndiyo chama ambacho kwa dhati kabisa mnaamini ni mbadala wa CCM?

  Kati ya wagombea waliofanywa wahanga wa mwenendo huu mbaya wa vyombo vya habari, walau Dr. Jakaya Kikwete ana bahati kuwa Chama chake kina nguvu kubwa ya kiuchumi ilinayokiwezesha kuwa na sauti katika baadhi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na baadhi ya makada wake, au vile kinavyovimiliki chenyewe moja kwa moja.

  Walau basi kupitia vyombo hivi kampeni yake inapata fursa za hapa na pale kupamba kurasa za mbele za baadhi ya magazeti. Lakini ni kitu gani kimetokea hadi 'uswahiba' wake mkubwa na vyombo vya habari uliojidhihirisha katika uchaguzi wa mwaka 2005 ukatoweka kwa kasi? Mbeleko ile imekwenda wapi ukizingatia kuwa Kikwete ni yule yule tuliyeambiwa kuwa ni 'CHAGUO LA MUNGU'?

  Tatizo kubwa liko kwa Profesa Lipumba. Kwa kuwa Lipumba ni Muislamu, tena Muislamu anayetekeleza majukumu yake ya kiibada, na kwa kuwa sehemu kubwa sana ya Waislamu wa kawaida wa nchi hii wamelazimika kukiunga mkono chama chake kutokana na sera yake ya 'HAKI SAWA KWA WOTE', Lipumba amejikuta katika mazingira magumu ya kukosa 'marafiki' wenye nguvu katika medani ya vyombo vya habari. Aidha, kwa kuwa chama chake ni cha 'Wananchi' kwa kila hali – wengi wao hata uwezo wa kuwanunulia watoto wao madaftari ya shule kwa wakati ni tatizo – uwezekano wa kuwa na makada wenye uwezo wa kumiliki vyombo vya habari haupo.

  Uzuri ni kwamba, hata historia ingepindishwa vipi, ukweli utabaki pale pale kwamba Waislamu walikuwa ndiyo wenye mchango mkubwa katika kuasisiwa kwa chama cha TANU na katika mapambano ambayo hatimaye yalileta uhuru wa Tanganyika.

  CCM ni zao la TANU NA ASP, kwa maana hiyo siyo kosa kudhania pia kuwa Waislamu walikuwa na mchango mkubwa katika kuzaliwa kwa chama hicho. Badala ya kukimbilia kuituhumu CUF kuwa chama cha udini kwa kuwa tu kinaungwa mkono na Waislamu wengi, changamoto kwa wasomi, wana-habari na wachambuzi ni hii: HUKO CCM KUMETOKEA NINI HADI WAISLAMU WANAPAKIMBIA?

  Tatizo kubwa la Tanzania ni umasikini wa Wananchi. Nchi yenyewe kama pande la ardhi si sahihi kuiita maskini kwa kuwa imejaaliwa raslimali nyingi sana. Watanzania ni masikini sana kwa sababu nchi yao imeongozwa hovyo sana kwa muda wa miaka 49 mfulululizo.

  Raslimali za nchi zikitumika vizuri umasikini utaondoka na pamoja nao yataondoka matatizo ya ajira, uhalifu, elimu duni, miundo mbinu hafifu, afya mbovu, njaa, rushwa, nakadhalika.

  Japokuwa wana-habari wetu hili hawalikubali, lakini ukweli unabaki kuwa Profesa Lipumba akiwa kama mchumi aliyebobea wa kiwango cha kimataifa, ndiye pekee mwenye uwezo wa kutuvusha kati ya wagombea wote wanaogombea urais kwa sasa.

