Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,475
- 34,515
Wimbi la wanasiasa kujimilikisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini limekuwa ni utamaduni unaoelekea kuzoeleka.
Waasisi wa utamaduni huu ni kundi la WANAMTANDAOambao walihusika kwa kiwango cha hali ya juu kuweka wateule wao madarakani kabla ya kuja kusambaratishwa kwa maslahi ya nchi. Nakumbuka nikiwa katika semina ya Wasanii na waandishi katika mapambano dhidi ya Rushwa pale Njuweni Kibaha mnamo mwaka 2005 mwanzoni, alipita katika hoteli hiyo Waziri (wakati huo) wa Mambo ya Nje ambaye alikuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Alisimama na msafara wake kusalimiana na Naibu Mkurugenzi wa TAKURU (enzi hiyo) Bw. Edward Hosea. Nilishtushwa na utitiri wa waandishi wa Habari katika msafara wake. Nilimuuliza mwandishi mmoja tuliyekuwa naye Semina hiyo akaniambia kwamba Mheshimiwa amekuwa anawakirimu Waandishi wa habari ambao wanaambatana naye kwenye ziara zake.
Alinijuza kuwa Waandishi wameanza (kipindi hicho) kuambatana na wanasiasa ambao wameonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi za juu ya nchi yetu. Hivyo kwa tafsiri yangu naamini kuwa tangu wakati huo waandishi waligundua shamba la mavuno kupitia siasa. Ikumbukwe ndicho kipindi ambapo waandishi wengi wa makala walitumia kalamu zao kama visu kuwachinja wale wote walioonyesha ni tishio kwa watu wao.
Nkumbuka mmiliki wa Habari Corporation enzi hizo bwana Jenerali Ulimwengu alijitahidi kuwakusanya waandishi wa makala nguli enzi hizo kama Privatus Karugendo, Mihangwa, Salva, Maggid na wengineo ambao walitumia kalamu zao kuibua hoja na vioja katika makala zao. Rais wa wakati huo Benjamin Mkapa alionekana dhalili mbele ya media naaliripotiwa kwa heshima ya urais wake lakini alikuwa anakosolewa vikali na waandishi walioonyesha tayari kuegemea upande unaowalipa.
Kuna pagemaker mmoja wa media house kubwa hapa nchini aliwahi kuniambia kwamba alikuwa anashuhudia namna wanasiasa walivyokuwa wanapishana kwenye chumba cha mhariri wakija na bahasha huku wakitoka bila bahasha hizo. Kipindi hiko vyama vya upinzani walipata nafasi finyu kutangazwa kwenye vyombo vingi vya habari, magazeti yaliyojitutumua kama Majira la Business Times Ltd walidhoofishwa kwa mbinu chfu sana. Nakumbuka (nilipewa tetesi na insider) Majira wakati ofisi zao zipo jirani na RahaTowers walikuwa ni newsroom iliyojaa wandishi makini waliletewa bili ya kodi kutoka TRA kwa shinikizo la Waziri mkuu wa siku hizo (Sumaye) ambaye moja ya mashari aliyotoa kwa mmiliki wa magazeti hayo ni kuwa aache kumwandika vibaya na akaletwa mwandishi ambaye alikuwa anafanya monitoring ya kipi kitoke na kipi kisitoke... Hali hii ilipelekea waandishi wengi kukimbia na hata gazeti kuporomoka...
Tuje katika zama hizi sasa. Hakuna asiyefahamu nguvu kubwa aliyoitumia bingwa wa rushwa nchini ya kuvimiliki vyombo vya habari vimtangaze yeye na watu wake ambapo alitumia mbinu ile ile ya kuwachafua wengine. Ikumbukwe kwamba Hata mitandao ya jamii mingi ilikuwa na bado ipo chini ya payrol yake. Na kinachofanyika sasa ni kwamba kikundi cha matajiriwamejiunga pamoja kuendesha mapambano dhidi ya serikali ambapo waandishi waliosomea na kupata maelekezo maalumu wamekuwa wakiandika taarifa kwa mtindo wa magharibi wa kuponda na kujenga picha hasi kwa kila serikali inachokifanya kwa watu wake.
