Vyombo vya habari Tanzania na hatma yetu

Kwa Tanzania na pato lilivyo dogo, wasomi wakiwa na watoto wengi tunaongeza white-collar crime (a crime committed by a person of respectability and high social status in the course of his occupation).

Mfano ni BOT, Richmond nk.

Bin Maryam,

I like the definition of white collar crime that you have availed us.

It is a white collar crime, is it not, that 50 years after Independence our people are poorer than they were when we started. You don’t have to look far to see this. Look at people that scramble for water in the Msimbazi Creek! Look at the many men and women that walk from Kimara to Kariakoo because they cannot afford to board a bus! Look at all the children that sit on the floor of their classrooms! Look at the patients that sleep three to a bed in our municipal hospitals!

Who, may I ask, is committing this white collar crime? Who are the white collar criminals? Is it not the people that have lorded it over us all this time, and want to continue to do so?

It is, I submit, collaboration with white collar criminals to vote for the same group!


 
Ni dhahiri kwamba baadhi ya vyombo vya habari huko nyumbani vimeshachukua msimamo wa kukipendelea chama tawala CCM.Kwao,habari ni zile zinazoihusu CCM tu,na lazima ziwe habari za kupendeza machoni au/na masikioni.Hatuwezi kuyalaumu magazeti kama Uhuru na Mzalendo,au Redio Uhuru (kama bado ipo) kwa vile vyombo hivyo vya habari vinamilikiwa na CCM.

Lakini haivumiliki kuona TBC,taasisi inayoendeshwa kwa fedha za walipa kodi pasipo kujali itikadi zao za kisiasa,ikielemea upande wa CCM.Awali niliposikia Tido Mhando ameteuliwa kuwa bosi wa taasisi hiyo ya habari nilipata matumaini makubwa hasa kwa vile kabla ya uteuzi huo,Tido alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),ambalo kwa hakika ni "mwiba mchungu" kwa serikali.Kwa BBC,cha muhimu ni habari na sio kujikomba kwa chama tawala.Wakati wa uongozi wa chama cha Labour,BBC ilijikuta mara kadhaa ikigongana na serikali huku ikituhumiwa kuwa habari zake zinalenga kuikosoa serikali ya chama kilichokuwa madarakani kwenye takriban kila jambo.


Huko nyumbani tatizo lina sura mbili:KUJIKOMBA na UOGA.Baadhi ya vyombo vya habari vinajikomba kwa watawala kwa sababu wanazojua wao wenyewe.Hili nalihusisha zaidi na legacy ya utawala wa chama kimoja ambapo kiongozi alikuwa mithili ya mungu-mtu.Habari za kiongozi sharti ziwe nzuri,awe amepongezwa au kupongeza,ametunukiwa nishani,ameng'ara katika suala fulani,nk.Lakini madudu yanayofanywa na watawala wetu ni off-limits.Vioja vinavyofanywa na waheshimiwa wetu wanapokutana Dodoma kwenye vikao vya Bunge havipaswi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari labda awe ni mwakilishi wa chama cha upinzani.

Tatizo la pili ni hilo la uoga.Sijui uoga huu unatoka wapi.Ingeeleweka kama habari husika zingekuwa za kutunga.Lakini kuna haja gani ya kuwanyima wasomaji/wasikilizaji haki yao ya msingi ya kuhabarishwa matukio mbalimbali yanayowahusu wanasiasa na viongozi wetu kwa vile tu habari hizo "hazitowapendeza" vigogo hao?

Kibaya zaidi ni pale hata habari zisizohusiana na maadili (kufumaniwa,ku-cheat,kutelekeza familia,nk) nazo zinaingia katika mkumbo huo.Na wakati mzuri wa kushuhudia upendeleo huu wa wazi ni katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.Inaelezwa kuwa jamaa wa TBC waliamua kuonyesha sehemu ya juu ya mwili wa Dkt Slaa katika mkutano wake kwenye viwanja vya Jangwani,jijini Dar hapo Jumamosi.Hofu ya TBC ni kwa watazamaji wao kuona idadi ya watu waliojitokeza kwenye shughuli hiyo.Hivi kwa akili yao wanadhani kuficha idadi ya wahudhuriaji itamkwaza Dkt Slaa kufikia mafanikio yake?Na kwanini wawanyime haki walipakodi wa Kitanzania ambao fedha zao ndio zinaendesha TBC?