  Ukilinganisha na wagombea anaochuana nao, wasifu wa Lipumba katika nyanja za uchumi na uzalendo kwa nchi yake unang'ara kama mti wa Krisimasi, na hilo hakuna anayeweza kupingana nalo! Hebu tutazame haya machache:
  Lipumba ni mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuangalia jinsi ya kuondoa umasikini katika nchi za dunia ya tatu. Angekuwa ni mtu asiye na uzalendo wa dhati kwa nchi yake, hivi sasa angekuwa huku na kule duniani akijikusanyia 'mapesa' na kuishi kitajiri na nyie 'wavimba macho' wa Tanzania mtajua wenyewe!
  Japokuwa Lipumba ndiye aliyesimama na kujenga hoja katika Bunge la Marekani (Congress) akitaka nchi za dunia ya tatu ziondolewe mzigo wa madeni, jambo ambalo lilitekelezwa, hata siku moja sijamsikia akijipigia debe kwa mafanikio hayo. Kwake yeye suala muhimu ni kwamba madeni yameondolewa, sasa nani anapewa sifa kwa mafanikio hayo siyo jambo la msingi
  Wakati wa mtikisiko wa kifedha wa nchi za mashariki ya mbali na kusini mwa bara la Asia, Lipumba ndiye aliyekabidhiwa jukumu na Umoja wa Mataifa la kuyashauri mataifa husika ni kitu gani wafanye. Sote ni mashahidi kuwa ndani ya miezi michache uchumi wa mataifa hayo ulikuwa umerejea kwenye hali yake ya kawaida.
  Namibia ilipopata uhuru, Lipumba ndiye aliyeitwa kulisaidia Taifa hilo kuunda mfumo wake wa fedha.
  Museveni wa Uganda, pamoja na uswahiba wake na CCM hakusika kumwomba Lipumba amshauri ni nini Uganda ifanye ili kuisadia nchi hiyo kukarabati uchumi wake.
  Brazil, moja ya mataifa makubwa sana kiuchumi hivi sasa duniani haikusita kumtafuta Lipumba awashauri wafanye nini na ardhi yao ya ziada ili ichangie kikamilifu katika uchumi wa nchi hiyo.

  Naamini kuwa pamoja na jitihada za wana-habari wetu kujaribu kufinyanga akili zetu ili twende kupiga kura na 'KUJIUZIA MBUZI KWENYE GUNIA', Watanzania wanajua tatizo lao ni nini; na watapiga kura wakiwa na dhamira ya kujikomboa. Wito wangu kwa wana-habari ni kwamba, bado hatujachelewa, tuwape wagombea wote nafasi sawa na kisha tuwaachie Wananchi wafanye maamuzi yao.

  Mwandishi wa makala haya, ni msomi wa shahada ya uzamili ya sayansi ya kemia na elimu pia ni mwanasiasa mahiri aliyeshiriki kuandika manifesto ya chama cha CUF mwaka 2000 ambayo ilichapishwa katika mfumo wa gazeti na baadaye kitabu.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  To me crap as usual. No comments
   
 3. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  umesoma lakini wewe..??
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ndio nimesoma so what? au kwa kuwa kaandika Juma Killaghai basi nitoe credit kwa upuuzi?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ninachokijua ni kimoja tu kuwa CCM na CUF wanalala kitanda kimoja baada ya kufunga ndoa, period.
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  nilimaanisha umeisoma hii thread yoote.. mimi sikuweza nimeona malelezo mengi! BTW!!! politics it is not my swagger kabisaa!!
   
 7. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni vema mwandishi angeficha aibu yake kwa kutojumuisha hayo maneno yenye rangi nyekundu.Usomi ni pamoja na kuwa objective badala ya kuendekeza subjectivity inayotokana na religious sentiments,or rather prejudice.Tatizo la ndugu yetu huyu sio udhaifu wa CCM bali wa Chadema.Na wala sio CUF itafanya nini bali yale ambayo Chadema haiwezi kuyatekeleza.