Wanasiasa wengi sasa wanamiliki mseto wa wanahabari na kila wanapokwenda wanaongozana nao. Na ijulikane kwamba Waandishi wengi walioajiriwa kwenye vyombo vya habari wanalipwa mara mbili mbili yaani kutoka vyanzo vya habari na mishahara. Waanzilishi wa mchezo huu waliowengi sasa ndiyo waliounda TEF na wanadumisha utamaduni
Nani anailipa TEF na inatoa wapi pesa za kuendeshea shughuli zake? hiyo siyo siri tena ambayo jukwaa la wahariri wamekuwa wakiimwaga. Nani alitoa fedha ya kupeleka Jukwaa la Wahariri kuchunguza kifo cha marehemu Chacha Wangwe? Kwa nini Kubenea alisisitiza kuwa taarifa ya kuvamiwa na mapanga kule makaburini isiandikwe? Haya ni maswali ambayo wapo watakaoyajibu mbeleni. Kwa nini Jukwaa la Wahariri na kusiwe na ushirikishwaji wa senior jurnalists? Kwa nini Jukwaa hili lilipata nguvu kubwa pale Sakina Datoo alipokuwa under The Guardian Limited? Tujiulize MOAT ni NGO au kampuni binafsi? kwani hakujawahi kufanyika uchaguzi wala mabadiliko ya kiutawala tangu ianzishwe. Katibu Mtendajiwake ndugu Mhanikaambaye namfahamu binafsi amekuwa hana nguvu zaidi ya kufuata maelekezo. Gazeti Mwananchi ambalo lipo chini ya Mwananchi Communications inayomilikiwa na Agakhan Foundations ambayo inamiliki Nation Media nchini kenya, gazeti hili limekuwa chini ya uangalizi wa Nation Media hata wahariri watendaji wengi wanatoka nchini Kenya. Na ikumbukwe kuwa Kenya haina mahaba na Tanzania kwa sababu za kiuchumi.... Taarifa nyingi zinazotoka Mwananchi Newspaper niza kung'ata na kupuliza. Hawaungi mkono sera za kitaifa. Siwezi kuzungumzia magazeti ya Uhuru na Tanzania Daima ambao sera zao zinajulikana wazi. Nakumbuka kesi ya Mzee Msendo hadi kufungwa kwake miaka mitano gerezani kupitia mpango mahsususi uliosukwa na wakubwa fulani mmoja serikalini na mwingine private sector. Nakumbuka Nilikuwepo The Guardian ambapo Mhariri wa Sunday Observer alitimuliwa kazi kwa kosa la kuhoji matumizi makubwa yaliyofanywa na msafara wa Makamu wa Rais (enzi hizo) marehemu Omari Ali Juma ambaye mmiliki wa chombo hiko alikuwa katika msafara huo...
Mitandao mingi ya kijamii imenunuliwa na kundi la hawa king makers ambao wanataka mtu wao apate nafasi ya urais ili kulinda maslahi yao. Ukitoa Jamii Forums pekee ambayo attempt nyingi imefanyika kuidhoofisha kimapato ili kutengeneza demand ya kununulika na wakashindwa, vyombo vingine vilijikuta vimeangukia kwenye mifuko ya wanasiasa. Naongelea Tanuru la Fikra ambapo mmja wa wamiliki wake amekuwa ni Socia media strategist wa Team L....
Hivi leo private media kwa asilimia zaidi ya 90 zimekuwa ni majukwaa ya kuipinga serikali katika juhudi zake za kutekekeza sera zake. Ifahamike kwamba kama media inakubali kutumika na maadui wa maendeleo basi ni rahisi kuiingiza nchi katika sintofahamu kubwa. Turejee kumbukumbu ya vita iliyopelekea mauaji ya kimbari Rwanda ambapo media ilihusika kwa kiasi kikubwa. Pia ikumbukwe katika miongoni mwa wahstakiwa wa kesi ya mauaji yaliyotokea Nchini Kenya baada ya Uchaguzi mkuu ambapo inaripotiwa mauaji yalijiri 2007-2008 alikuwepo mwandishi wa habari. Ikumbukwe Waandishi hawabebisilaha zaidi ya kutumia panga na nyembe za kalamu zao.
Leo lolote litakalotamkwa na kiongozi wa nchi ama wenye dhamana mbali mbali, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kupotosha nakutengeneza review zinazoegemea upande mmoja.
Niseme wazi kwamba vyombo vyetu vya habari vinakosa uzalendo na vinaangamiza vikra na mawazo chanya ya wanchi kwa nchi yao hivyo kuwalisha matango pori na uongo unaoenda kuligharimu taifa.
Waandishi kama Paschal Mayala ambao binafsi nawafahamu wamekuwa wachache mno kwenye jamii ambapo inahitajika kuwa na waandishi huru wanaoweza kusema ukweli na hata kusimamia maslahi ya nchi.
Mkiacha kusema ukweli basi ukweli mliouficha utakuja kuwahukumu.
Simamieni maadili ya kazi zenu.
Nchi kwanza