Kibaya zaidi,ugonjwa huu unaelekea pia kuvikumba vyombo vya habari vya kijamii (social media) hususan blogu.Haina haja ya kutajana majina lakini binafsi nilisikitishwa kwa baadhi ya mabloga wetu kupuuzia tukio hilo muhimu.Wanajijua,na wanafahamu wenyewe kwanini walifanya hivyo_Ofkozi,nafahamu fika kuwa uamuzi wa kuweka au kutoweka habari au/na picha ya tukio ni uamuzi wa blog husika,lakini ni muhimu kwa bloga kutambua kuwa wasomaji wake wana itikadi mbalimbali,na kuminya baadhi ya picha/habari kwa vile tu "zitawakasirisha wakubwa" ni kutowatendea haki wasomaji wetu.

Ni muhimu kuishi katika dunia halisi (realistically) ambapo lolote linawezekana katika siasa.Huyo Slaa mnayemsusia kwenye vyombo vyenu vya habari anaweza kabisa kuwa rais ajaye wa Tanzania.Je akishinda mtaendelea kukwepa habari zake?Kwanini tusijaribu kubalansi kati ya itikadi na maadili ya kazi,kwa upande mmoja,na mapendezeo yetu binafsi na matarajio ya baadhi ya wasomaji wetu?

Vyombo vya Habari na Upendeleo Kipindi Hiki cha Uchaguzi | KULIKONI UGHAIBUNI
 
TBC SITAITAJA KWANI WAO NILIWATARAJIA. Magazeti ya R. Mengi yanachefua sana kwani wanashindwa kusimamia maadili ya uandishi wanajikomba sana hawa ndugu hivi hawafahamu kwamba uchaguzi unapita? Watanzania ninaomba tutambuo vyombo na waandishi wa ukweli na wa uongo. Sitamfasahau kibonde huyu ni kibonde kwelikweli kwani katokwa na utu wake kwa vijisenti. Ninawapa pongezi mwananchi communication kwa umakini wao. Mengi changamka unapoteza heshima yako au umeamua kuwa mnafiki?
 
JAMIIFORUMS......MAJIRA...MWANANCHI...the list is long...AN-NUUR....AL-HUDA......cant be separated from the fact.....!
 
JAMIIFORUMS......MAJIRA...MWANANCHI...the list is long...AN-NUUR....AL-HUDA......cant be separated from the fact.....!
Mahesabu,
Naona umekosa kazi. Kawaambie wakubwa wako warudishe ile ambulance ya Bugando. Wana hela za kutosha kujinunulia yao.
 
Magezet yote makini yanayoandika habari huru na ku-report bila kuchakachua habari hayapatikani kwenye mtandao.
Yale yanayoandika habari za kuwapamba na kuwafurahisha mafisadi yote yanapatikana ndani ya mtandao.
Wakuu kuna nini? The problem seems to be serious, provide it occur during this time of national election campaign.
 
Nimekuwa nikisoma magazeti yao kwenye mtandao na mara nyingi tu wameshindwa au kwa maksudi wanachanganya ahadi za serikali na za mgombea.Utaonaona wanaandika serikali kufanya hili kwa miaka mitano ijayo,ukisoma zaidi wanasema hayo yamesemwa na mgombea urais wa ccm jk katika kampeni zake blahblahblah...Hawa jamaa wana maanisha nini?kwamba ni mambumbumbu au ndo wameshahakikishiwa JK lazima atashinda na uchaguzi ni geresha tu?Wananikera mno.
 
Kuendekeza njaa na kutokujua wanalofanya....
Tumechoshwa na ahadi zisizo na utekelezaji..embu waje wengine tuone inakuaje..
 
Nimekuwa nikisoma magazeti yao kwenye mtandao na mara nyingi tu wameshindwa au kwa maksudi wanachanganya ahadi za serikali na za mgombea.Utaonaona wanaandika serikali kufanya hili kwa miaka mitano ijayo,ukisoma zaidi wanasema hayo yamesemwa na mgombea urais wa ccm jk katika kampeni zake blahblahblah...Hawa jamaa wana maanisha nini?kwamba ni mambumbumbu au ndo wameshahakikishiwa JK lazima atashinda na uchaguzi ni geresha tu?Wananikera mno.
Hawana tofauti na mhariri wa Daily News.
Nmfahamu Mengi sana tu. hawezi kujipambanua nje ya ccm. muulizeni SAKINA DATOO
 
Back
Top Bottom