  The so-called usomi wa mwandishi umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na udini.Na udini ni moja ya mambo yanayokwaza CUF kuwa chama makini katika siasa za Tanzania Bara.Wasiwasi wa CUF kuhusu Chadema hauna tofauti na ule wa CCM kwa Chadema,except for the fact kuwa CUF inaihofia zaidi Chadema kutokana na mtizamo wa kidini wa CUF unaowafanya waione Chadema kama chama cha Kikristo,ilhali CCM inaihofia Chadema kutokana na msimamo wao (Chadema) dhidi ya ufisadi.

  Badala ya ,mwandishi na chama chake cha kidini cha CUF kujihangaisha na "udhaifu" wa Chadema wanapaswa wakae chini na kujiuliza nini hatma ya chama chao baada ya kushindwa katika uchaguzi ujao (hilo halina ubishi bali kinachosubiriwa ni how bad they will fare).Je Lipumba ataachia ngazi na kutoa fursa kwa mwana-CUF mwingine kuki-transform chama hicho kutoka kikundi chenye ajenda finyu ya udini na "kelele za kuonewa" huko Zanzibar?And talking of Zanzibar,hivi mwandishi anadhani kuwa divisional politics za kisiwani humo zitaruhusu CUF itawale,assuming they win mwaka huu?Je wakishindwa wataitambua serikali ya CCM hata kama wanafahamu kuwa CCM hiyo hiyo ndio iliyochakachua ushindi wao just as it has been done katika chaguzi zilizopita?

  Halafu ni vema ungetafuta namna nyingine ya kuwasilisha mada yako badala ya kuegemea hoja ya vyombo vya habari kumpendelea Dokta Slaa.Angekuwa anapendelewa Daily News,gazeti linaloendeshwa kwa fedha za walipa kodi,lingetamka hadharani kuwa Slaa hawezi kuwa rais wa 5 wa Tanzania?Kwa usomi wako unafahamu kuwa kauli ya gazeti hilo inaweza kutafsiriwa kama msimamo wa serikali iliyopo madarakani?

  Habari Leo,gazeti jingine linaloendeshwa kwa fedha za walipa kodi,liliamua kuweka kando maadili ya taaluma ya habari na ku-dedicate siku kadhaa kuzungumzia "uchumba wa Dkt Slaa".Halafu wewe mwandishi unayejiita msomi bado unasema Dkt Slaa anapendelewa na vyombo vya habari!

  Na katika hoja zako za udini kwanini msimkalie kooni ustaadhi mwenzenu Kikwete aliyawazuga mwaka 2005 kuwa angewapatia mahakama ya kadhi kabla hajawaacha solemba?Tatizo la watu wanaoendeshwa na chuki za dini ni kwamba hata pale Sheikh Mkuu akitumiwa na CCM au rais muislam asipojali maslahi ya Waislam,lawama zitaelekezwa kwa wakristo.Wanaosema udini husababisa upofu wala hawajakosea.

  Na makala hiyo ni uthibitisho tosha kuwa moja ya vikwazo vikuu katika ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili waumini wa dini ya Kiislam ni baadhi ya Waislam wenzao ambao wamebahatika kupata elimu ya juu lakini hawaitumii ipasavyo.Hebu angalia makala ya mwandishi ilivyoanza na kila dalili kuwa ana ufahamu wa masuala mbalimbali duniani lakini alipokuja kwenye local issues akabadilika na kuwa kama "mtu wa mtaani" tu na si msomi.TAMPRO ilijitahidi kuunganisha wasomi mbalimbali ku-address masuala ya Uislamu nchini Tanzania lakini kwa kutumia wasomi badala ya kuwategemea viongozi wa dini pekee.Yayumkinika kuhitimisha kuwa kinachoifanya taasisi hiyo kutokuwa na ufanisi wa kutosha ni kutanguliza anti-Christian agenda badala ya kutumia elimu na taaluma zao kuwasaidia waumini wenzao.

