Vyombo vya Habari vinamdhulumu Dr. Shika

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Kupitia mahojiano mbali mbali ya baadhi ya waandishi wa habari na wapangaji wenzie wanaeishi na Dr. Shika tumeweza kujua namna maisha ya dokta huyo yalivyo ya tabu na ikisemekana kuwa dokta huyo hata chakula kwake ni tatizo kubwa sanaa, anaishi maisha ambayo hata mnyama ana afadhali, na hana msaada toka kwa ndugu wala jamaa yake yoyote yule anaishi kwa neema na qudra tu za Mungu.

Sasa geukia upande wa pili, hawa wanao report, kushare na kupost habari za dokta Shika wanapata mamilion mengi tu, mfano Millard Ayo, video zake zote alizopost YouTube zimekuwa namba moja kwenye trending na zimetazamwa na malaki ya watu huku pia wanaomzamini Millard Ayo wakizidi kumwagia pesa za kufa mtu na YouTube wakimlipa mamilion ya fedha.

Sio Millard tu, kuna Mwananchi, Global nk nk. Ambao sasa wanauza sana kuliko wakati wowote kwa kutumia mahojiano yao na mzee huyu, na habari za mzee huyu zina sikika kuliko ata nyimbo na matukio ya wasanii kuliko hata habari za wabunge na Serikali.

Je, kuna namna yoyote mzee anafaidika?

Baada ya muda upepo huu utakwisha na mzee atarudi kuishi maisha yake yale yale ya kushinda njaa na upweke na hapa sijagusia Airtel ambao wametoa offer mpya na wanaiita "u mia tisa itapendeza" hawa nao najua watakua wamefanya uhuni tu, bado wale wa mashati ya 900 itapendeza, bado wale wa stika za magari za 900 itapendeza.

Mungu ana maksudi makubwa na mzee huyu, katujulisha waTanzania, kamtoa chakani, basi tumsaidie huyu mzee, na nyie wakina Millard lipeni fadhila mrudishieni ata asilimia 10 basi ya faida mlizo ingiza kwa kupitia yeye.

Tumsaidie mzee
 
Kweli kabisa kama hilo la airtel nimeliona mapema yaaani wamlipe huyu mzee hatakiwi tenakuishi maisha haya.huyu Mzee. Angepata mtu amsaidie wamlipe pesa zake
 
Kweli kabisa kama hilo la airtel nimeliona mapema yaaani wamlipe huyu mzee hatakiwi tenakuishi maisha haya.huyu Mzee. Angepata mtu amsaidie wamlipe pesa zake
Airtel wapuuzi sanaa, wamefanya utoto sanaa.
 
"Yaani Babu yeye chakula chake ni maji tu, pale bombani anaenda na kikombe chake, basi"

Hii kauli iliniuma sana! Maskini Mzee wa watu, ningekua lawyer ningeforce king mpaka wote wanamtumia kama ngazi wangemlipa!
Hapa nilisikitika sanaa, mzee hua amejifungia tu ndani ata mwezi mzima. Chakula chake ni maji tu.
 
Back
Top Bottom