Vyombo vya Habari Vimeihujumu na Kuipuuza Chadema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyombo vya Habari Vimeihujumu na Kuipuuza Chadema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, May 13, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maandamano yanayoendelea mikoa ya Kusini yamekosa mvuto na msisimko na kile kinachoelezwa kupuuzwa na vyombo vya habari magazeti na Television. Ni gazeni moja tu la Tanzania Daima ndio limekua liki ripoti kila mara nalo hatoi ukurasa wa mbele! Tofaut na maandamano ya kanda ya Ziwa yalileta msituka mkubwa hasa kwa Serikali ya Kikwete safari hii imekua tofauti na hata Viongozi wa Chadema ambao wako kwenye maandamano wameshangaa kuona mwitikio ni mdogo! Wataalam wa mambo ya siasa wanasema suala la Chadema kuandamana limezoeleka na sio jambo jipya kwa Watanzania.
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Wewe unataka mwitikio toka kwa vyombao vya habari wakati Chadema wanapata mwitikio wa wananchi. Unadhani CCM na serikali wanapata mshtuko kwa sababu ya vyombo vya habari au kwa sababu ya nguvu ya Chadema? Hatujutangazi lakini muulize Anna Makinda siku ya msiba kijijini kwake alipoteza wanan CCM wangapi kwenda Chadema? Mambo yanafanywa kimkakati sio ya Nape Nnauye na Mukama kubishana mbele ya vyombo vya habari. AIBU
   
 3. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watu wa kusini hawajawahi kuwa na maandamano yanamna hii, kwa hiyo hakuna walichokizoea,
  kama muitikio ni mdogo ndio maana CHADEMA wameenda uko ili kuwaamsha, ipo siku kutakuwa na
  muitikio mkubwa sana.

  Ni sawa na kwamba, mwaka 2005 Chadema ilipata wabunge watano wakuchaguliwa (muitikio ulikuwa
  mdogo), mwaka jana zaidi ya ishirini (good response, si ndio). Wakati Chadema wanaanza operation
  sangara mwaka 2007 hakuna aliyetegemea ingezaa matunda makubwa ya mabadiriko kanda ya ziwa.
  Kanda ya Ziwa CCM itakuwa chama cha upinzani dhaifu sana baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

  Kusini watabadilika, DR SLAA anasema maisha ya watu wale ni ya dhiki sana bila sababu za msingi,
  elimu duni, hakuna huduma za afya, nyumba za manyata, mfumo wa elimu kama wa karne ya tano.
  Mambo haya hayahitaji wanahabari kuyaelezea,muda si punde watabaini kwamba ni kweli
  CCM ndio chanzo, hapo ndio watakapoanza kuandamana bila ya DR SLAA, Mbowe wala ZITTO.

  Ujue hayo ni maandamano hatari zaidi.
  Karibu
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Cdm si chama cha promotion. Cdm haina marketing meneja kama mlivo ccm. Nlipozaliwa sikuona television yoyote ikifanya promosheni kuwa ukisoma sana utakuwa mhasibu,ila mwenyewe kwa kujua kuwa bila uhasibu Gsana hana amani moyoni,nlitafuta mwenyewe na kuipata,ndo maana pia leo naweza kufungua thread za jf na kuzisoma alafu nkajibu,ningesubiri TBC/TvT waje kwetu kilometa 9000km kutoka tbc1 mikocheni hadi leo nsingejua kusoma wala kuandika. Ivo ivo kwa journalists,walimu,daktari,wakili,businessmen na wote uwajuao,hawakuitwa wala kufungwa mnyororo ni tu ile juhudi binafsi. Ivo ivo,cdm haifanyi promo,hatakayeitaka ataitafuta. Kwa kuwa mzee wangu makamba senior alikuwa mnukuu biblia,na amevuliwa gamba,kwa kuwa mi sina gamba naomba jf itengue kanuni kwanza ili nivae miwani ya makamba na kunukuu biblia, "yeyote anayetaka ufalme wa Mungu,na abebe msalaba wake anifuate",(IODORUM NAZAREUM REX IESUS). Beba msalaba wako uifuate cdm,saa ya ukombozi ni sasa!
   
 5. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  changieni kwa hoja kabla VIWAVI hawajavamia humu. :majani7:
   
 6. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wimbo wenyewe ni ule ule leteni habari mpya, waandishi wa habari wataandika. Kila siku maandamano yasiyo na tija kwa wananchi halafu mwataka waandishi waandike! Wasomao gazeti lenu la Tanzania Daima watapata habari, magazeti mengine wnataka ulete habari mpya katika jamii.
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Unao uhakika ni kweli hakuna muitikio wa wananchi?,Kama ni kweli thibitisha.
  Picha tumeziona humu JF wote ni mashahidi wingi wa watu sasa huyu jamaa ni anataka tumuamini?sio kila utakachoandika tukakiamini-jitetee
  Sio kweli kuwa wale wanaohudhuria maandamano ndio wanaoiunga Chadema mkono,wapo wengine wamekosa nafasi kwa sbb mbalimbali hivyo Kama ukichukulia uwingi wa watu ktk maandamano kuwa hao tu ndio wanaoiunga Chadema mkono tu utakuwa haujafanya usawa
   
Loading...