  Anyway,ningeweza kuandika makala ndefu zaidi ya huyo "msomi" wetu lakini haya machache yanaweza kutosha "kumuaibisha" mwandishi huyo msomi anayeelekea kutojua vipaumbele vya dini na itikadi anayoshabikia.Na CUF ielewe kuwa "ndoa yake ya mkeka" na CCM itavunjika mara baada ya uchaguzi.Wanatumika na wanafahamu lakini kwa vile wanaamini ndoa hiyo itazuia "chama cha wakristo" kuingia madarakani basi wapo tayari kuweka rehani nafasi ya kisiasa ya chama hicho.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  najitahidi kuwaelewa na kuuelewa huu waraka mrefu namna hii.
  Nasita sita kusema huu ni nusu utumbo nusu taulo
   
 9. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kilaghai kwa kweli Amenishibisha kwa hoja motomoto Alizoziainisha hapa asante sana kwa kuzidi kutufunguwa macho kwani kuna mambo mengi ambayo tulikuwa hatujui Ametufafanulia kwa hoja safi na za kisomi!!! Hoja zakE ziko wazi kabisa na ukiona mtu anakuja hapa na kuanza kuongea kwa hasira na hoja zilizoshamiri chuki, basi tambua kuwa hoja zakE MWANDISHI zimemgusa yeye na chama chake!! Looo, kumbe slaa anataka alipwe mshahara mkubwa hivyo ikiwa ataukosa urai? Sasa fisadi maana yake ni nini? Lililo nisikitisha zaidi kumbe mgombea mwenza wa chadema ni wa darasa la 7!!! Uuuuuuuwi!!!

  Asante kilaghai naomba nijulisheNI ni wapi mwaka huu Anagombea ubunge ili niweze kuMfanyia kampeni watu kama HAWA ndio WnNaofaa kuwa viongozi!

  Haya wana chadema nasubiri matusi yenu!!!!
   
 10. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ulianza vizuri, lakini umekuja kuweka MIPUMBA hapo katikati (RANGI nyekundu), sasa hivi hatufikirii mambo yanayotugawa tunafikiria vitu vinavyotuunganisha kama watanzania, mfano kuupinga umaskini, harafu wewe unaleta mambo ya dini, hauna maana kabisa!!!!!!!!!!!, ina maana kama waislamu walihusika na uhuru iweje sasa???? kunapointi gani kwenye huu uchaguzi 2010?????, tumia taaluma yako kuelimisha watanzania, na siyo kutugawa kwa makundi eti fulani alipigania sana uhuru kuliko fulani, hiyo ni historia ilishapita sasa watanzania wengi ni masikini wa kutupwa!!!!!!!!!!!! tunalia na viongozi walio tusaliti kwa kupora rasilimali za nchi ama kwa kuhusika wao moja kwa moja au kupitia marafiki zao, tunataka kuona hatua madhubuti zina chukuliwa kiwaziwazi na kwa si kificho na kwa woga.
  Makubaliano ya Dr Slaa na chama chake hayatuhusu, wala darasa la saba halituhusu sisi tunaangalia je Dr anafaa au hafai kuwa kiongozi, na CCM tunaangalia je Dr Kikwete anadhamira ya utekelezaji au ni porojo tu, hivyo ndiyo baadhi ya maswali kwa wapiga kura, na Prof Lipumba si kwa sababu ya uislam wake ndiyo nitampigia kura, ni je anadhamira iliyo wazi ya kutukwamua kiuchumi? kwa ufupi rudi kaipitie hiyo makala yako uilete tena labda tutakuelewa,
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Duniani kuna mambo na hujafa hujaumbika.

  Hivi haya yameandikwa na mtu mwenye akili timamu kabisa kabisa? Hana mtindio wa ubongo au degedege?

  Hawa ndio mambo yakienda vibawa wanaweza kujiuza kwa bei dezo. Kila siku siyo Ijumaa. Sasa kama mambo hayamwendei vizuri Lipumba, Dr Slaaa anahusika vipi? Suala la dini linalikujaje?


