Vyombo vya habari vina wajibu wa kuandika kwa kina kuhusu Mafuta na Gesi Tanzania

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
WATANZANIA wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu sekta ya mafuta na gesi asili Tanzania kwa kuwa ni rasilimali mpya ambayo ndiyo kwanza imegunduliwa.

Kwa msingi huo, wanategemea zaidi kupashwa habari kupitia vyombo vya habari, hususan vya ndani, ili kuelewa manufaa ya rasilimali hizo na namna watakavyonufaika nazo wao na vizazi vijavyo.

Kutegemea taarifa za vyombo vya habari vya nje hakutaweza kutoa taswira chanya katika suala hili muhimu.

Tasnia ya habari tunaaminishwa kwamba ni muhimili wa nne wa Dola kwa sababu ndicho kiungo baina ya mamlaka na wananchi, kwani wanahabari ndio wanaopaswa kuisemea jamii ili mamlaka husika ziwezi kujua wapi kuna tatizo zichukue hatua.

Soma zaidi hapa => Vyombo vya habari vina wajibu wa kuandika kwa kina kuhusu Mafuta na Gesi Tanzania | Fikra Pevu
 
Tunashukuru kwa Makala nzuri ila sina hakika sana kama watachangia maana wako bize na majina ya ma dc
 
Vyombo vya habari ambavyo tuliamini ni vya kiharakati siku hizi navyo vinavuta bahasha.. Huko kwenye gesi kuna jipya gani zaidi ya sarakasi tu? Watu wanataka mahelaaa braza..
 
mkuu hawa waandishi wa habar wa bongo ni makanjanja tu, yaani wamekaa na vitambi vyao wanasubiria kuletewa habar kutoka kwenye blogs. haraf pia uzalendo kwa waandishi wetu ni sifuri, wepesi sana kuhongwa.
 
Back
Top Bottom