Vyombo vya habari Tanzania vinakwama wapi kwenye habari za Kimataifa?

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Katika taarifa za habari za kimataifa vyombo vya habari vya Tanzania viko nyuma sana. Ni kawaida kuangalia taarifa ya habari na kusiwepo habari za kimataifa hata kama kuna matukio makubwa yametokea duniani.

Star Tv kidogo wanajitahidi kutoa habari za kimataifa nazo kuna kipindi zinasua sua au zisiwepo kabisa. ITV hata habari za michezo kimataifa hakuna kabisa.

Star tv walikua na kipindi cha "Anga za kimataifa ambacho siku hizi hakipo"

Media za Tz zibadilike tusijifungie ndani tu, tawahabarishe wananchi matukio mbalimbali yanayoyokea duniani. Wengi wanapenda kufuatilia habari za mataifa mbalimbali japo hawana access na channels za kimataifa kama CNN, BBC, France 24 nk au lugha ya malkia inaleta shida.
 
Back
Top Bottom