  Amenichosha kuliko maelezo. Ngoja nikapumzike. Ila jamaa anahitaji kuonana na psychologist!
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hivi kasoma? kama ni graduate alisaidiwa tu na walimu wake maana kichwani hana chembe ya usomi. Kudadadeki. Kuwa na wasomi design hii kumetufikisha hapa.

  Wametufikisha mahali wanasema bila aibu kuwa hawajui kwa nini nchi yetu ni masikini pamoja na raslimali zote tulizonazo. Kudadadeki.
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Haya yanahusiana vipi na heading ya thread " Vyombo vya habari visipotoshe wapiga kura "
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Divele Dikalame,
  Mkuu mimi nimekusoma na nimejaribu sana kutoacha katikati ili nipate kujua haswa kipi kinakukera au ukweli wa maneno yako kwani pasipo kuelewa ulichoandika na ukweli wake nadhani itakuwa ujinga mkubwa kukujibu.

  Nimefurahi sana na kipande ulichoielezea kuhusu Udini na jinsi bakal;i Muluzi alivyokuwa akizungumziwa kaa Muislaam hali haikutokea kwa viongozi wengine wa Malawi. Sasa kama umeelewa hivyo nadhani rudi tanzania utakuta kjwamba Nyerere alikuwa akisemwa kwa Ukristu wake lakini Mwinyi na JK hakuzungumzwa.. Leo hii Dr. Slaa anazungumzwa kwa Ukristu wake hali Kikwete hazungumziwi kwa Uislaam wake..Je nasema uongo?

  Yawezekana tofauti iliyopo baina ya Malawi na Tanzania ni kwamba wenye nguvu kubwa yaani Wakristu ndio walipiga vita Uislaam huko Malawi lakini hapa Tanzania ni sababu gani haswa inayowafanya ndugu zangu CUF na CCM kumzungumzia Dr.Slaa kama ni mkristu hali mkijua wazi kwamba JK (aloshika Mpini) na Lipumba ni waislaam hivyo inaleta picha ya Udini zaidi ya kuzungumzia sera, uongozi bora na tumaini jipya kwani hawa wote wamekuja na vision yao kuhusiana na Tanzania ya kesho.

  Pili umezungumzia vizuri sana kuhusiana na Kusambaratika kwa Muafakla ulokuwepo baina ya Chadema na CUF kiasi kwamba Chadema waliweza kuweka mgombea wao pale ambapo CUF wamemsimamisha mtu alokuwa na nafasi kubwa ya ushindi. Kama sikosei nakumbuka mwaka 2006 baada tu ya uchaguzi ulopita niliweka hoja inayofanana sana na mfumo huu nikivitaka vyama pinzani kuunganisha nguvu zao na kuachiana sehemu ambazo kila chama kina nafasi ya ushindi. Sasa hapa tunazungumzia Uchaguzi huu ikiwa ni pamoja na uchaguzi mdogo ambao wewe umeutolea mfano. yaani uchaguzi wako ni baada ya CUF kushindwa vibaya bara kutokana na makosa yaliyofanyika mwanzo.

  Na kama uliwahi kuisoma makala yangu nilisema wazi kwamba CUF, Chadema,TLP na NCCR hawawezi kushirikiana vema ikiwa watakubaliana tu Muafaka wa kupeana support badala ya kuunganisha nguvu zao. Hamkusikia kmaziba nyote masikio yenu mkitazama mashali ya vyama mbele ya Utaifa kutounguana. Ni vigumu sana kwa vyama kuweza kukubali matakwa ya chama kingine hata kama ukweli upo wazi. Na nini hasa maana ya demokrasia ikiwa mnaachiana pasi hali kila mmoja wenu anafikira yeye angeweza kushinda!. Leo hii katika Uchaguzi huu mkuu unafikiri Lipumba anayo nafasi ya Ushindi? sasa kama hana kwa nini bado ameendelea kujinadi hali ushindi haupo, lakini muulize yeye kama hana nafasi ya Ushindi au wana CUF uwasikie watakacho sema. NNina hakika kabisa wana CUF wanaamini Lipumba anayo nafasi kubwa ya ushindi kuliko Dr.Slaa.. kana maneno yangu kama nasema Uongo!..

