G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Vyombo vya habari vya Tanzania ni vya hovyohovyo na vilivyojishikiza kwenye uoga, umasikini na usaka tonge wa hali ya juu!
Yaliyofanyika Zanzibar ni mambo ya kipuuzi kuliko maelezo! Ali Mohamed Shein ametumia mfumo kamili wa udikteta kujitwalia madaraka huku vyombo hivi vya habari vikimpamba na vingine vikiishia kujaa uoga wa kuuelezea ukweli!
TV zimeonyesha live tukio la kuapishwa kwa kiongozi huyo ambaye uchaguzi wake haujahakikiwa na chombo chochote kile! Umejaa hila, propaganda na kuminywa kwa haki kusikoelezeka.
Badala yake vyombo vya habari vilitakiwa kulaani vikali kitendo kilichofanyika Zanzibar na siyo kusifia upuzi hadharani! Kwa hili vyombo vyetu vya habari vimepotoka sana! Kwa kifupi hatuna vyombo vya habari bali kivuli tu cha vyombo vya habari!
Sisi wadau wa haki tunalaani kitendo kilichofanywa na vyombo vyetu vya habari na wana habari na tunaanza kuvipuuzilia mbali!