  Mkuu wangu hakuna mahala kuna watawala watatu walioungana au wawili ni lazima mmoja wao akubali kuwa chini ya mwenzake. Waswahili wanasema Madume mawili hayawezi kaa zizi moja na ndicho mlichojaribu Kufanya ktk muafaka wenu wa vyama vya Upinzani kuunda zizi moja lenye madume watano..Chadema, CUF na NCCR hamkutaka ushauri huu nyote mkitaka kupigiana danadana lakini ifikapo golini kila mmoja wenu alitaka kufunga..That is a fact, na hakika yaliyokukuta wewe ni matunda ya kile mlichokipanda, usiwalalamikie Chadema bali vyama vyote ikiwa ni pamoja na CUF ambao wao pia walikuja pinga wagomnbea wa Chadema huko Tarime na sehemu nyingine. Huwezi kulipa mabaya kwa ubaya ulofanyiwa ili iwe haki kisha unakuja dai kuchezewa rafu..Kisasi ni haki tu pale utakapo weza ipata haki ile lakini sii kumtendea mtu vibaya ili mradi naye akose.

  Leo hii kuwalaumu Chadema hali CUF pia walikuja fanya vile vile kama kulipiza kisasi inaonyesha wazi kila chama kilidhamiria kufanya ushenzi kwa sababu kila chama kilijitegemea zaidi ya kukubaliana. Ni hofu hiyo hiyo nilokuwa nayo kuhusiana na Muafaka baina ya CUF na CCM leo hii kwani haiwezekani kabisa CCM wakafikiria maslahi ya Zanzibar kwa mfumo au fikra za CUF kwa sababu ndicho kilichowafanya muwe vyama tofauti from the day one..CUF inahoji yote yale yaliyotokana na kile Baraza la Mapinduzi iliyajenga kwa manufaa ya Wazanzibar hivyo kuibadilisha historia ile ni sawa na kufuta kabisa Mapinduzi ambayo ndiyo yalileta Muungano..Hapa mkuu wangu nakwambia mbele ya matokeo ya Uchaguzi kwamba hili swala ni kubwa kuliko makubaliano yaliyofanyika, sawa na yale makubaliano ya mwanzo baina ya CUF, Chadema, TLP na NCCR.

  Mkuu wangu ifike wakati tukubali makosa, CUF kama chama kilipoteza sana Umaarufu wake bara baada ya kujiingiza sana ktk maswala ya Muungano kuliko uchumi na maendeleo ya Tanzania nzima bali kutaka kuandika Upya historia na mipaka ya nchi yetu..Na hakika bara hakuna mtu alokuwa tayari kurudi nyuma kutazama yaliyopita hali nchi yetu ikizidi kudidimia kiuchumi na kupoteza rasilimali zake kwa Mafisadi. na maadam CUf imekubali kuunda Mufaka na CCM kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano basi watavuna tena kile walichopanda..
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwandishi wa makala hii ni mtu wa ajabu sana, anapinga upuuzi halafu analeta upuuzi zaidi, lakini kwa kuwa tumefahamishwa kuwa ni mwanaCUF inaonekana kabisa ana ajenda za Ki CUF CUF. Ni vema wote tukumbuke kuwa SISI KWANZA NI WATANZANIA, baada ya hapo tuna dini, makabila na rangi mbalimbali. Whether Kikwete ameshindwa kudeliver hili halina uhusiano hata kidogo na dini yake, dini si determinant ya uwezo binafsi wa mtu. Whether Mkapa alikuwa anafanya biashara Ikulu this has nothing to do with his religion, it is him as a person. Si dini yake imemtuma kufanya hivyo. Incapability na dishonest ya kiongozi ina impact kwa watanzania wote regardless of their religions.

  Mwandishi anasema waisliamu ndio walioleta uhuru Tanzania, did they tell him kuwa walikuwa wanapigania uhuru wa uislamu/wasialmu au uhuru wa Tanzania? I give credit to them kwa kuwa historia inaonesha kuwa swali lililokuwa linaulizwa ni kuwa, wewe ni myonge? wewe unanyanyaswa? unapuuzwa? basi twende huku tupigane na wakoloni. Hawakuuliza kama wewe mwislamu, mndengereko au au mpagani.

  Tunafahamu kuwa media za nje huwa zinasema islamic militants, zikizungumzia ugaidi zinazungumzia mashariki ya kati, zikizungumzia umaskini zinazungumzia Afrika, some how media za Tanzania zinaiga. Lakini hazipotoshi, kuiga na kupotosha ni vitu viwili tofauti. Kwa hiyo hatuwezi kusema media zinaleta udini. Wanaoleta siasa za udini na ukabila ni wanasiasa mufilisi ambao hawana hoja za msingi.

  Lakini kwanini tuende mbali kuvisakama vyombo vya habari badala ya kuanza kuwasakama wanasiasa? Nani ni mpotoshaji, wanasiasa au media? We hear a lot of pack of lies from mouths of politicians than in media, may be there is more crap in media but we receive loads of packs of lie from politicians.
   
 16. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  acha unazi wewe kijiba cha roho kitakuua ati CHADEMA walinakili sera za CUF 2005? sasa kama matatizo ya nchi hii yanafanana Slaa aache kuzungumzia kwa vile CUF walichapisha kijitabu? Una wazimu wewe! ati CUF wanasingiziwa kuhusu kuharibu umoja wa vyama vya upinzani! umesahau kifo cha Wangwe sio nani alikuwa mbele kushutumu CHADEMA ati wamemuua? kisa dereva aliwahi kuwa Libya kwa semina ya vijana? Prof. Mapumba sio? nani asiyewajua nyie mlivyo na roho mbaya na msipoangalia hamtapata hata kiti kimoja bara uchaguzi huu! tuambie kwanza Lipumba aka Mapumba analipwa ngapi na CUF na pia Seif analipwa ngapi pia na CUF visiwani na fanya mahesabu ni asilimia ngapi hizo anazolipwa Slaa kama una uhakika ni mkataba umesainiwa weka vidhibiti hapa! na hizo hela za Sabado naona zinakuuma saana kuliko mchango wa RA CUF sio? huo udini wenu ndo umemkimbiza Lwakatare huko kwenu CUF na sishangai mtaendelea kuwa hivyohivyo huku chama kikidorora mkiendelea kulialia ati mbaya wenu ni CHADEMA! Mnaumwa nyie! mmefulia kweli! na mlivyomchukua mb. wa zamani wa CHADEMA kugombea jimbo la Tarime wakati mnajua CHADEMA ina nguvu tuseme nini? au kwa vile CHADEMA wanakaa kimya maana hawana mda mchafu kujibizana na upinzani wenzao bali CCM unawaona wajinga?
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Vyombo vya habari vimenunuliwa na Manyang'au.
   
 18. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Very Goog!!! Asipoelewa basi ana mtindio wa ubongo
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..kusema ukweli haipendezi kabisa vyama vya upinzani vinapoanza kushambuliana.

  ..kama ni mashambulizi ingependeza kama yangeelekezwa kwa chama tawala CCM.
   
 20. F

  Felister JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Everything works together for good for those who are loved by God!

  Kwani si itakuwa vizuri tukipata rais prof wa uchumi? Aiseeee, nimebadili mawazo kura yangu nampigia Prof Lipumba badala ya JK kumbe hata nikimpigia Lipumba ni POUA maana CCm itaendelea kuwepo. Asante kunihabarisha.
   
Loading...